Umejifunza nini kutoka kwenye Uchaguzi wa Marekani?

Uko sahihi, CCM tunapaswa kusoma alama za nyakati!

Mzee Tupatupa
Mzee tupatupa jaribu kuwashauri wenzio wa lumumba kuwa kuna kufa na kuchomwa moto baada ya dhambi ya hapa duniani. Kidhulumu haki na mamuzi ya wazanzibar hyo ni dhambi kubwa uliyowatendea watu wa mungu.

kwa mujibu wa vitabu vya mungu vinasema sauti ya watu wengi ndio sauti ya mungu. Akaenda zaidi akasema panapokuwa na mkusanyiko wa watu wengi nae yupo pamoja nao.

Sasa kwa dhambi mliyoitenda kwa huko zanzibar kwa kugeuza sauti ya mungu itawatafuna mapaka kwenye viunga vya lumumba.
 
1478690267489.jpg
 
sikwetu tu. Hata mataifa yote ya Africa yanapaswa yaige utaraitibu wa uwazi wa tume ya taifa ya uchaguzi wa USA.

Ingekuwa ni Africa na jinsi taifa la marekani lilivyo kubwa basi matokeo yangetangazwa baada ya miezi 6.

Pili vyombo vya ulinzi na usalama vya Africa vinapaswa vijifunze kwa wenzao Marekani.

Utofauti wao na kwetu ni mkubwa sana, kwa wenzetu hatukuona Magari ya washawasha, mapolisi, wajesi na matamko ya uvunjifu wa Amani.

Hapa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na vyama vya siasa vinachakujifunza kwa taifa la America.

Uchaguzi ulikuwa mzuri na wananchi wametumia haki yao kwa kumchagua yule wampendae.
 
Rushwa na dhuluma imewaharibu watu hapa Tanzania na Africa kwa ujumla.

Hata Kama tume ya uchaguzi ingekuwa inaweza kutangaza matokeo yote muda mfupi baada ya kura kupigwa. Ingeweza kuleta machafuko!

Inabidi huku kwetu uwaandae watu kisaikologia kushindwa.

Mfano hapa kwetu wagombea wangekuwa Hillary na Trump halafu wapiga kura wanatazamia Hillary kushinda. Ikatokea kama USA akashinda Trump. Wapiga kura wangeamini kuna wizi wa kura na wangeingia mtaani kutafuta haki yao.
 
Ushindi wa Rais Mteule wa Marekani Donald Trump lazima utufundishe yafuatayo;
-Kuacha kutumia muda mrefu kumtangaza mshindi, wenzetu ni siku moja tu na wao wako wengi kuliko sisi lakini sisi tunatumia siku tatu.

-Anayependwa na wananchi ndiye atakayechaguliwa na ndiye anapaswa kua mshindi, Donald Trump angekua Tanzania asingeweza kua Rais kwa namna yeyote ile kulingana na michezo yetu michafu ya kisiasa.Leo Lowassa angekua Marekani angekua Rais.

- Umaskini sio sababu ya kumfanya mtu kua mzalendo bali Dhamira ya mtu na taifa lake.

-Watawala wasiwachagulie wananchi Rais bali demokrasia ishike mkondo wake waamue wenyewe.
Lowasa angekuwa marekani angekuwa Rais? Labda rais wa chooni!
 
Kwa chadema ndio waligeuza mamuzi ya wananchi huko Zanzibar au chadema ndio wanasimamiaga uchaguzi au wanatawala kilagai kama ccm.

Kweli nimeamini ukiwa kada wa ccm lazima uwe kati ya ile formatio ya 4/1.

CCM wamezoea kugeuza nyeupe kuwa nyeusi. Sasa kwa ulaghai huu na mlivyozoea kuishi kwa mazoea mwisho wenu umekaribia.
 
We must change or be forcefully changed. Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump si mtu wa mchezomchezo. Kwakuwa hakuwahi kuwa mwanasiasa (hazijui mbinu za kisiasa kushinda hata pa kushindwa aka 'goli la mkono') atakuwa mtetezi wa 'demokrasia safi'.

Kama Rais Mteule wa taifa nambari moja duniani lenye nguvu za kiuchumi na hata kivita, Trump atakuwa msikilizaji wa malalamiko ya wale watakaopokwa ushindi wao kwenye kura. CCM lazima tubadilike. Tusitegemee ushindi wa mezani. Tunapaswa kuwatumikia wananchi na kutekeleza, pamoja na kidogo kuteleza, Ilani yetu.

Rais Mteule Trump si wa maneno mengi. Atatenda vya kupenda na kuponda. Atakuwa Rais mchukia 'rafu' za kisiasa popote duniani kwakuwa ni mgeni katika hilo. Atailinda demokrasia popote na kwa namna yoyote. Akilalamikiwa, atawafikia watakaolalamika na wanaolalamikiwa. Atakuwa Kiranja hasa wa dunia!

Huku Afrika, kunakolalamikiwa kama sehemu ya kuminywa kwa demokrasia, kunapaswa kubadilika. Vyama tawala, kama CCM yetu, vinapaswa kubadilika. Under Trump's rule, things will change. They will not be the way they used to be. In that coming momentum, CCM must change. Trump ndiyo kwanza anagonga hodi Ikulu ya Marekani.

Hatujachelewa kujipanga kupata ushindi 'mweupe' usio na mawaa wala hadaa hapo mwaka 2020 na kuendelea. Muda wa CCM kubadilika umefika!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)


Hata mm nimeogopa sana CCM yetu lazima sasa ibadilike haraka sana sana, iwe kama mm au Bashe alivyo, tuache mazoea kama kawaida.. tutafeli sana sanaaa ktk uchaguzi ujao, nimeshtuka sana mm kuhusu Trump alivyo shinda..

CCM lazima sasa ianze kugeukia wananchi kwa haraka sana sanaaa

1: Watumishi wa umma
2: Wanavyuo kwa mikopo haraka sana
3: Wafanyabiashara halali na wazalendo kuwapa hope ya waziwazi
4: Wakulima na wafugaji
5: Kila mbunge CCM ahakikishe anatatua kero sugu za wananchi wake, sio ombi iwe amri ya chama

6: Mh. Rais atimize ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni..

Nasema haya sbb niwe mkweli hali ya maisha ni mbaya sana. CCM lazima tukubali huu ukweli, tutajutia very soon
 
Pamoja na sababu nyingine lakini ukweli utabaki pale pale Mama HILARY kuwa mwanamke kumekatisha ndoto zake za kuwa rais wa 45 na wa taifa kubwa hapa dunia.


Wazungu ni watu ambao wanamthamini sana mwanamke katika mambo mepesi ila siyo mambo mazito kama hili la kuliongoza taifa kama Marekanai.


Wakati mwingine hizi sera za haki sawa kwa jinsi zote hawa wazungu wanatulazimisha sisi tu lakini kwao kuna nafasi ambazo mwanamke hawampatii, kama walivyofanya leo.

Kama Democracy wangekuwa na mtu wa jinsia ya kiume na akawa na sera zenye mwelekeo wa zile za Trump, huu uchaguzi ungekuwa mwepesi sana kwao maana Trump ni mwepesi sana kwa baadhi ya sera na tabia zake, hapa wamarekan wamekosa second option..yaani ni sawa uchaguzi ulikuwa wa mtu mmoja kwao, angali ushindi ulivyokuwa na gap kubwa.

Sera ya Trump ya kutaka kuifanya marekani kuwa more powerful imewaingia wamarekani sana, wamarekani walitaka mtu wa kurejesha heshima ya Marekani ambayo wandhani imepotea na wakakutana na sera za Trump zenye mwelekeo huo.

Kimsingi kilichomshindisha Trump ni baadhi ya sera zake na kuonekana ni mtu ambaye ni muwazi na mkweli.Hawakuangalia tabia zake binafsi kama sisi tunavyofanya.

Swala la nchi kubwa na tajiri mfano China Japani na baadhi ya nchi za Ulaya kumpinga Trump na kumuunga mkono Hilary kiliwafanya wamarekani kuona umhimu wa Trump kwa nchi yao na siyo Hilary. Wanamsemo wao we are Americans..

Kipindi wamarekani wanaangalia nchi yao sisi huwa tunaangalia vyama vyetu.

Nina uhakika huu uchaguzi wa USA ingekuwa ni hapa kwetu lazma ungefutwa tu na kutolewa sababu ya kuwa haukuwa huru na haki kwa sababu tusiyemtaka kashinda.
 
Wachambuzi wa Kibongo bana.

Ukitaka kujua watu waliobobea kwenye mambo ya Ulaya na Soka na mambo ya kiuchumi na siasa, we watafute wachambuzi wa kibongo....
 
Back
Top Bottom