Ulaji wa mayai kwa kuku wanaokunywa dawa

qtie

Member
Feb 3, 2017
35
11
Habari
Naomba kujua athari za dawa ya kuku kwenye mayai. Nimewapa kuku dawa ya typhoid inaitwa Fatrium bado wapo kwenye dozi, mayai yanaweza kuliwa au nisubiri siku kadhaa. Naomba anayefahamu anijuze
 
Majibu sahihi ya suala hili ni sawa na kuangalia horror movie
 
Tatizo wengi tunafanya mambo kwa mazoea na uzembe, ina maana uliponunua dawa hukuuliza kwa muuzaji au kusoma kibandiko cha maelekezo?
 
Nilisahau kuuliza, nikaenda duka la dawa lililopo karibu ila aliyekuwepo hakuwa mtaalam kwa hiyo hakua anajua pia, hadi nauliza hapa sijaona kikaratasi cha ndani wala maelezo yaliyopo kwenye dawa hayajielezi kuhusu mayai. Nimejaribu kugugo sijaona pia. Sijakurupuka tu.
Kama huna ushauri kaa utulie tu sio lazima kucoment.
 
Dawa nyingi hueleza matumizi ya nyama au mayai au kama ni mbogamboga , matunda n.k yataliwa muda gani baada ya kumpa mfugo au kupulizia,nyuzia kwenye mmea.

Kama haija andikwa tafuta daktari wa mifugo watakusaidia ila uwe mwangalifu na iyo kampuni iliyo tengeneza iyo dawa.unaweza kukuta nikampuni feki au dawa feki.
 
Ni hatari sana kwa afya. Hizo dawa huwa zimeandikwa muda wa kutotumia nyama/mayai ya kuku baada ya siku za dawa kwisha. Soma vizuri maelekezo.
 
Nilisahau kuuliza, nikaenda duka la dawa lililopo karibu ila aliyekuwepo hakuwa mtaalam kwa hiyo hakua anajua pia, hadi nauliza hapa sijaona kikaratasi cha ndani wala maelezo yaliyopo kwenye dawa hayajielezi kuhusu mayai. Nimejaribu kugugo sijaona pia. Sijakurupuka tu.
Kama huna ushauri kaa utulie tu sio lazima kucoment.
Acha upuuzi kijana wakati mwingine kubali ushauri hata kama unauma, hakuna dawa yoyote ya mifugo ama mimea inayokosa kibandiko cha matumizi na tahadhari. Ikiwa hyo dawa haina maelezo yoyote ni feki, jiandae kuugua kansa siku za mbele kwa kuendekeza kununua dawa zisizodhibitishwa.
 
Ni hatari sana kwa afya. Hizo dawa huwa zimeandikwa muda wa kutotumia nyama/mayai ya kuku baada ya siku za dawa kwisha. Soma vizuri maelekezo.
Hii imeandikwa muda wa kutotumia nyama lakin hamna wa mayai
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom