UMEJERUHI MOYO WA MPENZI WAKO NA UNATAKA KUUTIBU?

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
18,760
29,320
Inawezekana kukawa kumetokea kutokuelewana baina yenu, mkaachana. Ukiwa nje ya uhusiano wako, ukagundua kwamba chanzo cha matatizo yote ni wewe. Inategemea umemfanyia nini? Labda umemtukana sana, umeharibu samani zake nk, lakini mwisho wa siku unagundua kwamba wewe ni chanzo cha matatizo hayo ya kutengana.

- KUJERUHI NI KUPI HASA?
Maneno yako makali, tabia zako mbaya, vituko vya kila aina na hasara ulizomsababishia, zinaweza kuwa sababu ya kumjeruhi moyo wake. Majeraha pia yanaweza kusababishwa na jinsi usivyo msikivu kwake, wakati akiwa anaamini kwamba wewe ndiye mpenzi wa maisha yake yote.
Sawa, ameamua kurudiana na wewe, kwasababu anakupenda lakini bado anahisi kama utaendelea na matatizo yako ya zamani. Hakuamini. Anaona anaweza kuwa anatwanga maji kwenye kinu, ambapo ukweli ni kwamba mwishowe maji yote yatamwagika chini.

-UTAJUAJE KAMA UMEMJERUHI?
Yapo mengi, lakini kwa uchache sana, atapunguza mahaba na wewe. Ninaposema mahaba sina maana ya ngono, namaanisha mambo ya kimapenzi – mahanjam - manjonjo.
Anakuwa mgumu kupokea simu yako, hata akipokea hazungumzi maneno ya kimahaba kama zamani. Ukimwambia: “I love you dear,” yeye anaweza kukujibu kwa kifupi: “Ahsante,” tofauti na zamani ambapo alikuwa akikujibu kwa mahaba mazito: “I love you too my sweetie.”
Meseji zako hajibu, hata kama akijibu, atakujibu kwa mkato sana. Anaonekana hana msisimko na wewe. Atakuwa mzito hata kuachia tabasamu akizunguza na wewe, hakuamini sana.
Hakufuatilii sana, mara nyingi anaonekana mwenye mawazo mengi akiwa na wewe. Hafurahii anapokuwa na wewe na hata uchangamfu wake unapungua.
Kikubwa hapo ni kwamba hana imani kama ni kweli umeamua kwa dhati kubadilika na kurudi kwake mzima-mzima! Moyo wake unaendelea kukiri ndani kwamba anakupenda, lakini anashindana na imani kwamba yawezekana usibadilike, anachohofia yeye ni wewe kurudia makosa yale yale!
Kama ukiona dalili zote hizo ujue wazi kwamba bado ana wasiwasi na wewe, moyo wake umejeruhiwa. Kufahamu ni hatua ya kwanza, nzuri na muhimu sana kwako, kwani angalau sasa utakuwa unajua upo kwenye uhusiano na mtu wa aina gani, huku ukiwa makini katika kutafuta suluhisho la tatizo lenyewe.

-ONESHA UNAFAHAMU
Kitu cha kwanza kabisa unachotakiwa kufanya ni kuonesha kwamba umeshafahamu kwamba hakuamini na hana msisimko tena na wewe. Unatakiwa umfanye ajue kwamba unatambua kinachendelea, lakini unakiri kwamba ni haki yake kufanya hivyo, maana ni kweli kwamba mkosaji ulikuwa ni wewe.

-ACHA KUMLAUMU...
Katika makosa makubwa ambayo hutakiwi kufanya ni pamoja na kumlaumu! Hutakiwi kabisa kumlaumu kwamba anakosea kufanya anavyofanya. Lakini kwa vitendo, unatakiwa kuanza kubadilika taratibu huku ukionesha kumhurumia kwa hali aliyokuwa nayo.
Bado kuna vipengele vingine muhimu sana kwako kuvifahamu wakati unapofanya jitihada za kumrudisha mpenzi wako katika hali yake ya kawaida. Kumbuka, wewe ndiye uliyeharibu, hivyo ni wajibu wako kutengeneza.
 
Ka vipi akafie mbele tu..k za bwerere zimejaa mtaani unahangaika kubembeleza moja,kwan hyo yake ina sukari?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom