Ukuta katika machimbo ya Mererani wazua utata

Migodi wa North Mara, Tulawaka, Buzwagi yote imezungushiwa ukuta na mgodi wa Bulyanhulu uko hatua za mwisho kuanza ujenzi wa ukuta, nchi hii bila ukuta hakuna utakachopata, anzia makazi ya watu nenda masaki mikocheni kinondoni nyumba zote zimezungushiwa ukuta

vingunguti viwanda magodown na magereji yote yamezungushiwa ukuta. Huku Ilemela ofisi za halmashauri zimezungushiwa ukuta,

ukuta mererani lazima uwepo na utalindwa na jw ukiukwea unapigwa risasi ya kichwa.
 
Chuma, uchimbaji madini ni taaluma ni wale tu waliosomea mambo ya madini ndio watakaoruhusiwa kuingia ndani, tunataka uchimbaji wenye tija na wa kitaalamu, haya mambo ya kutoa makafara hayatakuwa na nafasi tena.
 
Hujiulizi kwanini bandarini kuna Ukuta lakini ni sehemu inayoongoza kwa wizi?
Kwa hiyo kutokuwa na ukuta katika ofisi za makao makuu ya CHADEMA kumepunguza wizi wa pesa za Chama na matumizi hovyo ya ruzuku!!!?????
Acheni upuu.zi enyi misukule. Mnapinga mambo ya msingi kwa hoja dhaifu. Jikiteni kwenye Sera sio kuvaa madera!
 
Tatizo letu kubwa Watanzania, haswa MISUKULE ya vyama vya siasa ni kuchangia hoja au kutoa matamko kwa ujuaji mwingi na mihemko, kejeli na matusi bila ya kufanya UTAFITI na kujiridhisha pasipo Shaka.
Hakuna kitu kibaya katika Jamii au Taifa kwa ujumla kama kupotosha umma na kupindisha mambo ya kitaalam kwa porojo, propaganda na chuki bila ya kutumia TAFITI.

Serikali ilipoamua kujenga Ukuta katika migodi ya Tanzanite nina hakika kuna tafiti zilifanyika muda mrefu na haikukurupuka katika hili. Kuna nchi nyingi zimefanikiwa katika hili zoezi la kuzungusha uzio kwenye sehemu nyeti kama; maeneo yenye rasilimali za nchi, maeneo ya jeshi, Ikulu za nchi, Bank reserves n.k. Tatizo kubwa la misukule ni kufikiri ya kwamba ukuta huo unajengwa kama kuta za kwenye nyumba za kawaida.

Wengi mmekuja na hoja dhaifu inayotia KINYAA kuhusu wana Apollo kuchimba mahandaki kuingia katika mgodi husika.....shame on you!
Mh. Rais aliposema zitafungwa camera ambazo zitagumdua na kuona Tanzanite hata ikiwa iko ndani ya tumbo. Wengi wenu mkifikiria hizi camera ni sawa na CCTV.
Kuna vifaa maalum vya kuweza kugundua hayo mahandaki (tunels) na viumbe vilivyomo humo.

Kuna kitu kinaitwa " Ground Penetrating RADAR System (GPRS).
Kuna teknolojia ya Gravimetric Satellites ie: GRACE.
Bila kusahau teknolojia ya airborne kwa kutumia Multispectral Infrared and Visible Imaging Spectrometer (MIVIS).
Hizi ni baadhi ya teknolojia chache na effective katika kupambana na hao wana Apollo na Wezi wa Rasilimali za Taifa letu kwa ujumla.

Watanzania tujifunze umuhimu wa kufanya UTAFITI katika masuala muhimu na sio kuropoka na kuhemka kwa sababu ya MISUKULE na propaganda za WanaSiasa.
No Research, No right to Speech.
Tanzania mpya inakuja.
Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kwa hiyo kutokuwa na ukuta katika ofisi za makao makuu ya CHADEMA kumepunguza wizi wa pesa za Chama na matumizi hovyo ya ruzuku!!!?????
Acheni upuu.zi enyi misukule. Mnapinga mambo ya msingi kwa hoja dhaifu. Jikiteni kwenye Sera sio kuvaa madera!
soma ulichokiandika kama utakielewa mwenyewe, halafu mimi sijataja chama nashangaa kuona povu
 
Haya mambo hayajaamuliwa na wanywa viroba kama nyinyi,

Mshauri Mkuu wa Rais kwenye madini ni Jopo la maprofesa na madaktari wanaoongozwa na Processor Mruma na Orosso watu wabobezi kwenye hii sector.

Cha ajabu mishipa na mipovu inakutoka ambaye hata primary ulimaliza kutokana na uzee darasani.

Watu mkae mtulize saivi nchi haiendeshwi na wanasiasa kama mlivyozoea nchi inaendeshwa na wataalam.
 
Sio kila mtu anatumia akili ktk kufanya kazi zake, hekima au busara, maana wengine hawana hvyo, nature iko fair sana kwani pia wako wanaotumia nguvu kufanya kazi zao. Mgongano unakuja pale wanaodhani akili ni bora zaidi kuliko nguvu ktk uongozi wa uma, na hili liache liendelee maana haliwezi kubadili mambo yalivyo sasa. Watanzania tunalo ombwe la kutokuandaa viongozi, tukubali tukatae, na hili litazidi kututafuna Leo na kesho.
 
Habari wana jamvi,

Kama kichwa kisemavyo,

Huu ukuta wa Mererani ulioagizwa na Mh Magufuli umezua utata kwa namna ulivyopokelewa hasa na washikadau wa shughuli husika za madini.

Kwanza wameshangaa kutolewa maamuzi ya namna ile ambayo kwayo wamesikitika kwamba kwanini nguvu hio na gharama hizo wasingejenga barabara sehemu zenye uhitaji.

Wakaenda mbali zaaidi juu ya washauri wa mh. Magufuli kana kwamba elimu yao ni yakinadharia tuu imewanyima ujuzi wa uhalisia kufikia maamuzi yasiyo na tija au wanaamua kumpotisha tuu mh. Magufuli.

Wanasema kama mh. Magufuli hawajui wachimba madini na wadau wake atakuja shtuka shimo linachimbwa mererani wanapolo wanatokea Arusha au hata chumbani kwa mtu na hapo ndo hasara ya kamera itakapo onekana, pia patakua na njia nyingi tuu za kufanikisha wizi kwa serikali kama serikali haitokuja na sera rafiki, shirikishi katika ukusanyaji kodi.

Mimi ni mzalando!!
Una elimu yoyote ya maana kutoka kwenye combination ya masomo geology? Sio kila kitu roporopo mambo mengine waachie wasomi jadili mambo ambayo akili yako finyu inayamudu.
 
Hatujajipanga, tatizo mara nyingi ni umasikini wa kufikiri, kusuluhisha jambo kwa njia zisizo sahihi na elimu za kuungaunga.
 
Sio kila mtu anatumia akili ktk kufanya kazi zake, hekima au busara, maana wengine hawana hvyo, nature iko fair sana kwani pia wako wanaotumia nguvu kufanya kazi zao. Mgongano unakuja pale wanaodhani akili ni bora zaidi kuliko nguvu ktk uongozi wa uma, na hili liache liendelee maana haliwezi kubadili mambo yalivyo sasa. Watanzania tunalo ombwe la kutokuandaa viongozi, tukubali tukatae, na hili litazidi kututafuna Leo na kesho.
Mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa kwenye hii issue ya ukuta Mererani ni

Mambo ya hekima na busara hayo ni masuala ya jukwaani, Tofautisha utendaji na siasa.
 
Back
Top Bottom