Ukiwa Dar ogopa maeneo haya

headline_bullet.jpg
Uhalifu, mauaji nje nje!

Imeandikwa na Anastazia Alfred, Magdalena Balisidya, Amina Mrope (DSJ), Beatrice Shayo, Restuta James, Joseph Mwendapole, Richard Makore, Moshi Lusonzo, Romana Mallya na Eliwinjuka Shani.

CHANZO: NIPASHE

Jamani hayo Matatizo ya uhalifu na uuwaji yatakwisha lini hapo DAR?
Habari hii tu Waandishi kumi...! Dah!
 
Sasa kama ni hivyo, mbona Dar yote ni hatari maana haya ndiyo maeneo ya watu wa Kawaida, Ubungo Darajani imenikumbusha wakati fulani nilizingirwa katikati ya Daraja usiku, ilibidi nijifanye rafiki yao kwa kutoa kiasi cha pesa halafu nikawaomba wanipe nauli kwa ajili ya kesho yake, baada ya hapo walinisindikiza hadi karibu na Home. Sometimes ukikutana na hawa watu jaribu kuwa mpole maana vinginevyo hiyo roba ya misumari itakuhusu
 
Tatizo la vibaka haliwezi kumalizwa na polisi bali wanasiasa na watunga sera. Ongezeko la watu linapokuwa kubwa wakati maisha yanzidi kushuka kutokana kukosa sera bora za kukuza ajira na kuboresha maisha ya vijijini ambako ndiyo kuna nguvu kazi kubwa inayokilimbilia mijini baada ya kukosa huduma bora za jamii ni sawa na bomu linalosubiri muda ufike lilipuke.

Kamwe polisi hawawezi kuwepo kila mahala, njia pekee ni kwa serikali kuliona hili katika jicho la "National security issue" na njia pekee ni kuwachukulia hatua kali wale wote wanarudisha nyuma maendeleo kwa kupora mali ya umma na kutotekeleza majukumu yao waliyochaguliwa kwayo. Badala ya kuelekeza nguvu katika kushinda uchaguzi ni vizuri nguvu hizo zielekezwe katika kuboresha mazingira ya ajira na kujiajiri miongoni mwa vijana.

Hakuna mtu anazaliwa jambazi au kibaka ila hali ya maisha inafanya watu wakate tamaa ya kuishi na kuamua kuchukua risk ya kuwa majambazi kwani hata wakiuwawa wao wanasema ajali kazini. Serikali iboereshe maisha vijijini hali ambayo itapunguza urban migration. Hivi vyote haviwezi kufanywa na watu wanaoingia madarakani wakiwa na mawazo ya kujitajirisha badala ya kutumikia Taifa. Kama sheria kali zitawekwa kama za kunyongwa ukipatikana na hatia ya kula rushwa especially grand corruption ambayo ina effect kubwa kwa uchumi na maendeleo ya nchi watu watajifunza.
 
Haya maeneo yaliyotajwa ni kweli yote ni maeneo mabaya sana kiusalama
 
...The saddest thing in all this is that bado wakazi wa maeneo hayo WANAWAOMBA Polisi kuwaepushia dhahama hii badala ya KUWATAKA !!:mad: Aliyeturoga allishakufa bila kuacha mrithi!
 
mkuu! bongo sio salama kabisa!!!
Ninawafahamu in person, watu wanne ambao wamefunga nyumba zao huko Mbezi, makongo na Kigamboni na kuhamia Sinza kwenye nyumba za kupanga!!.......
Ni noma mazee!!

Mkuu,
Kigamboni maeneo gani? Maana nina kiwanja changu maeneo ya Tuangoma na najikusanya ili nijenge kibanda changu huko
 
Mkuu Dar ni kubwa na wameleta taarifa za sehemu nyingi kwahiyo walisambaa kwenda kwenye hizo kona kutafuta hizo taarifa
Mkuu ina maana wamekwenda kufanya utafiti kisha habari inakuja just 5 lines...! Sikubaliani na ilo, watafute kazi za kufanya bana si uhandishi wa mistari ya kuhesabika.
 
Mkuu ina maana wamekwenda kufanya utafiti kisha habari inakuja just 5 lines...! Sikubaliani na ilo, watafute kazi za kufanya bana si uhandishi wa mistari ya kuhesabika.
Mkuu mbona unaleta Ubishi wa simba na yanga? Muandishi wa habari gani ambaye anaweza kuleta hiyo habari peke yake? Mkuu X-PASTER unatoka wapi wewe Tanzania? Unajuwa Dares-Salaam ni mji mkubwa na ni Jiji kubwa katika hapo Tanzania? Mji wa Dares-salaam unakaribia watu Millioni 5 unayo hiyo Habari mkuu X-PASTER?
 
sasa hivi kuna maeneo ya kipunguni b machimbo na kitunda baada ya watu kuvunjiwa kipawa uku mtaani kumevamiwa kweli kweli vibaka wa madirishani wakuvunja nyumba ,wa silaha alafu awaji usiku ni kuanzia saa mbili usiku wanapiga hewani wanachukua kama zao yani
 
Mkuu mbona unaleta Ubishi wa simba na yanga? Muandishi wa habari gani ambaye anaweza kuleta hiyo habari peke yake? Mkuu X-PASTER unatoka wapi wewe Tanzania? Unajuwa Dares-Salaam ni mji mkubwa na ni Jiji kubwa katika hapo Tanzania? Mji wa Dares-salaam unakaribia watu Millioni 5 unayo hiyo Habari mkuu X-PASTER?
Si ubishi wa simba wala yanga, ila habari ipo too shallow, nilitegemea habari ingekaa ki-research zaidi... Any way wacha tuwape ongera ngaa kidogo.
 
Sasa unataka wakale wapiii??? Maisha ni timing tu,

We mmoja wao nini? huwezi kutoa kauli kama hiyo kwa wahanga ka sisi. Mimi tarehe 28/5/10 mdogo wangu alipigwa risasi nyumbani kwake Mbezi. Tukamzika tarehe 1/6/10. Wewe leo unasema wakale wapi? Hata haya huoni. Mods I think this guy need he dont deserve to be here. Tunakutaka uombe radhi kwa kauli yako
 
Mkuu ina maana wamekwenda kufanya utafiti kisha habari inakuja just 5 lines...! Sikubaliani na ilo, watafute kazi za kufanya bana si uhandishi wa mistari ya kuhesabika.

Mkuu X-PASTER hiyo mistari mitano umeihesabu wapi? mbona naona zaidi ya mistari mitano? labda nahesabu kingumbaru. Mzima lakini Mkuu?
 
Mkuu X-PASTER hiyo mistari mitano umeihesabu wapi? mbona naona zaidi ya mistari mitano? labda nahesabu kingumbaru. Mzima lakini Mkuu?
Mkuu habari za kuwajibika ndugu yangu, mi nipo poa kabisa, ila hizi habari kwa uoni wangu hazijitosherezi kabisa, yaani waandishi kumi...! Mwandishi mmoja angetosha sana kutuhabarisha mkuu.
 
We mmoja wao nini? huwezi kutoa kauli kama hiyo kwa wahanga ka sisi. Mimi tarehe 28/5/10 mdogo wangu alipigwa risasi nyumbani kwake Mbezi. Tukamzika tarehe 1/6/10. Wewe leo unasema wakale wapi? Hata haya huoni. Mods I think this guy need he dont deserve to be here. Tunakutaka uombe radhi kwa kauli yako

pole sana ndugu.
 
Back
Top Bottom