Vesper-valens
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 5,287
- 7,388
Habari wakuu,
Miaka ya hivi karibuni kumezuka makampuni mengi yanayouza viwanja, lakini katika hayo makampuni sio yote yanafuata taratibu katika upimaji wa viwanja,hali inayopelekea migogoro mingi wakati wa ku process hati miliki
Kuna umuhimu sana kununua kiwanja kilichopimwa na survey plan yake ni approved tayari wizarani.
Wauzaji wengi wa viwanja wanakuambia viwanja vimepimwa. Ila katika uhalisia ili kujiridhisha na upimwaji wa kiwanja husika ni muhimu muuzaji akuonyeshe approved survey plan kutoka wizarani. Nasisitiza hili coz ilishawai kunitokea nliponunua kiwanja kigamboni kwa kampuni moja hivi
Kuna kampuni iliniuzia kiwanja kigamboni ambacho kina ukubwa wa 960sq, ila kumbe katika upimaji wao walikosea barabara walizibana sana nafkiri ni katika kutafuta faida kubwa zaidi
Sasa kimbembe kikaja walivyokua wanataka kuanza ku process hati walivyopeleka survey plan yao ikakataliwa ...ikabidi watumie surveyor mwingine kuja kupima tena
Walivyopima tena kiwanja changu kikapungua kutoka 960sq mpaka 835sq kutokana na kutanuliwa kwa barabara za mitaa. Ndo survey plan yao ikawa approved wizarani
Hivi viwanja vya siku hizi wauzaji wamekua wanapima kiholela bila kufuata taratibu zilizopitishwa wizarani , mwisho wa siku mtu ukija ku process hati unatumia gharama kubwa sana kutokana na makosa ya waliokuuzia kiwanja
Note:
Tuwe makini sana tunapotaka kununua viwanja hasa sehemu za miji