Ukombozi kwenye media zetu ni MUHIMU kwa TAIFA

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Nimeipenda hii nimeikuta Facebook, kwa kweli tunahitaji ukombozi kwenye media zetu, ili zitusaidie kukomboa nchi yetu inayokabiliwa na matatizo makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

"Natumia siku hii ya Mei 3, kuomboleza: Media ni kama kikosi cha uokoaji. Inapotokea gari la zimamoto likawaka moto, inapotokea buldoza linalopaswa kuopoa magari yaliyozama linazama, ujue hali ni MBAYA na ya HATARI zaidi. Nakumbuka siku ya mafuriko Dar es Salaam, kulikua na picha mbili zinazonipa tafakuri nzito! Moja ni ile ya gari la zimamoto na uokoaji kutumbukia katika maji na ile ya katapila lililofika Mbezi Beach kuopoa magari lilipozama. Nikatafakari na sasa naona kama sisi waandishi wa habari wa Tanzania tumezama katika Taifa la watu waliokata tamaa wanaohitaji kuokolewa, nani atawaokoa? Naomboleza nikitoa wito kwa waandishi wa habari kuanzisha mapambano ya kujikomboa kwanza wenyewe ili tuweze kuikomboa nchi".

Source:

http://m.facebook.com/story.php?story_fbid=405093316179310&id=100000359340894&ref=pb&_rdr#405099729512002
 
Back
Top Bottom