Si jambo la siri au kificho kwamba kuna ufisadi mkubwa, tena wa kutisha uliofanywa na unaoendelea kufanywa na Mkuu wa chuo cha Ufundi Arusha. Mtu anaweza kushangaa au kuuliza kwanini Mkuu wa Chuo na siyo Menejimenti ya Chuo? Ukweli ni kwamba ni kama vile Chuo hakina Menejimenti kwa sababu Mkuu wa Chuo ndio kila kitu katika Chuo hiki. Mkuu wa chuo ndiye anayeamua masuala ya ununuzi, ukaguzi, uhasibu, sheria, rasilimali watu, na hata idara zifanye nini. Kwa namna anavyofanya kazi ametaka aonekane kama mtendaji wa kila kitu na kwa maana hiyo wasaidizi wake hawana cha kufanya ila kuwa watazamaji tu.
Ni katika hali hiyo Mkuu wa chuo ameona inafaa kutumia nafasi hiyo kujichukulia fedha za serikali na umma kama anavyotaka. Mkuu wa Chuo alianza kwa kujizidishia mshahara kwa kulipwa katika ngazi kubwa kuliko cheo chake. Akawa anakula fedha zinazotengwa kwa ajili ya mafunzo viwandani. Fedha hizi amekuwa akizila kwa kuongeza idadi ya wanafuzi wa kulipwa na kupunguza idadi ya siku kwa waalimu kwenda kukagua wanafuzi wakiwa viwandani. Aliponogewa zaidi aliamua kutoa malipo hewa kutoka katika miradi mbalimbali ya ujenzi na kuyapitishia katika akaunti ya chuo ijulikanayo kama ATC-PCB ambapo huwa amekuwa akiamua kula pesa kutoka katika akaunti hiyo kama anavyotaka. Kama haitoshi Mkuu wa chuo amekuwa akila fedha inayotengwa kwa ajili ya chakula cha wanafunzi kwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata huduma hiyo.
Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. Mkuu wa chuo alienda mbali zaidi na kuamua kula mshahara wa mwezi mmoja kwa wafanyakazi 25 wa Chuo bila maelezo. Mkuu wa chuo alikula sehemu kubwa ya fedha zilizotolewa na DIDF kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji katika shamba la Oljoro Arusha. Ubunifu wa Ulafi wa Mkuu wa Chuo uliongezeka na aligundua njia ya kujipatia mapato kutoka mishahara ya wafanyakazi wanaoishi katika nyumba za chuo. Mkuu wa chuo anaishi nyumba ya chuo na halipi chochote lakini aliamua bila ridhaa ya wafanyakazi kukata pesa kutoka mishahara ya wafanyakazi huku ikiwa haifahamiki fedha hizo ziko wapi au zinafanya nini.
Ulafi wa Mkuu wa chuo amepanuka mpaka kufikia kiwango cha kuwa akiongeza gharama za miradi ya ujenzi inayofanywa chuoni. Kwa mfano, Ujenzi wa jengo la madarasa linalojulikana kama Jengo la Umwagiliaji limeongezwa mpaka kukaribia mara dufu. Jengo hilo lilikadiriwa kujengwa kwa Tsh 2.67 bilioni zilizokuwa katika mkataba wa ujenzi lakini mpaka mwisho jengo hilo limetafuna kiasi cha Tsh 4.0 bilioni huku muonekano wake kwa ndani ukionekana kufanywa kwa kiwango cha chini kabisa. Pia katika ujenzi huo idadi kubwa sana ya matofali inaweza kuandikwa kuwa yaliibiwa. Idadi ya matofali yaliyochukuliwa kwa mwavuli wa ukubwa wa Mkuu wa Chuo ni 20,000, idadi ya matofali ambayo yangetosha kujenga madarasa 18 mengine.
Fedha nyingi ambayo ingeweza kufanya maendeleo mengine kwa aajili ya chuo na Taifa inaonekana kuliwa kwa njia ya kifisadi kwa sababu tu ya ulafi wa mtu mmoja asiyekuwa na chembe ya Uzalendo kwa nchi yake.
Madhara ya ulafi na kukosa uzalendo kunaonekana kwenda mpaka kuathiri kiwango cha elimu inayotolewa. Kwa mfano, Mkuu wa chuo ameshindwa kabisa huhuisha mitaala iliyopitwa na wakati inayotumika kufundishia wanafunzi. Kibaya zaidi ni kwamba kwa maelekezo ya Mkuu wa Chuo baadhi ya Idara za kitaaluma zimekuwa zikitumia mitaala isiyofahamika ambayo haijapitishwa na Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) wala Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
Katika kutaka kubana matumizi ili pia kupata pesa ya kuweza kuiba kwa njia ya ufisadi na ulafi, Mkuu wa Chuo anatumia wafanyakazi waendeshaji wasio na sifa kufundisha wanafunzi wa ngazi ya shahada. (Bachelor of Engineering). Ni mambo ya ajabu sana yanayofanyika kweli mtu mwenye akili zake timamu akiyaona anaweza kushangaa sana na kujiuliza kama Mkuu wa Chuo anayo elimu ya kiwango kinachozungumzwa maana yanayofanyika yanasikitisha. Msomi wa kiwango cha PhD ni mtafiti na huamini katika utafiti lakini hapa ni tofauti.
Hivi karibuni kulikuwa na habari za ugunduzi wa chopa (Helicopter) uliofanywa na chuo lakini hakukuwa na utafiti wowote uliokuwa umefanywa ili kutokana na utafiti huo chopa hiyo iweze kutengenezwa. Hakukuwa na andiko lolote la kitaalamu ambalo lingekuwa mwongozo wa utengenezaji wa chopa hiyo. Hata hivyo utengenezaji wa toy hiyo ya chopa ulipigwa marufuku na serikali na hivyo kuwa imetumia muda na rasilimali za serikali bila tija yoyote.
Katika mazingira yanayofanana na hayo pia kulikuwa na mbwembwe na viapizo vingi sana kuwa Chuo cha Ufundi Arusha Chaapa kumaliza tatizo la umeme nchini. Lakini sababu kubwa ya viapizo hivyo ilikuwa ni utafiti uliokuwa umefanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuhusu kutengeneza mashine (turbine) ya kuweza kufua umeme kwa njia ya maji ambayo haikuwa imefika mwisho. Hakukuwa na utafiti wowote uliofanywa na chuo wala hakukuwa na andiko lolote lililokuwa limeandikwa na chuo huhusu utengenezaji wa turbine za kufua umeme ambao Mkuu wa chuo alionekana kwa wakati huo kila chombo cha habari akijaribu kuchota akili za watanzania kwa mambo yasiyo ya kweli.
Ni wakati sasa Uchunguzi wa kina wa umahiri wa kitaaluma wa chuo hiki uweze kufanyika ili kuepusha hasara kubwa zaidi inayoweza kusababishwa kwa kuendelea kuamini kisichokuwepo. Elimu ni msingi wa maendeleo ya Taifa lolote, Ni hujuma mbaya sana ikiwa tutakubali elimu ya Taifa letu ikahujumiwa na walafi wa aina ya Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha.