Umetafuta Fundi wa gari yako? Uliza chochote kuhusu gari lako

Hivi gari nikitoka tu kujaza mafuta wapi sheli sijui oilcom, basi nikienda maili kadha gari inazima kisha taa za dashbord zote zinawaka, au nikiwa low motion kwenye foleni basi engine inazima, gari hii honda petrol fuel, mtalaam tusaidiane.
Baada ya siku kadhaa gari huwa kawaida bila kuzima. Tatizo lipo wapi ni mafuta machafu au nini, nimefanya service ya engine oil, gearbox, diff, na plug hivi karibuni
 
Msaada kwa mwenye uzoefu wa gari Mazda Premacy DBA-Crew cc1990 size family. Kuhusu ubora spare nk
 
Gari kutoa moshi mweusi ni kiashiria cha nini.?

Na moshi mweusi je?

Piston rings ndio mdudu gani huyu?

NAWASILISHA NA KUTANGULIZA SHUKRANI.
 
Huyu mnaemuuliza maswali atakuwa ni mmasai mbona kala nduki.
Hivi level ya oil ikipungua kidogo sana kuna shida?
Yeyote anaejua tuachane na huyo baba yoyoo
 
Huyu mnaemuuliza maswali atakuwa ni mmasai mbona kala nduki.
Hivi level ya oil ikipungua kidogo sana kuna shida?
Yeyote anaejua tuachane na huyo baba yoyoo
Ilimradi iwe ndani ya ile range kwenye deep stick, haina shida isipokuwa kama unauliza nini kinasababisha oil kupungua kidogo.
 
Gari kutoa moshi mweusi ni kiashiria cha nini.?
Kuwa mafuta hayachomwi vizuri

Na moshi mweusi je?
Kama ulimaanisha moshi mweupe, oil inaingia kwenye chemba ya kulipua mafuta.

Piston rings ndio mdudu gani huyu?
Ndio ring zinazowekwa kwenye piston kwaajili ya ku-seal na kulainisha

NAWASILISHA NA KUTANGULIZA SHUKRANI.
 
Hivi kwanini tairi huwa zinatoa harufu ya kutaka kuungua? Na suluhisho ni nini?
.
Swali lako haliko wazi sana lakini nitajaribu kulielezea.

kama unaongelea harufu ya 'rubber' kuungua hii inaweza kusababishwa na tairi kupata joto linalo tokana na msuguano baina ya tairi na barabara. Tairi huanza kutoa harufu ya kuungua wakati 'rubber' inapoanza kubadilika hali yake, kikemia (molten state). Inawezekana matairi unayotumia hayakutengenezwa kwaajili ya nchi za joto. Hata hivyo sidhani kama hili ndilo tatizo lako.

Sababu ya pili ambayo inaweza kuleta harufu ni ile inayotoka kwenye breki (rotor). Gari ni nzito sana na inapokuwa na mwendo (momentum) inahitajika nguvu ya ziada kuisimamisha. Unapofunga breki, kiasi kikubwa cha nishati hiyo ya mwendo kasi hubadilika kuwa joto. Joto hili huwa kali kiasi cha kuunguza vipande vidogo vidogo vya vyuma na vumbi vilivyo ganda kwenye breki. Hii huleta harufu ya kuungua kwenye matairi.

Sababu kubwa ya hili tatizo la pili linatokana na kufunga breki kwa muda mrefu mfululizo bila kuzipa muda wa kupoa. Mfano pale unapokuwa unateremka mlima mrefu (kitonga) .Utatuzi wa hili ni kusimama kwa muda ili breki zipoe.

Pia inawezekana 'brake pads' zimeisha kiasi cha vyuma kusuguana na kutoa harufu ya kuungua. Pia kuna uwezekano wa breki zako kuwa zime jam, kwahiyo zinakuwa zimebana na kusababisha msuguano unaotoa harufu wakati tairi likizunguka. Hapa inabidi zibadlilishwe.
 
Back
Top Bottom