SoC02 Ukitaka kutatua matatizo yako, tafuta na kusaidia kutatua changamoto za wengine

Stories of Change - 2022 Competition

Elia Lomitu

New Member
Jul 16, 2021
2
1
Furaha kubwa na utoshelevu atakayokuanayo mwanadamu ni pale anapofanya Jambo la kusaidia mwenzake kustawi .

Furaha ya namna hii unayoipata Kwa kumwinua Mtu mwingine kutoka chini kwenda juu ni utajiri haswa na nafsi inayosaidia na jamii Kwa Ujumla.

Utajiri mkubwa na uwekezaji mzuri wa asili ni Kwa Watu

Aliye na watu ni Tajiri. Watu ni chakula" watu ni makazi, watu ni biashara ' watu ni soko. Maisha bwana ni watu.
Unaweza ukawa na maBillioni ya pesa na Bado ukakata tamaa ya maisha na ukaenda kujinyonga. Hivyo pesa sio Utajiri. Utajiri ni kuwatumikia watu wengine.

Fikiri , najua Kila Mtu ana changamoto zake, lakini je' unaweza kufanya Jambo la kumsaidia mwingine?

Ukifikiri vizuri, utaona kuwa pamoja na shida zako, Bado unaweza kutengeneza furaha na tabasamu Kwa nafsi ya Mtu mwingine .

Sikuwahi kufikiri kuwa naweza fadhili Mtu akosome VETA. Lakini nilijaribu na kumbe ninaweza kuchangia kuongeza THAMANI ya Mtu mwingine. Nilijisikia furaha sana.

Kuna Mtu mwenye shida na matatizo mengi lakini anaweza akanunua dozi ya dawa Kwa mgonjwa asiye na uwezo.

Kuna Mtu ni mgonjwa lakini ana chakula cha kumpa mwenye njaa akashiba.

Hakuna anayetumikia wengine , akafa njaa.

Mtumishi wa Wengi ni Tajiri sana. Hakuna aliyewahi kutatua matatizo ya Wengi akawa na maisha mabaya.

CHACHU nzuri katika Uongozi ni kutatua shida za watu wengine. Uchawi mkubwa katika Uongozi ni ubnafsi. Hata katika nchi nyingi na tawala za Dunia, Uongozi hudorora Kwa kukosekana Utumishi Kwa Kiongozi .

Umiliki wa Mali Duniani sio wito kwani hukuzaliwa nayo na hautaondoka navyo utakavyo fariki Dunia . Duniani ulikuja bila kitu na utaondoka bila kitu. Lakini furaha ya kumshika Mtu na kumwinua ni kubwa sana!

Tafsiri ya Umiliki wa vitu Duniani maana yake ni Kuaminiwa kusimamia Kwa ajili ya wengine . Na unaposimamia Kwa ajili ya wengine ndipo na chakula chako kilipo yaani Faida, hisa na kadhalika.

Kama wewe ni mwajiriwa " usimtukane mwenye kampuni kwani Yeye ameambiwa na Mwenyezi Mungu kusimamia kampuni Kwa ajili ya nafsi nyingi , yaani waajiriwa .

Laana ya mfanyakazi Kwa kisa Eti, mshahara mdgo , haitamkuta mwajiri Kwa sababu, mtumishi wa Wengi ni mwajiri na anasimamia Mali Kwa ajili ya wengine .

Ni ukweli unao aminika kuwa katika THAMANI ya Mali/ biashara yenye Bilioni 5 . Bilioni 4.5 sio Mali ya Tajiri Bali ya wadau wengine katika biashara hiyo .

Ukitatua matatizo katika jamii, umefanikiwa kimaisha sana.

Anayepanda Mti wa parachichi, akiwa na Miaka 70, angali akijua kuwa mpaka Mti huo utoa matunda, Yeye hatakueopo, basi huyu anajua maana ya maisha .

Fanya kitu Kwa ajili ya mwingine, hakika hutakuwa fukara.

Stori ya Mbunge wa Arusha ( Gambo), alikotokea ni kuwa , kuna siku Moja aliwahi kumsaidia Raisi JK Kurekebisha Komputer yake, hapo ndipo alipoanzia.

Huwezi ukatatua tatizo la Mtu ukabaki hivyo hivyo.

Unaweza Fanya kitu kidgo Kwa ajili ya mwingine , Fanya Sasa!
 
Back
Top Bottom