Ukishindwa kumnyonyesha mtoto miezi sita bila kumpa kitu chochote, andaa pesa ya tuition

Some mothers wana maziwa mengi lakini mepesi, hakuna jinsi zaidi ya kuwalisha kidogo + kunynyesha, la sivyo hicho kilio ni balaa
 
Mtoto Mchanga anatakiwa kupewa maji ya kunywa baada ya miezi mingapi?
 
Vipi kama mama anamnyonyesha pia anampa mtoto maziwa ya ng'ombe Kwa Muda ambao anakuwa mbali na mtoto hususan kuanzia miezi mitatu
 
sasa jmn kuhusiana na mada hiyo mwenzenu yashanitokea hivi nipo katka wakat mgumu hivyo nawaomba ushauri wadau mke wangu anamtoto wa miez 6 kasoro siku lkn nimempa mimba hivyo wadau naomba mnipe ushauri ni jinsi gani nitamlea huyu mtoto ili akuwe vzuri na hal kadhalika nimlee mke wangu akiwa mjamzito yaan huu km mtihan kwangu wajamen
Mpe lishe bora mkeo tena ya ukweli.Pia mtoto apate lishe bora kabisa.Mtoto aendelee kunyonya kama kawaida.Ila kipindi cha ujauzito maziwa ya mama huwa yanapungukiwa viinilishe kwani mama huyo huyo huwa anamlisha mtoto wa Tumboni.
 
Je, kwa mtoto aliyezaliwa na bahati mbaya mama yake akafariki huyo mtoto atapataje rishe nzuri ya maziwa kutoka kwa mama yake?
 
mimi na mwenzangu tumekwenda mbele zaidi miezi nane bila chochote , baada ya hapo vyakula mbali mbali kidogo kidogo isipokuwa SUKARI ama chai mpaka atakapofunga 6 years , mpaka sasa ni mwaka na nusu na matunda ninayaona, hakuna homa za kijinga jinga!
 
Je, kwa mtoto aliyezaliwa na bahati mbaya mama yake akafariki huyo mtoto atapataje rishe nzuri ya maziwa kutoka kwa mama yake?
hakuna namna itabidi kuendana na ushauri wa wataalamu wa masuala ya nutrition, zingatia .....onana na wataalam
 
Yaani kama taarifa zako zinaungwa mkono na takwimu za kiutafiti; basi napendekeza katika fomu za kuomba udiwani, ubunge na urais, kipengele cha kwamba mgombea alinyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita mfululizo kiweke. Napendekeza zaidi ili kukijaza kihitaji ushuhuda kama kile tunachojaza tunapoomba passport, yaani ushahidi usainiwe na wazee watatu kuoka kijijini kwake walio na uhakika kwamba ni kweli mgombea alinyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita mfululizo. Kwa namna hii tutaepuka kupata viongozi wasio na uwezo kiakili kutuongoza.
itatusaidia nini hii kwenye nchi yetu?

Kama hakunyonyeshwa miezi sita hasigombee uongozi au unamaanisha nini?

Je, ni kosa la nani kwa mtoto kutokunyonya miezi sita, mtoto au mzazi?
 
NI KWELI BILA KUPINGA MM WATOTO WANGU WALA HAWAKULISHWA CHOCHOTE NOW WANAMWAKA MMOJA WANAFANYA VITU AMBAVYO NI UN BELIEVABLE KWA KWELI IKIPITA ROKETI JUU ANANILAZIMISHA KWA KUNIPARUA USONI NA ANANYOOSHA KIDOLE ANAONESHA, ANAKATAZA KAMA MTU YEYOTE AKIGUSA CHOCHOTE ALICHOWEKA MAMA AU BABA YAKE KWA KWELI IS TRUE. ACHENI KUWAPA NYONYO BANDIA WATOTO ZA KUBANA MIDOMO WASINYONYE WATAKUA VILAZA MWANZO MWISHO
kuna vitu vingine kabla ya kuviandika tuvifikirie kama kweli vinamaanisha huo u-genius tunaoujadili hapa otherwise tunadanganyana
 
Mimi kuacha ziwa ilikuwa mbinde, nimeenda hadi three years.

Nilianza tuition ya hesabu darasa la sita, masomo ya tuition yakawa yanaongezeka kila mwaka.
Ina maana maziwa ya mama yangu yameExpire au?

Kaka yangu aliacha ziwa mwenyewe at 1year. Mpaka leo hapendi maziwa. Mwenzangu alianza tuition A level. Leo engineer. Mimi? Haha saa nyingine kupotezaga tu Mahela ya tuition haha

Of course unapaswa kunyonyesha mtoto miezi sita bila kitu.
wewe kweli housegirl maana umenichekesha sana kwa comment yako hii. Dah watu wengine i wish hii ingekuwa ni open forum nikuone tu
 
Jamani kumekuwa na tabia ya watu kuwa busy na kushindwa kuwanyonyesha watoto kwa miezi sita bila kuwapa kitu chochote, hili ni kosa na tatizo kubwa sana kwa jamii.

