Ukicheka na nyani:polisi watatu wafa ajalini

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
"Polisi watatu wafa katika ajali" Nipashe ya 20/12/2008[/B]Ajali hii ni ya kufunga mwaka wana JF,
Polisi watatu wameuwawa na dereva wa basi pale Kibaha , na dereva huyo kukimbia.
Dereva alisababisha ajali Kibaha na kuua.Akakimbia na basi pamoja na abiria wake mpaka Mikese kilometa karibu 100, mwanaume anakimbia tu!
Yamekuwapo malalamiko mengi kuwa Polisi wa Barabarani wamekuwa kama wanafanya mchezo wa kuigiza katika kudhibiti madereva wazembe, hasa katika barabara zetu za kwenda mikoani.
Hii ajali iliyotokea ya kusikitisha lazima iwaamshe wenzetu wa Polisi Usalama Barabarani kuwa kucheza cheza na hao madereva wa mabasi, hasa yaendayo Mbeya ndiko kuewamaliza wenzao watatu.
Ajali za mabasi ruti hii ya Mbeya zimekithiri, na dereva kuua Polisi na kuondoka, huo ni ujasiri wa pekee.
Polisi Usalama barabarani lazima wajiulize utendaji wao umekaa vipi ili kudhibiti matukio kama haya.
Leo limewatokea , tena wenyewe, ni suala la kusikitisha.
 
.....na sasa wanavuna mabua. Hii yote ni kwaajili ya kuendekeza kitu kidogo. Mpaka hapo watakapo acha kuchukua rushwa ndogondogo kupitia kwenye vifaili wanavyojifanya vya kuchorea ramani na kuandikia namba za magari, madereva makatili wataendelea kuwagonga mpaka watakapojirekebisha
 
[SIZE="[COLOR="Red"]3Polisi watatu wameuwawa na dereva wa basi pale Kibaha , na dereva huyo kukimbia.
Dereva alisababisha ajali Kibaha na kuua.][/COLOR]


Kwa wanaofahamu zigizaga ya kipolisi pale Kibaha, kuanzia mzani mpaka stend, nadhani washukuru kwamba ambao hawakuuwawa ni abiria. Pako shaghalabhaghala sana pale, hasa between 630 and 10 am.

Kuna sababu ya kumlaumu dereva, kwanza kwa sababu kaua, pili kwa kuwa alikimbia. Lakini hatuna sababu ya kumuhukumu. Kwa jinsi Kibaha ilivyo, kama fair play ya kisheria ikichezeshwa, wale POLICE wanaweza kuwa na makosa kabisa. Haiwezekani wafe watatu wenyewe tu. Lazima dereva alikuwa anajua na kuna kisa before.
 
Back
Top Bottom