Huo uchapakazi wake umeinufaisha vipi Tanzania?
Hili suala la uchapakazi wa Lowassa sasa ni just a constructed reality!!!!
thanks bro/sisy,
hawa watu wananikera sana mimi....huyu wanayetuaminisha ni mtendaji ametenda nini cha kujivunia kwa kuwepo kwake serikalini for that long.
CCM ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo,mbona halisemei hilo anajifanya kuisema serikali kwa kuwa yeye alimwagwa na mafisadi wenzie!!!??leo kwa nafasi yake ya uMwenyekiti wa kamati ya Bunge ya usalama na mambo ya Nje anafanya nini kuzuia uozo unaoendela kwenye eneo hilo???mbona tunazidi kusikia ufisadi tu kwenye hizo wizara? mbona hakemei au kwa kuwa yeye anataka Urais basi haya mengine hayaoni?? juzi wanakomaa wapitishe mswaada wa kununua vitu chakavu au scrapper....yeye amenyamaza sio bure usikute wameandaa mzigo wa kutuuzia na invoice zimeshaandaliwa wanasubiri upitishwe wazikombe tena kama kawaida yao..!!! inasikitisha sana.
mimi nimebahatika kutumia gari mpya ya ofisi na gari chakavu ya binafsi...kuna utofauti mkubwa sana in the two. gari mpya ukiwa mtumiaji mwenye discipline unaweza kuliendesha kwa miaka mitano bila kununua spare, wewe ni service tu...ila used utakoma ubishi, mpaka bodi inakatika unashangaa,taa zinadondoka, shoch up zinavuja,break zinaJam, injini inavuja mpaka unaweza kupata hasira na kuisusa tu nyumbani.....halafu serkali inapitisha sheria ya kununua scrapper na huyo mnayemwita mtendaji kanyamaza ili apige dili...thubutu!!!Used, duh eti tununue Meli used,ndege used,treni used ili kubana matumizi! kweli? mbona hamuongelei maV8 mnayoyatumia? mtu anakaa masaki anatumia V8 ya zaidi ya millioni 250 kwa nini msitumie RAV4 ili tuone mko serious???wizara ingehitaji V8 tatu kwa ajili ya safari ktk kila wizara na sio kama ilivyo sasa kila mkurugenzi na lake na wajuu yake vivyo hivyo.....Halafu mtendaji wenu yupo tu anasubiri kuwa Rais ndo aseme!!!
Kilimo kwanza wananunua mapower tiller yanapata kutu pale Mwenge tena baada ya kuyanunua kwa ufisadi, wakulima wamelima kwa nguvu zao wanaambiwa msiuuze nje chakula watu wa Dar watakosa cha kununua???!! why lakini? mtu wa Dar anakula burger wakati wa kijijini hata chumvi hana haafu unamzuia kuuza chake eti kwa kuwahurumia wengine???Mfano hai ni kwamba mdogo wangu amenikopa TZS 300000 akalima viazi na akapata magunia 40....ila kuja kwenye kuuza ameuza gunia moja TZS 8000 na kuambulia 320,000 tu baada ya mwaka mzima wa kuhangaikia shamba lake...hakuna soko la uhakika,hakuna barabara za kusafirishia mazao...sasa amekata tamaa anataka kuwa mchuuzi hataki tena kulima.
Mchapa kazi do you see these things oOOH! wanaokusifia umewapa nini wewe mtu? agrrr agriiiiiiiiiiiiii mwe mwe mweeeeeeeeeee!
nimechanganyachanganya mambo kwa sbb ya hasira, najaribu kuthink otherwise kwa nini hawa watu wanamsifia huyu mtu