Uliza ujibiwe Kisayansi kuhusu viumbe pori

Je ungependa kujua jambo gani kuhusu viumbe pori waliopo Tanzania na popote duniani ikiwezekana! Lengo ni kupata elimu ya maswala tata yanayohusu wanyama mwitu tukijumuisha maisha yao, tabia zao na mambo mengine mengi!

Karibu tushirikiane kujibu pale ambapo tuna elimu japo kidogo.

Hv mamba anaweza kutafuta windo lake nje ya uwepo wa maj(nchi kavu)?....Lakn pia ni mambo gan yamemfanya awe adapted ktk maj?
 
Hv mamba anaweza kutafuta windo lake nje ya uwepo wa maj(nchi kavu)?....Lakn pia ni mambo gan yamemfanya awe adapted ktk maj?

Mamba ni mnyama kundi la reptilia yaani kundi moja na nyoka mijusi nk. Kwa kawaida mamba huishi katika maji yaliyotulia (still water) au yenye kina kifupi (shallow water). Mamba kama walivyo wanyama wengine ambao wana damu baridi yaani cold blooded ambao kitaalamu zaidi hujumuishwa kwenye kundi la (ectotherms) ie wanyama wasio na uwezo wa kurekebisha joto mwili wenyewe hulazimika kutoka ndani ya maji na kuota jua (basking) nje ya maji. Chakula chake hutegemea na eneo husika lakini Mara nyingi hufakiniwa zaidi kuwinda akiwa majini ambapo pia ana uwezo wa kula viumbe maji kama samaki nk.

Si lazima mamba kuishi majini ikiwa anayapata mahitaji mengine muhimu ardhini lakini maji yana umuhimu sana kwa maisha yao ya kila siku ikiwamo kujikinga na maadui

Tazama video hii: http://youtu.be/SbHtMT62rUY
 
munirah.

Kwanza nakupa pongeza kwa kuacha muda wako na kutupa ilm ambayo Allah amekupa.

Nakuombea umri mrefu watu wengi wazidi kufaidika na darsa lako.

Maswali yangu...

1) Inakuaje dume la simba wakati mwingine linakula watoto wake.

2) Tembo ana zaa mtoto zaidi ya mmoja.

3) Ni kweli Bundi mchana aoni.
 
Last edited by a moderator:
Kuna ndege huwa hajengi kiota ila anataga kwenye viota vya ndege aina nyingine. Na timing ya kuanguliwa mayai yake huwa ni faster kuliko mayai ya ndege mwenye kiota. Huyu ndege mvamizi akitaga harudi tena pale. Ila mayai yake yakianguliwa vile vifaranga vikiwa hata havijaanza kuona vinayatoa mayai ya ndege mwenye kiota na kuyaangusha chini. Hivi vifaranga vikikuwa kabisa na kuruka vinaenda kuwatafuta wazazi wao original. Huu uwezo wa kujua mambo kabla vinaupata vipi na vinatumia mfumo gani kujua na kuwafuata wazazi wao ambao wanaondoka kabisa kwenda kwingine mbali kabisa safari ya masafa marefu
Angalia link

https://youtu.be/SO1WccH2_YM
 
Mkuu kwanza ongera sana kwa kujibu maswali haya , pili nilitaka kujua kwanini wanyama kama mbwa uwa anapenda kumnusa mwenzake sehemu yake ya uzazi hasa dume kumnusa jike, na hii nimeona kwa ng'ombe hata mbuzi aweZi kumpanda kwanza mpaka amnuse ! Nini maana yake?
 
hivi kuna binadamu mwenye macho kama ya paka au mjusi? kuna kiongozi zanzibar alisema mwanasiasa flani siyo mzanzibar kisa ana macho kama paka
 
Kunusa au smelling ni mojawapo ya njia ya mawasiliano miongoni mwa wanyama hasa mamalia! Kupitia kumusa mnyama dume anaweza kujua iwapo jike yupo tayari kupandwa hatimaye kurahisisha tendo la kupandana na kuweza kuwa na tija katka tendo husika
 
Back
Top Bottom