Ukiusikiliza mjadala wa TBC juu ya Chanjo ya Corona, utaihurumia Afrika

Hata tukisema tuwapuuze inakuwa ngumu kwa sababu wanapandikiza ujinga kwa wananchi wasio na upeo. Kila kitu kuhusu hizi chanjo kimeshatolewa maelezo ya kitaalam na kina. Tatizo la nchi yetu watu hawana utamaduni wa kusoma, na wale wanaosoma asilimia kubwa wanasoma mambo ya kijinga. Kwanza kwa ujinga wao kashfa zao zinalenga nchi za magharibi tu wakati hata India na China zimetengeneza chanjo zao.
 
Ethiopia haikuwahi tawala lkn ni masikini.Kutawaliwa hakuifanyi nchi kuwa masikini hapo ni sawa na kusema mzee wangu akunisomesha thus Mimi ni masikini.Mzungu aliondoka Tza miaka 60 iliyopita tena alirudi kwao na boksa tu KILA kitu aliacha nchini.Shida ya tza hatujapata kiongozi kwenye uchungu na maendeleo,kama wakoloni wao waliweza tuletea maendeleo hawa wameshindwa nn hali kila kitu kipo.
Wakoloni hawajawahi kuondoka

Achana na ulivyokariri darasani, tumia akili yako uliyopewa na mwenyezi Mungu

Mimi sio msomi sina namna nzuri ya kukuelewesha, nikwambie tu bado tunapambana na ukoloni

Tuacheni
 
Wacha uwongo, Prof Mgaya ni Zoologist not Chemist! UDSM alikuwa anafundisha aquatic life na alikuwa Idara ya Zoology yenye tawi Kunduchi. Hajawahi kuwa Idara ya Kemia, amemfundishaje JPM? Kwanini mnapendaga uwongo humu? If you are not sure of something don't publish instead seek for right facts kwanza.
Wana uhaba wa taarifa, wakishajua kupanua vidole basi wameshakuwa wachambuz wa siasa
 
Prof Mgaya wa NIMRI siyo Mwalimu wa chemistry, Mwalimu wa aquatic science

IMG_20210308_150947_288.jpg


Ulimi hauna mfupa na ndimi hutereza haswa taarifa za kuchakata zinapokuwa nyingi.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Inachukua nchi miaka mingapi kuondokana na hathari za fikra na uchumi za ukoloni !!??
 
Wewe naona hujui maana ya chanjo na upo tayari kujifunza. Tatizo lililopo ni kwamba kuna watu wanaojua vizuri tu uviko-19 lakini wanatulisha matango pori. Kuna kila misinformation, disinformation na hata malinformation( in mama Amon's voice). Lengo la yote haya? Hapo tbc wangekuwepo clinical/medical microbiologists na hasa virologists ambao sio sycophants ungefaidi. Tungejifunza mengi.
We mtu ni kama vile kuna a,b,c za maana unazo lakin nawe umerusha mpira kila mtu acheze. mi lay person, kuhusu chanjo, niko na msimamo wa rais. taarifa halali na haram za nje na ndan mpaka sasa haziruhusu ubongo unaotafakar kukubali hii chanzo. hasa neno mRNA na DNA modification ni maneno ya kusisimua sana. ukiongezea na kipigo cha kununua hiyo chanjo kuzalisha maden yasiyo na kichwa wala miguu, ndo bas tena!
 
Hii ni hatari. Mabandiko yaliyonichefua hadi sasa yako yanaongoza. Unajiita scientist? Kichefuchefu. Labda kama Mgaya alipokea kijiti kwa Mwele yaweza kuwa zamu yako. Si mlikuwa ninyi watatu na mkulu wa nne?

Kwanza hiyo tu kubobea katika botany na chemistry ni ubobezi wa ualimu tu. Kufundisha science ya scientists. Kusoma au kufundisha masomo ya science hakumfanyi mtu kuwa scientist automatically!

Natoa mfano wa Uranium kuelezea tofauti kati ya scientist, engineer na technologist. Unajua uranium ni element. Nafasi yake kwenye periodic table (92) ilijulikana kabla hata mvumbuzi wake hajazaliwa. Marie Curie kaivumbua. Kamaliza. Katunukiwa nishani ya Nobel. Kuna watu kwa kuisoma vizuri uranium wakasema yaweza tumika kuzalisha nishati ya umeme. Wakakokotoa na kiasi kitachozalishwa. Wakamaliza. Wazo lao hadi hapo halijazalisha umeme!

Wakaja wengine wakajenga viwanda/plants(sio mimea) Wakarutubisha uranium. Mchakato wa kuzalisha umeme ukaanza. Umeme ukawaka. Marie Curie ni scientist. Wenye wazo la kutumia uranium katika kuzalisha umeme ni engineers. Wanaojenga plants za kuzalisha umeme ni technologists. Huko chini kabisa ndiko unakuta wanaofundisha au kusoma atomic physics/chemistry. By default wanajiita scientists. Wapi na wapi? Misnomer!
 
Unazunguamzia dawa kupatikana au ugonjwa kuzuka, tumia akili nimekwambia tangu kugunguliwa kwa ARV sio ukimwi
Ukimwi umekuwepo kwa zaidi ya miaka 30, wataalam wetu bado wanafanya utafiti wa chanjo kutukinga na janga hilo au wanasubiri mabeberu watutengenezee ili watizamie, kisha waanze kutuonesha walivyo mahiri na wabobezi katika fani hiyo? Wataalam wasomi tekelezeni wajibu wenu. mmepata bure toeni kwa mshahara!!!
 
Kutarajia kuwa Prof atae msimamo wake binafsi kwenye National TV ni kutarajia mwamba utoe maji bila muujiza.
 
Back
Top Bottom