Ukimya wa Magufuli TANROADS wazua hofu mpya

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Ukimya wa Magufuli TANROADS wazua hofu mpya

Na Mwandishi Wetu

AHADI iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli kumaliza mgogoro wa uongozi uliodumu kwa muda mrefu ndani ya Wakala wa Barabara

nchini (TANROADS) imezua hofu mpya kutokana na suala hilo kuendelea kubaki gizani.

Ukimya wa waziri huyo anayeaminika na wananchi wengi kutokana na utendaji wake wa vitendo, umeanza kuwapa wasiwasi wafanyakazi wa wizara hiyo walioamini kwamba ahadi yake ya kumaliza suala hilo ndani ya mwezi mmoja na nusu, itatekelezwa haraka.

Baada ya Bw. Magufuli kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuongoza wizara Ujenzi mwishoni mwa mwaka jana, wafanyakazi wengi wa wizara hiyo waliamini kuwa mgogoro ndani ya TANROADS uliosababisha kutoendelea kwa mkataba wa mtendaji wa zamani, Bw. Ephraim Mrema, ungepatiwa jibu haraka kwa nafasi hiyo kujazwa haraka.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya wizara hiyo zimeeleza kwamba kusua kwa Dkt. Magufuli kufanya uteuzi wa kudumu wa nafasi hiyo, kumeanza kujenga hofu mpya hali inayozidisha utata wa uongozi ndani ya wakala huo.

"Ni kitu cha kushangaza kuwa tangu Mheshimiwa Magufuli ateuliwe kushika tena Wizara ya Ujenzi miezi mitatu sasa imepita hali ya uongozi katika wizara hiyo na wakala zake zote ni utata mtupu," kilisema chanzo chetu ndani ya TANROAD na kuongeza;

“Tunavyomfahamu Magufuli ni mchapakazi na sio mcheleweshaji wa mambo na ni mtu wa haki. Hakuzoea kuchelewesha mambo kwa nia ya kupindisha ukweli kwa maslahi binafsi au kuchakachua,lakini tunashangaza safari hii amechukua muda mrefu sana kupanga safu za watendaji wake wakuu.

"Hata hapo TANROADS ni utata mtupu kwani mpaka sasa safu haijapangwa. Tunashangaa mtedaji mkuu wa wakala huo muhimu hajateuliwa hadi leo pamoja na (Waziri Magufuli) kuahidi kulimaliza suala hilo ndani ya mwezi mmoja na nusu."

Vyanzo hivyo vilieleza kuwa hali hiyo inaathiri kwa kiasi kikubwa utendaji ndani ya wizara hiyo kwani hadi sasa hakuna mtu mwenye uhakika wa nafasi aliyo nayo.

"Bora tu angemthibitisha huyo rafiki yake Injinia Mfugale anayekaimu nafasi hiyo kwa sasa ili awe na ujasiri wa kutekeleza na kuamua mambo muhimu ya wakala huo kuliko ilivyo sasa? Hapa wizarani vile vile hakuna mwenye nguvu za kuamua lolote kwani hatujapangwa, imebaki katibu mkuu kuamua kila kitu hata kama ni jambo dogo hii ni hatari sana kwani tunarudi kule kule kabla ya Waziri Magufuli kurejeshwa,” kilisema chanzo hicho na kusisitiza;

"Tunashangaa kwanini imechukua muda mrefu hivyo wakati waziri aliahidi kusukuma kwa kasi na kusimamia haki katika mchakato wa kumpata mtendaji mkuu mpya? Wengine wanasema labda Ikulu ndio inamchelewesha kwani hii sio kawaida yake kwa mambo aliyoahidi.

"Pia inashangaza kwani Mwenyekiti wa Bodi ya TANROADS amekataa kuitisha vikao kwa madai kwamba hakuridhishwa na hatua ya kumwondoa Mrema madarakani bila yeye kuhusishwa? Magufuli naye hili amelifumbia macho," kilidai chanzo hicho na kulalamika.

Hata hivyo chanzo kingine ndani ya wizara ya Ujenzi kilisema kuwa bado wafanyakazi wa wizara hiyo wanaimani kubwa na Dkt. Magufuli kupatia ufumbuzi suala hilo kwa kuwapatia mtendaji mkuu mpya wa TANROADS wakati wowote.

Gazeti hili lilidokezwa kwamba kutokana na hali hiyo kuna wasiwasi kuwa hata nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) iliyotangazwa hivi karibuni, inaweza kuwa kiini macho kwani nafasi zingine zote za watendaji wakuu wa wakala ikiwemo TEMESA, TANROADS, TAA nk. zilizokwisha tangawa, hazijafanyiwa kazi hadi leo.

"Kwa hali ilivyo kuna wasiwasi kwamba watu wengi wenye sifa zinazofaa hawatapeleka maombi kwani wanaona jambo hilo kama ni kuwapotezea muda wao,'kilisema chanzo hicho.

Majira lilipomtafuta Dkt. Magufuli jana alasiri kupata ufafanuzi wa suala hilo, simu yake ilikuwa ikiita kwa muda mfupi bila kupokelewa na kukatika.
 
PHP:
"Bora tu angemthibitisha huyo rafiki yake Injinia  Mfugale anayekaimu  nafasi hiyo kwa sasa ili awe na ujasiri wa  kutekeleza na kuamua mambo  muhimu ya wakala huo kuliko ilivyo sasa?  Hapa wizarani vile vile hakuna  mwenye nguvu za kuamua lolote kwani  hatujapangwa, imebaki katibu mkuu  kuamua kila kitu hata kama ni jambo  dogo hii ni hatari sana kwani  tunarudi kule kule kabla ya Waziri  Magufuli kurejeshwa," kilisema chanzo  hicho na kusisitiza;

Hivi hizi kazi zinatolewa kiurafiki au kulingana na matokeo ya ushindani kwa wale walioomba na wenye sifa?
 
PHP:
Gazeti hili lilidokezwa kwamba kutokana na hali hiyo kuna wasiwasi kuwa   hata nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) iliyotangazwa   hivi karibuni, inaweza kuwa kiini macho kwani nafasi zingine zote za   watendaji wakuu wa wakala ikiwemo TEMESA, TANROADS, TAA nk. zilizokwisha   tangawa, hazijafanyiwa kazi hadi leo. 
 
"Kwa hali ilivyo kuna wasiwasi kwamba watu wengi wenye sifa zinazofaa   hawatapeleka maombi kwani wanaona jambo hilo kama ni kuwapotezea muda   wao,'kilisema chanzo hicho.

Mwenye akilitimamu hawezi kuhangaika na kazi za serikalini ambazo hata kabla haijatangazwa anajulikana atakayeipata.............
 
Ukimya wa Magufuli TANROADS wazua hofu mpya

Na Mwandishi Wetu

AHADI iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli kumaliza mgogoro wa uongozi uliodumu kwa muda mrefu ndani ya Wakala wa Barabara
nchini (TANROADS) imezua hofu mpya kutokana na suala hilo kuendelea kubaki gizani.

Ukimya wa waziri huyo anayeaminika na wananchi wengi kutokana na utendaji wake wa vitendo, umeanza kuwapa wasiwasi wafanyakazi wa wizara hiyo walioamini kwamba ahadi yake ya kumaliza suala hilo ndani ya mwezi mmoja na nusu, itatekelezwa haraka.

Baada ya Bw. Magufuli kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuongoza wizara Ujenzi mwishoni mwa mwaka jana, wafanyakazi wengi wa wizara hiyo waliamini kuwa mgogoro ndani ya TANROADS uliosababisha kutoendelea kwa mkataba wa mtendaji wa zamani, Bw. Ephraim Mrema, ungepatiwa jibu haraka kwa nafasi hiyo kujazwa haraka.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya wizara hiyo zimeeleza kwamba kusua kwa Dkt. Magufuli kufanya uteuzi wa kudumu wa nafasi hiyo, kumeanza kujenga hofu mpya hali inayozidisha utata wa uongozi ndani ya wakala huo.

