BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,379
- 8,123
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt. Ikrah Abdallah ametoa wito kwa Jamii kutofanya tendo la ndoa mara kwa mara badala yake tendo hilo linaweza kufanyika angalau mara Tatu (3) au Nne (4) kwa wiki ili kuondokana na hatari ya kupata UTI
Dkt. Ikrah ametoa ushauri huo wa kitaalamu leo, Jumatatu Januari 15.2024 wakati akifanya mahojiano maalumu Clouds FM kupitia Kipindi cha Power Breakfast
"Tendo la ndoa likifanyika mara kwa mara na lenyewe linamfanya mtu kuwa katika hali hatarishi ya kupata UTI, kwa Wanawake vile vijidudu kutoka pale nje na kuingia ndani vinakuwa katika hali ya haraka zaidi" -Dkt. Ikrah
"Angalau Watu wafanye tendo la ndoa mara Tatu (3) au Nne (4) kwa wiki na mara baada ya kufanya tendo la ndoa tabia ya kutoa haraka kwenye kukojoa au kutoa haja ndogo ni tabia nzuri sana ya kukufanya usipate UTI mara kwa mara" -Dkt. Ikrah