Ukweli kuhusu Ndege ya Air Tanzania "kuegeshwa" bila kuruka

Lakini hiyo ndege si haina hata mda mrefu iweje iwe imeshafikisha ayo masaa ambayo itatakiwa kufanyiwa matengenezo...... Kwani hayo matengenezo yanatakiwa yafanywe baada ya mda gani
 
Kuna uzembe ulifanyika sielewi kwa nini mtoa mada anaficha. Vifaa vikivyomaliza masaa yake vineagizwa ndege ikiwa grounded
Huo ni uzembe wa kiwango cha lami.
Nashangaa mpaka sasa haijatangazwa waliotumbuliwa !
Uzembe ilikuwa sio kugundua muda wa kuisha tu Bali hata kuagiza vifaa husika
Huwezi kuagiza vifaa wakati tayari vinavyotakiwa kubadiriwa Masaa yamekwisha
Vifaa vingi vya ndege ni "plug n play" hivyo uzembe ndio uneifanya ndege moja iwe kwenye loss mode
pesa zilikuwa hazina mkuu
 
Zina magurudumu ya bajaji!!! UNABISHA?
GURUDUMU ZA BAJAJI INAWEZEKANA KAMA HIYO KAPUNI YA BAJAJI INATENGENEZA GURUDUMU ZA NDEGE. ILA KAMA NI HIZI ZA BAJAJI TUZIONAZO MITAANI HUKU SIAMINI KAMA ZINAMUDU MSUKOSUKO WA NDEGE INAPOTUA IKIWA NA SPIDI ISIYOPUNGUA KM 250 KWA SAA NA ULE UZITO INAPOTUA KWENYE LAMI KWA KISHINDO
 
Wakuu salamu,sababu ya tofauti ya majira ya huku nilipo na huko nyumbani,basi kuna mambo yamekuwa yakinipita humu jukwaani,ama ninakuwa usingizini au nakuwa busy na kazi iliyonileta.

Nimekuta msgs nyingi na "mentions" nyingi sana za barafu watu wakibishana kuhusu ndege ya ATCL kuharibika.

Kifupi na kwa taarifa rasmi za kiufundi japo nipo mbali na nyumbani ni kuwa,ndege hiyo ya ATCL haijaharibika na sio kweli kuwa eti mainjinia 50 wameshindwa kuitengeneza.Daah!!Jamani huu uongo na masimango kwa shirika letu la ndege inatoka wapi?

Ni kweli hata mimi kuna mambo sikubaliani na JPM,hasa katika masuala ya bunge kuonekana mubashara na uminywaji wa upinzani,lakini simtakii mabaya wala kuizushia serikali yake uwongo.Yoyote unaemuuliza,wewe umepata wapi taarifa hizo?Atakwambia "Mange kasema"....Huyu anayetajwa ni Mhandisi?

Kwa wale waliofuatilia ujio wa ndege hizi wakati zinaletwa Tanzania,watakumbuka kuwa ndege moja ilitangulia kabla ya nyingine,iliyotangulia ni ile iliyokuja na namba za usajili za Canada za C-FHNF ambapo ilipofika Tanzania ikapewa namba ya 5H-TCB.

Hii 5H-TCB ndio ilianza kufanya kazi mbele ya ile ya pili yenye usajili wa 5H-TCD.Kwa hiyo hata kwa masaa ya kukaa hewani,hii iliyotangulia ya 5H-TCB ndiyo yenye masaa mengi hewani kuliko 5H-TCD iliyokuja baadae na kuanza kufanya kazi.

Ndege iliyoegeshwa kwa muda kwa ajili ya matengenezo madogo ni 5H-TCB,na hii si Tanzania tu,bali dunia nzima.Ndege inapofikisha masaa kadhaa kuwa hewani,let say masaa 12000 hewani,inatakiwa kuwa grounded ili kuweza kubadilishiwa vifaa kadhaa ambavyo masaa yake yanakuwa yamekwisha kwa vyenyewe kutimika.

Hii ni hata kwenye magari,tunashauriwa kutumia matairi ya magari kwa masaa kadhaa,yakipita hayo masaa basi tunapaswa kubadilisha,lakini kiswahili-swahili watu huendesha tu magari mpaka yanawapasukia na kupata ajali.Usafiri wa anga ni tofauti,mambo ya "safety" ni jambo la kwanza na la muhimu.

Kilichotokea kwa ndege moja ya ATCL ni kuwa grounded kwa sababu za kiufundi na kiusalama (safety),ili kufanyiwa "cheki" ya baadhi ya vifaa na kuweza kubadilishwa ili irudi hewani kwa uhakika zaidi.Hii ni kote duniani.

Sisi tunaweza kuona kwa wepesi sababu shirika letu la ATCL lina ndege mbili tu,moja ikienda "hunger" (maintanance area) inakuwa rahisi kujulikana sababu moja tu ndio inabaki ku-operate,lakini jambo hili ni kawaida,leo ukienda Kenya utakuta ndege zilizoegeshwa sbb ya masaa kupita,ukienda KLM,Swiss International,South Africa Airways,Qatar nk.Si jambo la ajabu,kwanini libebwe kama mada?

ATCL ni moja ya kampuni yenye wahandisi wazuri walio wazawa.Na kwa aina ya mkataba wa kampuni ya bombardier,mpaka sasa ATCL imekuwa "attached" na mtaalamu mmoja (Consultant) toka Canada,atakayekuwa kwa muda fulani kama mshauri wa kiufundi moja kwa moja toka kiwandani.

Habari hizo tuzipuuze,si njema kwa mafanikio ya heri ya shirika letu.Tuwatie moyo ATCL,inawasaidia sana watu katika usafiri wa ndani ya nchi.Kwa sasa safari zake za Dodoma,K'njaro,Tabora,Kigoma,Mtwara na Songea zimeokoa muda na kusaidia watu wengi.Safari ya Hahaya-Commoro imekuwa na mafanikio makubwa na yenye faida....Sio kila kitu yule "Binti" akisema kinakuwa na ukweli....

ATCL-The Wings of The Kilimanjaro.......

BARAFU : Kwa nyongeza ni kwamba watu wanapenda kuishi kwa umbea na wanakuwa hawana maanuzi,thinking zao ni kama TV ukiamua kupeleka any channel inakwenda na ukiamua kuizima inazima,
Ni vyema watu wasio jua mambo ya engineering wakaacha udaku kwa vitu ambavyo havina any logic,
Kwanza wanatakiwa wajue kuwakuna
Autonomous maintenance ,Preventive maintenance na kila equipment ina Working standard Instruction,Ndege sio bajaji au yutong

Sasa unakuta mtu hajua hata principle ya ndege kupaa analeta maneno ya Kipumbavu ,then unajiita mtanzania,
Engineering sio Facebook,sio instagram etc,Engineering ni Fact na reality,

429083-ced0b2eabe7bfc8e091e96aadbae25d3.jpg

Hii ni moja ya nege ya FN ambayo ipo ground na ipo kwa ajili ya matengenezo ,mbona hampigi kelele kwenye hizi ambazo hata quality yake sasa imeshuka???

Roho zinawauma sana kuona ndege ya watu fulani haitembei sasa mnaleta majungu,

Basi Huyo mange na wengine waseme hii ndege ni ya nani kama hawata kimbia

429085-853570adab4904337d20e0049abe74a2.jpg
 

Attachments

  • bbb.jpg
    bbb.jpg
    29.2 KB · Views: 30
  • IMG_20150818_161728.jpg
    IMG_20150818_161728.jpg
    236.3 KB · Views: 34
Umeongea upumbavu kabisa.....Mimi ni mmoja wa waathirika wa kadhia hii ya ATC......jana tumeingia saa sita usiku toka KIA baada ya kufaulishwa kwenye Precision Air.....ninachojiuliza kama wanajua yote haya ulivyoeleza ni routine maintenance sasa kwa nini majuzi tu walinipa tiketi inayoonyesha kwamba nitarudi na ndege yao jana jpili saa moja usiku??? ...na wenzetu wengine wakafanikiwa kusafiri kwa bahati kwa Precision siku ya jmosi badala ya jpili kama tiketi zinavyoonyesha.......yaani kabla ya kusafiri tulikuwa tumepewa taarifa tofauti tofauti za kusafiri kama mara tatu hivi...usiongee kisiasa...
Sasa mimi upumbavu wangu ni upi?Kwanini matusi wakati hapa tunaeleweshana tu?
Pole kwa kupata usumbufu,hizo ndio kadhia za usafiri wa ndege,better late than never
 
Barafu mtaaramu wa mambo ya Aerospace na Anayetumika na CHADEMA!
Natumika na Chadema kufanyaje?
Mkuu mimi nipo huru,napongeza na kukosoa kwa kiasi...Mwenzako level za ushabiki nilishazipita
 
MmMmmh hivi tulisubiri zote zifike au iliyotangulia iliendelea kufanya kazi?
Mbona kama nakumbuka baada ya uzinduzi ndio zote zilianza kufanya kazi?
Unakumbuka sawasawa. Lakini ulichosahau ni kuwa kuna iliyotangulia kufika, kutengenezwa, kujaribiwa na masaa unayoelezwa hapo yanahusika na huko pia(siyo tu yale yaliyoanzia baada ya uzinduzi). Maana yake Kama ile ya kwanza imetoka kiwandani mwezi mmoja kabla ya ya pili, ikaanza majaribio mwezi kabla ya ile ya pili ni kuwa itafikisha masaa ya service mwezi 1 kabla ya ile ya pili, tukifikiria kwamba hizo tests na shughuli zote zimefanyika sawasawa kwa ndege zote(Kitu ambacho inaweza isiwe hivyo).
 
Shida ni hao ATCL wenyewe wanakua kimya sana mpaka watu wanaongea ongea ovyo na kumtumia huyo 'binti' picha za ushahidi... Kwani wangetoa maelezo kama haya tusingeelewa. Hata uswahilni kama una gari moja nalo likapata matatizo ukalilaza garage kwa muda ukaanza kubanana na sisi kwenye daladala tutaongea tu kua umeishiwa/ umeliuza/ umekosa hela ya mafuta/ mbio za sakafuni n.k.
Maelezo mazuri haya lakini yangetoka ATCL au hata wizarani.
 
Mkuu hayo matengenezo kwa wastani huwa yanachukua muda gani?
Katika service ya ndege, kuna kuondoa bearings kadhaa kutoka kwenye engine; process hiyo hutegemea na ubora wa vifaa walivyo navyo mafundi lakini inaweza kuchukua wiki tatu hadi mwezi mzima au zaidi. Kwa kawaida katika workshop kubwa huwa hawabadili bearings hizo mara moja bali huondoa injini yote na kuweka injini nyingine kusudi ndege irudi hewani huku injini iliyotolewa ikiwa inatayarishwa kwa matumizi ya baadaye.
 
mange ni muongo...sasa hvi wote wanaangali Ikulu weshaachana na bajeti yao..

UFIPA uzalendo uko kisogoni..
 
Mkuu Barafu uko sahihi kabisa, Unajua limezuka kundi la Watu kwa Media kila Japo wao ni kukosoa tu na Kuombea Tushindwe yani hakuna tena uzalendo, Hata kama kuna kupingana na Mkuu machache lakini sio mpaka issue Technical mtu analeta siasa, Ivi waandisi 50 kweli? Na mtu still ana amini na kuanza kutokwa Povu
Nakubaliana na wewe kuwa si kila yanayoletwa mtandaoni ni ya kweli. lakini pia watu ambao naturally si wazalendo, japo wengi wanaozaliwa kuwa na hali hiyo hivi karibuni wanasababishiwa na tabaka tawala maana kila linapofanya jambo hukimbilia kujigamba na kuzodoa wale wasio wa tabaka tawala. Hali hiyo hupelekea kuwepo ushindani wa pande hizi mbili katika kila jambo hali ambayo huathiri interests za taifa.

Ila naomba kupingana na wewe unapotumia kigezo cha kuwa na wahandisi 50 kama ndio sababu ya kutotokea matatizo yanayodaiwa kutokea. Kwani kote tunakoharibu ni kwa sababu hatuna watu competent/trained kwa kazi hizo? hao wanaosadikiwa kuharibu kwenye suala la mchanga, ni kweli hawakuwa wanatosha? Hata CV ya Prof. Muhongo haitoshi kwenye suala la madini? Kifupi ni kwamba wanaweza kuwepo hata wahandisi 200 lakini for some reason(s) mambo yakaharibika tu...

Mi "ni mweupe" kabisa kwenye hayo masuala ya aviation, kwa hiyo sina opinion katika hilo linalojadiliwa.
 
Back
Top Bottom