"Ni kitu cha kushangaza kuwa tangu Mheshimiwa Magufuli ateuliwe kushika tena Wizara ya Ujenzi miezi mitatu sasa imepita hali ya uongozi katika wizara hiyo na wakala zake zote ni utata mtupu," kilisema chanzo chetu ndani ya TANROAD na kuongeza;

Tunavyomfahamu Magufuli ni mchapakazi na sio mcheleweshaji wa mambo na ni mtu wa haki. Hakuzoea kuchelewesha mambo kwa nia ya kupindisha ukweli kwa maslahi binafsi au kuchakachua,lakini tunashangaza safari hii amechukua muda mrefu sana kupanga safu za watendaji wake wakuu.

"Hata hapo TANROADS ni utata mtupu kwani mpaka sasa safu haijapangwa. Tunashangaa mtedaji mkuu wa wakala huo muhimu hajateuliwa hadi leo pamoja na (Waziri Magufuli) kuahidi kulimaliza suala hilo ndani ya mwezi mmoja na nusu."

Vyanzo hivyo vilieleza kuwa hali hiyo inaathiri kwa kiasi kikubwa utendaji ndani ya wizara hiyo kwani hadi sasa hakuna mtu mwenye uhakika wa nafasi aliyo nayo.

"Bora tu angemthibitisha huyo rafiki yake Injinia Mfugale anayekaimu nafasi hiyo kwa sasa ili awe na ujasiri wa kutekeleza na kuamua mambo muhimu ya wakala huo kuliko ilivyo sasa? Hapa wizarani vile vile hakuna mwenye nguvu za kuamua lolote kwani hatujapangwa, imebaki katibu mkuu kuamua kila kitu hata kama ni jambo dogo hii ni hatari sana kwani tunarudi kule kule kabla ya Waziri Magufuli kurejeshwa, kilisema chanzo hicho na kusisitiza;

"Tunashangaa kwanini imechukua muda mrefu hivyo wakati waziri aliahidi kusukuma kwa kasi na kusimamia haki katika mchakato wa kumpata mtendaji mkuu mpya? Wengine wanasema labda Ikulu ndio inamchelewesha kwani hii sio kawaida yake kwa mambo aliyoahidi.

"Pia inashangaza kwani Mwenyekiti wa Bodi ya TANROADS amekataa kuitisha vikao kwa madai kwamba hakuridhishwa na hatua ya kumwondoa Mrema madarakani bila yeye kuhusishwa? Magufuli naye hili amelifumbia macho," kilidai chanzo hicho na kulalamika.

Hata hivyo chanzo kingine ndani ya wizara ya Ujenzi kilisema kuwa bado wafanyakazi wa wizara hiyo wanaimani kubwa na Dkt. Magufuli kupatia ufumbuzi suala hilo kwa kuwapatia mtendaji mkuu mpya wa TANROADS wakati wowote.

Gazeti hili lilidokezwa kwamba kutokana na hali hiyo kuna wasiwasi kuwa hata nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) iliyotangazwa hivi karibuni, inaweza kuwa kiini macho kwani nafasi zingine zote za watendaji wakuu wa wakala ikiwemo TEMESA, TANROADS, TAA nk. zilizokwisha tangawa, hazijafanyiwa kazi hadi leo.

"Kwa hali ilivyo kuna wasiwasi kwamba watu wengi wenye sifa zinazofaa hawatapeleka maombi kwani wanaona jambo hilo kama ni kuwapotezea muda wao,'kilisema chanzo hicho.

Majira lilipomtafuta Dkt. Magufuli jana alasiri kupata ufafanuzi wa suala hilo, simu yake ilikuwa ikiita kwa muda mfupi bila kupokelewa na kukatika.
Daaah kuna mambo yalianza zamani sana, kuna paragraph hapo eti "rafiki yake"
 
Back
Top Bottom