Ukichaa wa akili ya mwanadamu tatizo kubwa Duniani

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,564
3,472
Hakuna kipindi ambacho jamii yetu inahitaji elimu ya kujifahamu "consciousness education"kama sasa. Tunapita kwenye kipindi chenye upotofu mwingi juu ya "mtu ni nani " kuliko kipindi chochote kile.

Taasisi za misingi ya jamii kama familia, shule na maeneo ya ibada leo kwa kiasi kikubwa zimepelea sana kuhakikisha mwanajamii anajitambua yeye ni nani ili kupunguza matatizo ya ukichaa wa mwanadamu kutokujifahamu badala yake zimekuwa zikiongeza ugumu wa mtu kujifahamu. Siyo ajabu leo kumkuta mtu akijitambua kwa vitu, kazi hadhi n.k.

Elimu imekuwa ikiwaandaa watu kufikiri kina kuliko kujifahamu Kwa kina. Ikumbukwe kufikiri bila kujifahamu ni utata mwingine wa uwepo wa binadamu. Kufikiri ni sehemu ndogo sana ya kujifahamu. Ndiyo maana leo tuna tuna wafikirifu wakubwa ndani ya ukichaa wa akili ya mwanadamu. Usishangae hata Profesa akifanya kituko, ukichaa kwenye akili ya mwanadamu katika kizazi chetu ni zaidi ya janga la ulimwengu.

Kutokana na ukichaa kwenye akili ya wanadamu leo mahitaji ya msingi kwa mwanadamu kama vile; chakula, mavazi na malazi hayapatikani watu wote kutokana na kutokuwepo kwa usawa katika mgawanyo wa raslimali kunakosababishwa na binadamu. Yaani kuna wachache waliotanguliza uchu na ubinfsi na hivyo wao kuhitaji kupata zaidi kuliko wenzao "insane and rapacious need/ greed of the ego".Tunaishi katika zama ambazo kila kitu kimeingizwa kwenye dijiti ikiwemo raslimali watu kwa lengo la kutafuta kupata zaidi.

View attachment 2764257
 
Yaani kuna wachache waliotanguliza uchu na ubinfsi na hivyo wao kuhitaji kupata zaidi kuliko wenzao "insane and rapacious need/ greed of the ego".Tunaishi katika zama ambazo kila kitu kimeingizwa kwenye dijiti ikiwemo raslimali watu kwa lengo la kutafuta kupata zaidi.

Sio kweli.
Nani amekuzuia wewe kuwa kati ya hao wachache au kujimilikisha mali?
Nani amekuzuia wewe kupata zaidi ya wengine?
 
Data ziko wapi?
Wewe unaeona wenzako wana shida ya akili ndio mwenye shida ndiomaana haupo kati ya wanaolamba asali au kuishi maisha bora.

Soma kwa kuelewa sijaandika kujionesha kuwa mimi ni malaika ila kuonesha tabia ya ukichaa tuliyonayo wanadamu na namna inavuotuathiri.
Tabia hii mtu yeyote (Mimi/ wewe n.k) anaweza kuwa nayo.
..................................
 
Sio kweli.
Nani amekuzuia wewe kuwa kati ya hao wachache au kujimilikisha mali?
Nani amekuzuia wewe kupata zaidi ya wengine?
Sijazungumzia Mimi kuzuiliwa ila nimezungumzia hali hii ya ukichaa ambayo ni tatizo katika akili zetu.
......................
Jenga hoja basi acha personal attack...haisaidii kitu, kama kuna upotofu uweke wazi ujadiliwe.
 
Data ziko wapi?
Wewe unaeona wenzako wana shida ya akili ndio mwenye shida ndiomaana haupo kati ya wanaolamba asali au kuishi maisha bora.
Ndugu,
Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa inakadiriwa Duniani kuwa na watu Bilioni 8. Inasemekana pia pamoja na ongezeko hilo bado raslimali za kustahimili ongezeko zinaongezeka.
........................................................
 
Hakuna kipindi ambacho jamii yetu inahitaji elimu ya kujifahamu "consciousness education"kama sasa. Tunapita kwenye kipindi chenye upotofu mwingi juu ya "mtu ni nani " kuliko kipindi chochote kile.

Taasisi za misingi ya jamii kama familia, shule na maeneo ya ibada leo kwa kiasi kikubwa zimepelea sana kuhakikisha mwanajamii anajitambua yeye ni nani ili kupunguza matatizo ya ukichaa wa mwanadamu kutokujifahamu badala yake zimekuwa zikiongeza ugumu wa mtu kujifahamu. Siyo ajabu leo kumkuta mtu akijitambua kwa vitu, kazi hadhi n.k.

Elimu imekuwa ikiwaandaa watu kufikiri kina kuliko kujifahamu Kwa kina. Ikumbukwe kufikiri bila kujifahamu ni utata mwingine wa uwepo wa binadamu. Kufikiri ni sehemu ndogo sana ya kujifahamu. Ndiyo maana leo tuna tuna wafikirifu wakubwa ndani ya ukichaa wa akili ya mwanadamu. Usishangae hata Profesa akifanya kituko, ukichaa kwenye akili ya mwanadamu katika kizazi chetu ni zaidi ya janga la ulimwengu.

Kutokana na ukichaa kwenye akili ya wanadamu leo mahitaji ya msingi kwa mwanadamu kama vile; chakula, mavazi na malazi hayapatikani watu wote kutokana na kutokuwepo kwa usawa katika mgawanyo wa raslimali kunakosababishwa na binadamu. Yaani kuna wachache waliotanguliza uchu na ubinfsi na hivyo wao kuhitaji kupata zaidi kuliko wenzao "insane and rapacious need/ greed of the ego".Tunaishi katika zama ambazo kila kitu kimeingizwa kwenye dijiti ikiwemo raslimali watu kwa lengo la kutafuta kupata zaidi.
0923a93ead13c585b5535cc661e94b73.jpg
33d651ad0f39f37ff5cb8809b40a6c3d.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom