Ukibadili mke zaidi ya mara mbili mwenye shida ni wewe

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,929
Kwa aina hii ya ndoa za kisasa ambazo hazina vetting ya kutosha kupata mwenza bora ni turufu.. Yaani ni sawa na kubet kisha upatie
Kwa kasi hii ya talaka.. Rejea ripoti ya RITA ni wazi ndoa hizi za kileo huangukia pua baada ya muda mfupi na sababu kubwa zikiwa tuhuma za usaliti, kiburi, uchafu, uchawi, wakwe, ndugu, changamoto za maisha nk

Ndoa hizi za kileo huangazia zaidi, kipato, mwonekano ama umaarufu.. Hisia na upendo hujengwa kwenye misingi hiyo na ndio maana wengi hufeli baada ya muda mfupi.. Kwakuwa hisia na upendo havipewi kipaumbele no 1

Baada ya ndoa kila kitu hubadilika
Simu na chatting za kila saa hukoma
Kurushiana vocha na kutumiana pesa hupungua kabisa
Outings ni mpaka kuwe na sherehe..!

Mnalala chumba kimoja, kitanda kimoja
Sasa mnaonana kila siku mtake msitake.. Ni kwenye ukaribu huu ndio kasoro na mapungufu ya kila mmoja yanaanza kuonekana! Taratibu zile hisia na upendo vinaanza kutoweka! Unaanza kuona kero kila mwenza wako awapo karibu yako

Hapa ndio penye role ya mwanaume kuonesha ukomavu.. Kama amekua kiakili lakini.. Maisha kabla ya ndoa ni tofauti kabisa na maisha ndani ya ndoa.. Mambo mengi hubadilika. Na wanaume wengi hushindiwa hapa!
Wanawake wengi huongozwa na hisia.. Mpe kila kitu lakini KAMWE! usiache wala usisahau kuwekeza kwenye hisia zake tena kwa vitu vidogo kabisa..! Kile ambacho kilimfanya akanasa kwenye mtego wako kihisia USIKIACHE kamwe! Ukokosea hapo utachapiwa mpaka na usioeadhania
Wanaume wengi hupenda kuheshimiwa na kutumikiwa, wanapenda kunyenyekewa, sometimes kwa vitu vya kijinga kabisa!

Kwa maisha ya sasa wengi huingia kwenye ndoa bila kuyajua haya mengi ya msingi, lakini mwanaume ndio mwenye jukumu kubwa la kuona ndoa inastawi ama inakufa! Kuna mahali inafika hakuna namna tena, baada ya kufanya jitihada zote na kushindikana.. Hapo ni kumwacha aende ukizidi kukomaa naye atakuua!
Kwahiyo ndoa ya kwanza inakuwa kama chuo. Ukiingia kwenye ndoa ya pili unakuwa ni mhitimu uliyeiva huwezi kubabaika tena kuanzia kwenye uchaguzi, mahusiano ya awali mpaka kwenye ndoa.. Kuzinguliwa kupo lakini sasa una uzoefu hubabaiki tena!

Shida itakuja kama na hii ya pili itakushinda, pengine unaweza kusameheka! Kwamba out of frustration ukaingia chaka tena! Lakini ikija na ya tatu tena.. Aaah hapo mwenye shida ni wewe sasa ... Na jamii itaanza kuhoji mengi kukuhusu

Kuna mtangazaji nadhani kila mwaka anaolewa tena! Hii ni special case.. Pengine huyu Kunguru hafugiki!!!!
 
b53da5b2-89d8-4b84-ad78-d5cd23bfe045.jpg
 
Ndoa ndoana!! Just imagine unapenda na kumheshimu mkeo afu kuna vijana wa ovyo wanapuliza honi??
Heshima ni nje huko upepuni.. Pale kitandani ni jihad blaza.. Pale ni ufundi na utundu pale hupigi kwa jina la baba...
 
Tulisemaga hayana forumula sio! Au fomla imepatikana, mshana unazungumziaje kuhusu suala la nyota kwenye uchaguz wa mpenzi
 
Back
Top Bottom