Ulishawahi fanya maamuzi yapi ya kimaisha kwa sababu ambayo ilikuwa 'haielezeki'? Ilikuwa ipi?

Wildlifer

JF-Expert Member
May 12, 2021
1,883
5,191
Nawasalimu katika jina la DP World (chagua muitikio; mkataba uendelee au usiendelee)

Katika maisha huwa tunafanya maamuzi kadha wa kadha kwa sababu zinazoelezeka na kueleweka. Lakini kumbe zipo sababu za undani/faragha/aibu ambazo hazielezeki hadharani lakini zinamantiki.

Niliwahi panga nyumba moja ambayo ilikuwa self contained lakini ni bafu tu, choo kilikuwa nje ambacho tulikuwa tunashare vyumba vitano.

Changamoto ya kile choo ilikuwa unapita koridoni hadi kukifikia nikivuka vyumba vinne.

Sasa shida ilikuwa ukitaka kwenda toilet umebeba ndoo yako ya maji, unakuta wanawake wamerundikana koridoni. Na wale wanawake walikuwa ni mashangingishangingi. Hili jambo lilikuwa linanipa ugumu sana.

Siku moja ninaumwa tumbo, kuwapita mara kwa mara, na tumbo la kuendesha halina siri hata ukiwa chooni, hahaha. Kesho yake dalali wangu nikamwambia hapa majirani wanakelele sana za radio, nitafutie chumba kingine. Na nimekaa wiki 3 tu.

Wewe, ulishakumbana na lipi lisiloelezeka na kukufanya ufanye maamuzi fulani?
 
Aisee kuna kipindi nilikuwa vibaya kipesa wakati huo niko form two.
Nilikuwa nauhitaji wa kufuga sungura hivyo nilihitaji 20000 ili ninunue sungura hao.
Asa kwa wakati huo choo kikawa kimeziba kwenye nyumba yetu ndogo ambayo asilimia kubwa kulikuwa na wapangaji.
Nikawa nimepewa deal la kumtafuta mzibua choo aisee ilinibidi nifanye maamuz ya kukizibua choo kile mimi ili niipate ile hela.
Nikampanga jamaa mmoja alikuwa classmate ajifanye yeye ndo mzibuaji choo.
Kazi nikaipiga usiku kucha.
Mwishoe nikamaliza nikiwa nanuka vibaya.
But nashukuru nilitimiza malengo yangu na kuanza kufuga sungura.
Nilikaa nao kipindi kirefu ila kuna wahuni waliniotea wakapita nao.
Aiseee nililia kwa uchungu sana maana niliwapata kwa tabu sana but all in all maisha yalisonga.
 
Dah, hii imeniuma sana. Nimehisi ni mimi.
 
Usiwaze man. Mwanaume ni kuvumilia maumivu
 
Back
Top Bottom