EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Acheni utani, JF imekuwa ya msaada sana kwangu.
Nakumbuka zilikuwa zimebaki siku chache sana nifunge ndoa. Bestman wangu akawa haeleweki. Nikiwasiliana naye kuhusu mipango ya kwenda kufanya manunuzi (tena kwa ghalama zangu) ananikwepa. Nilipomkumbusha siku ya kwenda rehearsal na kubaini hatuko ukurasa mmoja nikachanganyikiwa. Haraka sana nikamkumbuka mtu mmoja aliyewahi kuniomba mchango wa harusi kwa PM hapa JF. Huyu mtu japo nilimchangia, hatukuwa tumewahi kukutana na wala hatukuwa tunajuana. Roho ikanituma kuwasiliana naye. Jibu lilikuwa, USIPATE SHIDA. Hivyo ndivyo ilivyokuwa JF ikawa imenipa Bestman and Best-friend. Asante sana JF, Udumu Milele
Mkuu nimeipenda hii.