Ulisha wahi kumdai mtu pesa yako halafu anakujibu hivi?

Jakubumba

JF-Expert Member
Mar 5, 2011
1,624
500
juma ni mwalimu mwenzangu aliniomba sh 2000(elfu mbili) akanunue dagaa maana mshahara ulikuwa bado kidogo utoke atanirudishia, namjua alivyo mgumu kurudisha deni hasa pesa. Bahati nzuri tukaenda wote bank kuchukua mshahara kwa kutumia atm na mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo;

mimi: Juma nipe basi ile pesa yangu nahitaji kuitumia
juma: Pesa gani?(anajibu kwa ukali) then anasema ahaaa ile 2000? Nitakupa tukifika home maana sijahesabu bado.
Mimi:(nikawa mkali) aisee nipe pesa yangu vipi wewe? Mbona ulikopa umechuchumaa sasa hivi unnakuwa mkali?
Juma: Sikupi sasa!; kwanza nani shahidi ulinikopa?
Mimi: Hilo jibu lilinikatisha tamaa,nilimwangalia nikashindwa kummeza.


Wenye katabia kama haka waache sio kazuri,hata kama ni sh 1 ni yangu nipe ninafundisha kwa shida.
 
umejibiwa vizuri hivyo...niliambiwaga neno nikaapa kumkopesha mtu pesa kama nakupa nakupa tu nikijua sina changu.maana nilijitazama kwenye kioo upya
 
Sio fresh ila Juma aelewe shida si siku moja kwan tuelewe kwamba tenda wema nenda zako usingoje malipo!!
 
kaka nimecheka japo ukifirilia sana inauma pole sana ndo matatzo ya kukopesha hayo
 
kweli bana 2000 ni kubwa, lakini imekusaidia kujiwekea ngao asije kukukopa tena. Kuna jamaa ni matapeli na walalamishi. Anaanza na 10000 analipa, baada ya mda anaongeza dau mpaka 2000 analipa, akisha jenga uaminifu ndo anakupiga dau kubwa ambalo hautokaa ulipate.
 
kuna raia huwa wanadhani kuwa mkorofi ni kitu cha kujivunia ila hawajui nao kuna siku yatawakuta yale wanayowafanyia wenzao halafu yakiwakuta wao mama yangu wanalia kama mbwa. Nitarudi baadae kidogo
 
na wewe ulizidi kumdai kwa nguvu, si alikwambia atakupa akifika home?

Hata mimi ukinidai ki-baba koku baba koku nakutolea uvivu.
 
umejibiwa vizuri hivyo...niliambiwaga neno nikaapa kumkopesha mtu pesa kama nakupa nakupa tu nikijua sina changu.maana nilijitazama kwenye kioo upya

Ukipigwa shavu shavu la koshoto geuza na la kulia so ulipaswa kumwogeza 2000 nyingine
 
Back
Top Bottom