Ukihiyo wa Polisi Tanzania wazidi kujidhihirisha

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,023
18,562
Kama unataka kudanganya na kupotosha uma, basi ni afadhali hata utumie akili japo kidogo, si kama alivyojidhihirisha huyu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, kwa kile alichokisema;

Alipoulizwa jana kuhusiana na tukio hilo, Kamanda Barlow alithibitisha na kusema kwamba Ofisa Uhamiaji huyo alifananishwa kwa kila kitu na jambazi aliyekuwa anakusudia kwenda kuvamia na kupora katika ghala moja maeneo ya Nyakato ambalo hata hivyo hakulitaja.

Hivi inaingia akilini kwamba mtu anawekewa mtego kwa kukusudia kupora, mbali kabisa na eneo ambalo anakusudia kulipora, na sio mtego unawekwa kwenye eneo ambalo linakusudiwa kuporwa? Na ukimkamata mtu huyo "anayekusudia kupora" mbali na eneo la kupora, utamfikisha mahakamani kwa kosa gani - tulimakamata njiani akiwa anawaza kupora?

Tunajua Polisi wetu wengi ni wavivu wa kutumia akili na wepesi wa kutumia nguvu, lakini wasidhani kwamba Watanzania wote ni wajinga kiasi hicho.

Ukweli ni kwamba bwana Buchafwe ulilengeshwa kuuwawa na mshukuru Muumba wako kwa kukuepusha na kifo.
 
Samahani kwa hili, ni kweli kabisa kimbilio la waliofeli na kwa asilimia kubwa wenye uwezo mdogo kiakili ni polisi, hata awe na cheo gani, polisi wengi wa tanzania ni mbumbumbu wa kutupwa, bahati yao wako chini ya kilaza mwenzao hapo kwenye shombo la samaki kama unavuka kwenda kigamboni
 
Hawa polisi kweli wanakera. Hii kuuwa watu kama wanavyotaka ndiyo itawaangamiza. Inaumiza sana kuona hakuna kati yao mwenye akili timamu. Jamani angalieni ya Kamuhanda. Angalieni Saidi mwema. Ni yupi kati yao ana walau akili timamu? Tumeishia kwenye ujinga na upumbavu mtupu wa watu kuvishwa uniforms na kupewe silaha za kwenda kuulia wenzao wasio na hatia. Je hakuna utaratibi katika training yao unaohusu jinsi ya kufanya kazi kwa maadili? Yaani ni rushwa, kuua, kubambikizia watu makesi na madudu ya kila namna? Mbon auongozi wa hili jeshi hauna hata aibu?
 
jiiungeni wenye akili na shule tupate mabadiliko kwenye polisi!

Ukisoma kuna haja gani ya kwenda kung'arisha buti na amri kibao! Waliokimbia umande utotoni ndo maeneo yao ya kujidai, nguvu kwa wingi akili kidogo...
 
Msilaumu polisi bure. haya yote ni malezi ya nchi ambazo zilifuata siasa za unyama za kikomunisti, Ukifika China na Urussi haya ya bongo ni cha mtoto! Polisi china akikusimamisha tuu , hukuangalia mfukoni na kutabasamu! wewe ingiza mfukoni toa chalo halafu uishie! Pale poland ndio usiseme mkuu, polisi ni mbumbumbu kama debe la mpunga. akikukama mtu raia wa kigeni, basi yeye anajua kapata wali na nyama.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom