Ukimtongoza mwanamke na akakuambia muwe marafiki kwanza ujue hapo amekukataa tayari jiongeze achana naye

Artifact Collector

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
6,539
10,007
Katika harakati za kutongoza huwaga mwanaume anakutana na majibu mengi mojawapo ni hili la mwanamke kumwambia mwanaume wawe marafiki ukweli ni kwamba hapa umeshakataliwa tayari

Kama mwanamke kavutiwa na mwanaume kamwe hawez mwambia wawe marafiki lazima atamkubali ila kama hajavutiwa na mwanaume mara nyingi anamwambia wawe marafiki kwanza ila ukweli ni kwamba hajavutiwa naye

Mwanamke anayekuambia muwe kwenye friendzone wengi wao ni wastaarabu na jua anajaribu kujitahid kukupenda lakin hakupendi yaan akili inataka hisia hazitaki ni ukweli mchungu ambao mwanaume unatakiwa kukubaliana nao

Mara nyingi hii mbinu huwaga wanatumia wanawake wastaarabu kumkataa mwanaume wale kiburi-flow lazima akutolee maneno ya shombo na dhihaka

Mwanaume ukiambiwa muwe marafiki ni vizuri ukaachana na huyo mwanamke sababu ukiendelea kulazimisha utakuja umia sababu wewe hukuenda kwake kwa ajili ya urafiki bali mahusiano kuulinda moyo wako usiumie ni bora ukaachana naye.

Nimewasilisha
 
Kumtongoza mwanamke ni process inayohitaji kuzingatia vitu vingi na moja wapo ni uwezo wako wa ku predict outcomes before making a move.
Yan kuna mamzingira unapaswa kujua kabisa hapa kwa namna yoyote ile the answer will be no..na kuna mazingira unaweza kutengeneza ili ku guarantee a Yes as an answer
 
Kijana uliyepost inabidi upimwe uanaume wako kwasababu kama ni hivyo itabidi utongoze wanawake wengi sana ambapo pia unaweza usifanikiwe. Enzi za ujinga wangu nilikuwa kama wewe kumbe yule manzi alikuwa ananipenda... ndo siku moja akaniwashia taa ya kijani kwa kuniambia HAPENDI MWANAUME MKATA TAMAA... tulikuja kuwa wapenzi tuliopendana sana kabla ya kutenganishwa na MSUKUMA.
 
Kumtongoza mwanamke ni process inayohitaji kuzingatia vitu vingi na moja wapo ni uwezo wako wa ku predict outcomes before making a move.
Yan kuna mamzingira unapaswa kujua kabisa hapa kwa namna yoyote ile the answer will be no..na kuna mazingira unaweza kutengeneza ili ku guarantee a Yes as an answer
Mimi kuna mchepuko mmoja, sijui naanza kumtongozea wapi.
Akikutana na mimi anakuwa Serious kupita maelezo yani.
Sijui ni uoga ama vipi!!
 
Ni nadra sana kwa mwanamke kubadilisha mtizamo wake wa mara ya kwanza
Sio kweli. Si kila mwanamke anatongozwa haraka.

Mara nyingi akisema hivyo ni hataki kukupoteza. Akikwambia sikutaki ni kwamba utapotea hutokuwa karibu nae naye hataki hilo litokee. Na wakati huo huenda anataka apime kama utamfaa ama laah.

So ni rahisi akiona humfai kabisa wakati mko friend mkabaki friend. Bt ukimfaa mnasogea hatua nyingine.

Ukikubali urafiki wewe endelea kumjali na kuweka ukaribu nae usimtongoze tongoze tena mara mbili mbili. Utakuja shtuka tu mnaanza kuitana babe.😂😂
 
Back
Top Bottom