Umeme kuzimika Airport kwa zaidi ya dakika 1

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,212
6,409
Leo nimeshuhudia aibu kubwa, Airport umeme kukatika kwa zaidi ya dakika 1 kwenye mida ya saa 2 na dakika 13. Je hakuna majenereta automatic? Nimeskia aibu sana. Au ndio mzigo umepitishwa? Hata kiusalama sio nzuri hata kidogo.
 
kuna vitu wanapitisha wewe hebu shtuka Tanzania ni zaidi ya uijuavyo
 
Hapo kuna neno zito. .....mzigo umepitishwa. Hapana chezea Tanzania. Aisee
 
Halafu vigogo bila aibu wanakwenda kujinadi nje ati Tanzania is the perfect place to invest in Africa, imagine hao investors kama ndiyo wameshuka hapo mida hiyo
 
Serikali iko busy na bunge la katiba!! utafikiri zinatengenezwa kanuni za kwenda mbinguni!
 
Yaani hawa watu wanatufanya kila siku tujutie kuwa raia wa nchi yetu bwana yaani wenzetu wanakimbia sisi hata juhudi za kutambaa hatuonyeshi utazani vilema bwana
 
Leo nimejisikia aibu kubwa sana kama Mtanzania
 
Leo nimeshuhudia aibu kubwa, Airport umeme kukatika kwa zaidi ya dakika 1 kwenye mida ya saa 2 na dakika 13. Je hakuna majenereta automatic? Nimeskia aibu sana. Au ndio mzigo umepitishwa? Hata kiusalama sio nzuri hata kidogo.

DK 1??

Unazungumzia airport ya Tanzania au kwa wenzetu? Utakuwa mgeni wewe au unataka kuonesha ulifika airport ....
 
Tumethubutu, tumeweza na sasa tunasonga mbele~Kikwete DHAIFU na MACCM.
 
DK 1??

Unazungumzia airport ya Tanzania au kwa wenzetu? Utakuwa mgeni wewe au unataka kuonesha ulifika airport ....

Airport ni kitu cha ajabu sana mpaka nioneshe nimefika ndugu yangu? Nimeanza kufika Airport tangu nikiwa na miaka 6. Sio kufika tu na kusafiri. Kilichonishangaza sio tu kukatika umeme bali mda mrefu kupita bila kurudi. Ni hatari kiusalama.Sehemu nyeti kama hile inatakiwa kuwa na majenereta automatic. Pale tu umeme unakatika yenyewe yanajiwasha. Huoni hatari hapo? Je watu wakitengeneza hitilafu alafu akapitishwa mtu hatari au mtuhumiwa? Au we akili yako tukio kama hili unawazua nini? Yani how do you make of it
 
C kwamba nilikudharau mkuu, bali mm binafsi nimekuwa mahali hapo mara nyingi na hiyo kadhia imetokea mara nyingi. Kwa jinsi ambavyo nimekumbana na tatizo hilo dk 1 naweza kusema haukukatika kwani ni kawaida sana kukatika hata nusu saa!
Ipo siku ulishawahi kukatika masaa mawli na ushee hv, baadae ikagundulika hata majenereta hayakuwa na mafuta achilia mbali kuwa na ubovu wa hapa na pale !!!!!!!!!

Sorry mkuu kama nilikukwaza, haikuwa nia yangu.
 
Back
Top Bottom