Utafiti unaonyesha watoto wanaonyonyeshwa miezi sita bila kula kitu chochote wanakuwa na kinga imara dhidi ya magonjwa na ubongo mkubwa ukilinganisha na wale wanaoanza kupewa chakula au maji kabla ya muda huo.

Andaa pesa ya tuition kama utashindwa kumnyonyesha mtoto miezi sita mfululizo bila kitu chochote hata kama umempeleka international schools.

Wanawake msiwe busy sana na kazi na kusahau wajibu wenu wa malezi. Lakini pia ni vyema wenza kujipanga vizuri kabla ya kuzaa mtoto ili akizaliwa apate malezi mazuri.

Ukitaka mtoto mwenye afya imara na akili nyingi, anza kwa kumuandaa mke wako kabla ya kumpa mimba na pia lea mimba kwa upendo na uaminifu mkubwa. Mkinge mkeo na magonjwa yanayozuilika akiwa mjamzito. Baada ya mimba mpe malezi mazuri akizaa mpaka miaka miwili kwa maana ya chakula.

Nawaasa watu kuuiga pia utamaduni wa Wachagga katika kulea mke akizaa na utamaduni wa Wairaq katika kulea mimba.

Mkuu Paka, binafsi ninafahamu namna wachagga wanavyolea wazazi baada ya kujifungua lakini sifahamu namna Wairaq wanavyolea mimba kiasi kwamba wanaonekana kuwa mfano wa kuigwa. Kama hutojali tunaomba ueleze kidogo kuhusu hili ili wengi wetu tuweze kujifunza.
 
wachaga wana utamaduni mzuri sana wa kulea mke siku arobaini akijifungua. wachaga mwanamke atachnjiwa mbuzi, kondoo na kupewa chakulakizuri, nenda kwa wenzangu wanyakyusa, mwanamke akijifungua ananunuliwa kila ya nyama na mbalaga. wambulu wao humchinjia mwanamke mbuzi kuanzia pale anapokuwa na miezi minne mpaka kujifungua kama wana uwezo. sasa wenzetu wa morogoro nni taabu tupu


Ujinga ni kitu kibaya sana..aliyekwambia kula nyama sana au kula nyama zaidi ndio utamaduni mzuri au ndio kujenga mtoto mwenye afya njema ni nani?

Tafadhari usipotoshe watu, wewe sio authority kwenye health science, tupe ushahidi wa kisayansi sio kushawishi watu kwa hisia tu. Bahati mbaya sana watanzania wengi siku hizi wanapenda kusikiliza hadithi za vijiweni then wanakurupuka kutekeleza, hizi ramli kwenye maisha ya watu ni mbaya sana.

Mwanafyale, huu uzi wako utapotosha jamii. Najua ni kwa sababu tu ya ujinga, nashawishi watu wajisomee na kufuatilia njia sahihi za kutoa lishe bora.

Jambo moja nakubaliana na wewe na limethibitika kisayansi kupitia kwenye journals na vitabu mbali mbali, ni kweli mtoto anakuwa na kinga imara na afya njema akinyonya maziwa halisi ya mama katika miezi sita ya mwanzo. Mambo ya wachaga kuwa na akili nyingi sijui kitu gani hizi ni gossips.
 
  • Thanks
Reactions: nao
sidhani kama kweli sana,kuna mtoto alinyonua miezi 3 tu maziwa ya mama yakakauka lakini ni tishio darasani kwa sasa tena anasoma hizo shule zenu za national sijui national park
sidhani kama kweli sana,kuna mtoto alinyonua miezi 3 tu maziwa ya mama yakakauka lakini ni tishio darasani kwa sasa tena anasoma hizo shule zenu za national sijui national park
sidhani kama kweli sana,kuna mtoto alinyonua miezi 3 tu maziwa ya mama yakakauka lakini ni tishio darasani kwa sasa tena anasoma hizo shule zenu za national sijui national park
hahahahah et national park
 
wachaga wana utamaduni mzuri sana wa kulea mke siku arobaini akijifungua. wachaga mwanamke atachnjiwa mbuzi, kondoo na kupewa chakulakizuri, nenda kwa wenzangu wanyakyusa, mwanamke akijifungua ananunuliwa kila ya nyama na mbalaga. wambulu wao humchinjia mwanamke mbuzi kuanzia pale anapokuwa na miezi minne mpaka kujifungua kama wana uwezo. sasa wenzetu wa morogoro nni taabu tupu
Mara nyingi tunazaa kutimiza wajibu na ni kawaida kusikia hii mimba ni bahati mbaya.Hata kama ni ndoa,ndio chanzo cha yote hayo.Hata ndege wanatushinda,huanza kuanda viota baada ya hapo watoto waja.Sisi tunazaa kwanza ndio tunakumbuka kuandaa na kujipanga.Ukitaka familia bora na ufurahie wote mke/mpenzi/hawala/nyumba ndogo mjipange kiakili.
 
Back
Top Bottom