Ukweli kuhusu tukio la tuhuma za rushwa monduli dhidi ya Masyaga Matinyi

kwanza unatumia jina ambalo halifanani na hoja yako, unajiita marksman wakati umeshindwa hata kulenga ukweli wa unalolisema. hakika ukubwa wa mwili si hoja.

Go back to Mwambungu, get his report. Kama kuna mapendekezo unayoyasema yaweke hewani. Pia namfahamu Masyaga sana sana, huyo mwanajeshi mstaafu ni nani.

Kazi njema mpiganaji a.k.a. Marksman.

Alichoandika marksman ni cha ukweli kabisa ya kile kilichotokea. Nilikuwa pale NH wakati ule - Muhingo alimrudisha kazi kinyume cha mapendekezo ya Mwambungu!

Mie nadhani ktk hali ilivyo haikuwa vyema kwa Mobhare kumtetea ndugu yake humu JF kwani kuna mengi yanaweza kuibuka hapa. msisahau pia watu wa Takukuru nao husoma JF hivyo wanaweza kuwa wanapata lines flani za kufuatilia kuhusu mtuhumiwa.
 
Watanzania wenzangu,

Nachukua nafasi hii, kwa masikitiko, kutoaTamko fupi kama kaka wa MASYAGA MATINYI - mdogo wangu anayenifuatia kwa baba namama yetu. Aidha, mimi pia ni mtumiaji wa jina la ubini la “MATINYI” na ndiyomaana baadhi yenu mlihisi kwamba ni mimi niliyekamatwa na TAKUKURU. MASYAGA anamwanasheria wake na itakapobidi atatoa Tamko la kisheria lakini ili kuondoaukungu nimeona ni heri nitoe UFAFANUZI wa tukio zima. Zaidi, ni uzalendo wanguna mapenzi yangu kwa haki, na wanaonifahamu wanalijua hili vema.

Naomba nirudie: KESI NZIMA YA RUSHWA DHIDIYA MASYAGA NA WENZAKE NI UONGO. Huu si utetezi tu bali pia ni UKWELI wakilichotokea. Hakuna kuficha: TAKUKURU ina tatizo.

Ipo sababu kwa nini imenichukua muda mrefukulisemea jambo hili. Natamka wazi kwamba nina uhakika na hiki nikisemacho;mwenye hadithi tofauti akawasaidie TAKUKURU mahakamani. Kwa kuzingatia kuwakesi haijaanza kusikilizwa, Tamko hili kamwe si kuingilia uhuru wa mahakama(contempt of court) bali ni kuingilia uovu – siyo utendaji - wa TAKUKURU. MASYAGA hakuizungumzia rushwa wala hongo; hakuiomba na wala hakuipokea.
Kwa wanaofuatilia vizuri habari za Tanzania, MASYAGA ni mmoja wa waandishi wa habari mahiri nchini linapokuja suala lakutetea na kulinda maslahi ya taifa letu na anaijua vema sekta yetu yamaliasili. Sisemi hivi kwa kuwa ni mdogo wangu, bali kwa kuwa maandishi yake yapo kama uthibitisho. Itakumbukwa kwamba wiki moja kabla ya tukio hili alitoahabari nyeti ambayo sitashangaa nikisikia baadaye kwamba ndiyo imemponza.

MUHTASARI WA AWALI
Alhamisi Juni 14, 2012, mtandao wa JamiiForum na televisheni ya TBC walisambaza habari duniani na nchini kuhusu tukiola kukamatwa kwa waliowaitwa waandishi wa habari watatu akiwemo MASYAGAMATINYI, Mhariri wa gazeti la Rai. TBC1 walimkariri kamanda wa TAKUKURU wa mkoawa Arusha akidai kwamba akina MASYAGA walimwomba rushwa mtumishi wa Tanescohuko Monduli ya sh. milioni 1.8 na kisha kupokea sh. 200,000 kamakianzio. TBC1 waliinukuu TAKUKURU wakidai eti waandishi hawa walikuwa wakimbanaMtanesko huyo kwa tuhuma kwamba hana sifa za kushika nafasi aliyonayo.

Ijumaa MASYAGA na wenzake walifikishwamahakamani mjini Arusha na kusomewa mashitaka ya kuomba rushwa ya sh.milioni 1.5 na siyo sh. milioni 1.8 tena na eti walizipokea sh. 200,000.TAKUKURU haikueleza kwa nini kiwango kimebadilika.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka ambayo nakalayake ninayo kibindoni, mtuhumiwa wa pili amebambikiziwa kosa la pili lakumchukulia MASYAGA huo mzigo wa rushwa. Watuhumiwa wote watatu, wengine wakiwani MWITA CHOMETE na BORA BIDIGA, wamepata dhamana na kesi yao itatajwa tenaJuni 29, 2012. Tunaishukuru mahakama ya Arusha na mwendesha mashitaka waserikali kwa kuiheshimu haki.

KILICHOTOKEA
1...Mtanesko ANDREA MEZAanalalamikiwa na jamii kujihusisha na ufisadi wa magogo ya miti ya stimu nandiyo tatizo lililowapeleka akina MASYAGA kwake pamoja suala la sifa zakezilizompa nafasi ya msimamizi wa mafundi wa TANESCO Monduli.

2...Mtuhumiwa wa tatu, BORA, simwandishi bali ndiye aliyemwambia MASYAGA kwamba kuna tatizo Tanesco Monduli.Hata kama MASYAGA angetaka hongo, ni wazi kwamba asingeweza kuomba na kupokeambele ya mtu aliyemstua kuhusu suala hili la mistimu. Hii ni common sense tu.

3...Tatizo lilianzia kwenye kitimutimu cha Mtanesko ANDREA na watu walioko Arusha ambao walikuwa wakimpigiasimu kumtisha kuhusu mambo yake ya mistimu. Hatimaye aliwatumia sh. 400,000zinazodaiwa kuwa ni za TAKUKURU kwa M-PESA na wakazipokea na kukubaliana kujakubeba zingine Alhamisi asubuhi. Wakati akina MASYAGA wanakwenda ofisini kwake Alhamisi asubuhi, ANDREA kwa ujuha wake, alifikiri ni watu wale wa Arusha, hivyo, akawaambia TAKUKURU mchezo umekamilika na wenyewe wakarundikana TanescoMonduli kwa ushari bila kujua wanafanya nini. Kiongozi wa kundi lao alitokaArusha kuja kufanya operesheni ya kikomandoo.

4...Kwa staili za ushushushu wasinema za James Bond, TAKUKURU walimpa ANDREA kirekodia sauti na kishawakajificha mahali kininja. Ili kuimarisha ushahidi wakamwambia ANDREAamweke Mtanesko mwingine ofisini mwake. Akina MASYAGA walipofika wakaanza mahojiano na ANDREA huku yule kijana (shahidi) akasisitiza kwamba wamalize mambo kishikaji (lengo likiwa kuwadakisha akina MASYAGA hongo na kupata rekodi ya sauti). MASYAGA akasema HAPANA. Kisheria, kumchomokea mtu afanye uhalifu kama walivyofanya Matakukuru hawa ni uhalifu.

5...ANDREA na huyu kijana wake wakatoka kuzungumza faragha. Waliporejea yule kijana akamwekea sh. 200,000 CHOMETE mfukoni na yeye bila kuchelewa akazitupa nje ya dirisha. Matakukuru zaidi ya sita wakaingia na kutoa kipigo kikali kwa CHOMETE pamoja na matusi yasiyoandikika hapa. Walimpa kipigo kitakatifu na ameishia kutibiwa kwa PF3. Hawakujali kwamba wangeweza kuua. Ni matumaini yetu kwamba atapona vema. Kisheria, kumpiga mtuhumiwa ili umshikishe hongo mkononi ni uhalifu.

6...Matakukuru wakaenda kwenyegari la akina MASYAGA kupekua kinguvu (bila kibali) ili kupata zile laki nne za M-PESA. Hawakupata kitu. Wakawapeleka Arusha huku wakiamini kuwa MASYAGA ameshapokea laki nne. Kwa akili nyepesi tu hili lilishakuwa suala la mistaken identity lakini Matakukuru wakachagua kuendelea kuwa brutal,unprofessional, unethical, n.k.

7... Baada tu ya tukio, kamanda wao mkubwa akawaita TBC1 na papo hapo habari zikafika JamiiForum kimazingaombwe na usiku saa 2:00 ikawa ndiyo habari ya kwanza. Hii ni kinyume cha maadili ya kazi za vyombo kama TAKUKURU, Polisi, Uhamiaji, n.k. Ni uhuni. Huwezi kutangaza kitu unachokichunguza na tena ambacho kimeshatoa dalili kwamba kina walakini. Ndiyo maana TBC hawakuelezwa kuhusu zile lakini nne. Kulikuwa na haraka gani wakati “watuhumiwa wao” walishapatikana? Kwa nini waiite TBC1 pekee– televisheni mbovu ya taifa letu?

8...Katika hali ya ajabu, TBC1 wameishikilia habari hii kuliko wanavyofanya kwenye habari zingine na kuzua maswali kwamba nini hasa lengo lao. TBC1 walilala na kuamka nayo kwa kadri walivyomudu. Aidha, Jamii Forum - wao ni nani katika mfumo wa utoaji habari za TAKUKURU?

9...TAKUKURU walipofika Arusha wakaisikiliza ile rekodi. Haikuwa na sentensi wala robo ya neno la MASYAGA kuomba rushwa. Kwenye statement wakakwepa kukitaja kile kirekodia sauti lakini MASYAGA akasema hawezi kusaini mpaka waandike ukweli. Kimsingi alikuwa tayari apigwe hadi kufa lakini siyo kusaini uongo. Alitumia ushujaa kuilinda haki yake. Mahojiano yaliisha saa tano usiku na watuhumiwa wakawekwa rumande kusubiri majaliwa ya siku ya pili. Kwa kuheshimu ukweli wa tukio, ni hakika hii ilikuwa unlawful confinement. Huwezi kuwaweka watu ndani baada ya kuwasukumia kosa la uongo, tena kwa kipigo, mateso na matusi. Hiyo ndiyo TAKUKURU yetu.

10...Ijumaa asubuhi TAKUKURU wakawapeleka mahakamani na suala la sh. laki nne wakaliacha. Kwanini? Aidha, zile sh. milioni 1.8 zikabadilishwa na kuwa sh. milioni 1.5 kwenye hati ya mashitaka. Kwanini? Hata hivyo, gazeti la MAJIRA limechagua kuandika sh.milioni 5; hili ni tatizo jingine kabisa. Si vyombo vingi vya habari vilivyoishadidia habari hii zaidi ya TBC1 kwenye siku ile ya kwanza kutokana na umakini wa wahariri wake.

11...Kule Jamii Forum kuna wahusika wengi walionunua kesi hii huku wakiwa hawajui chochote cha ndani.Upumbavu wetu wa siku zote Watanzania. Jamii Forum walijifanya kwamba hawaijui TAKUKURU na vioja vyake. Mtanzania mwingine aliyeko Japan naye aliamua kusambaza habari hizi kwa nguvu zake zote kila sehemu aliyoweza; yuko Japan lakini ana kiherehere cha mambo ya Monduli.

12...Bado kuna maswali kuhusiana na kiu hii ya usambazaji na utangazaji huu wa habari hizi kwa nguvu zote iwapo ina uhusiano na binadamu walioandikwa na MASYAGA hivi karibuni. Kama tujuavyo, mbuga zetu ni shamba la bibi lakini ni upumbavu kuamua kwamba Watanzania wote tukae kimya. TAKUKURU walikuwa na shida gani ya kuwasukumia raia wema mambo haya, tena kwa kipigo, uongo, utesaji, utangazaji wa kihuni, n.k.? Kunasiri gani?

HITIMISHO
Hizo laki nne ziko wapi? Kwa nini hazizungumziwi tena? TAKUKURU waeleze tangu lini wakawa na haki ya kumshikisha mtu pesa kwa kipigo. Matakukuru wakitoe kirekodia sauti walichompa Mtanesko waona kamwe wasiseme eti hakuweza kurekodi vema.

TAKUKURU waoneshe jinsi MASYAGA alivyopokea laki nne huko M-PESA kwani aliwapa simu zake kwa hiyo wasilikwepe hili na ndio jambo walilolidai baada ya kumkamata. TAKUKURU waeleze ni kivipi MASYAGA angeomba rushwa mbele ya mtu aliyekuwa anamlalamikia Mtanesko huyu. TAKUKURU waeleze mikono ya MASYAGA ilikuwa wapi mpaka ikabidi apokelewe hongo na CHOMETE wakati wote walikuwa hapo hapo?

TAKUKURU waeleze kwa nini walianza na madaiya sh. milioni 1.8 na kesho yake wakapunguza hadi sh. milioni 1.5? TAKUKURU watudokezee tujue uhusiano wao na mwandishi wa TBC1 na mhariri wa TBC1 kwamba hata habari ikiwa na mashaka bado itarushwa tu mfululizo kwa siku kibao - wana ubia gani kwenye hili tu? TAKUKURU waeleze kwamba wana maslahi gani ya kumlinda mtu anayelalamikiwa na wananchi kwamba anafanya uhalifu?

Mpenda haki yeyote aelewe kinachoendelea na mzushi yeyote aseme lake lakini MAHAKAMA itamaliza mchezo wote.

Asalam Aleikum!
MOBHARE MATINYI, WashingtonDC, Juni 17, 2012.
Tata Mobhare, hivi bila JF ungeandika yote haya wapi? Umeteleza kidogo, JF si wa kulaumiwa it's place where we dare to talk loud and openly. Hata wewe umeweza, na kwa nini hukwenda TBC1 au kwingine? bila shaka usingesikika. Poleni familia ya Matinyi
 
Hayo ya Masyaga ni ukweli tu, ingawa anaweza kujinasua kutokana na kwamba bahasha ya hela hakuchukuwa yeye, hivyo ataruka kimanga.

Kuhusu yale ya New Habari, ni ukweli mtupu!!!! asikatae.
 
Hivi Mhariri mzima atoke Dar kufuatilia mtumishi wa Tanesco ngazi ya wilaya hii inaingia akilini kweli?
Kwangu hiyo ni clue namba moja ya kuonyesha kuwa safari ilikuwa na sababu ya ziada.... Hata hizo fedha kwanini walizirusha dirishani kwenda nje. Kama mtu yuko na wewe ndani halafu anakulazimishia fedha utazirusha nje kupitia dirishani au utaacha zidondoke chini? Wasitudanganye bwana. TAKUKURU wajaribu kufuatilia pale fedha za m-pesa zilipochukuliwa na kumhiji mlipaji ni watu wa aina gani waliolipwa...
 
Back
Top Bottom