Ukatili wa kutisha: Mume amng'oa meno kwa praizi Mke na kumtoboa jicho kwa bisibisi

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
IMG_20230528_000521_701.jpg


Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Jackline Mnkonyi{38} mkazi wa Sombetini Jijini Arusha amejeruhiwa vibaya kwa kipigo kikali kutoka kwa mume wake, Isaac Mnyagi ikiwa ni pamoja na kung’olewa jino la mbele na kutobolewa jicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi

Akizungumza kwa tabu na waandishi wa habari nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sinoni, Daraja Mbili Jijini Arusha, Jackline ambaye anamtoto mchanga, alidai kuwa baada ya kipigo hicho mume alimpakia kwenye gari yake akiwa hajitambui na kwenda kumtupa getini nyumbani kwa wazazi wake Sinoni.

Akizungumza Mkasa huo alisema kuwa, mchana wa mei 23 mwaka huu alitembelewa na mjomba wake ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} mkoa wa Simiyu, Vicenti Matai kwa lengo la kumsalimia.

Alisema mume wake huyo aitwaye, Isaack Mnyagi ambaye ni Mwalimu aliyezaa naye watoto wawili, amekuwa na tabia ya kumpiga pindi anapofika nyumbani kwake baada ya muda wa zaidi ya miezi mitatu na siku ya tukio alikuja ghafla majira ya usiku.

IMG-20230526-WA0041.jpg

IMG_0613.jpeg

Bwana Isaac Mnyagi

Alisema siku ya tukio mumewe alifika nyumbani kwake majira ya saa 4.45 usiku na kugonga mlango na kufunguliwa na watoto, lakini hakutaka salamu na mkewe ila aliingia chumbani na alipomfuata alitoka chumbani.

Jackline alipoona hivyo alimuuliza kulikoni na alichoambulia ni maneno mazito na matusi na kuulizwa mchana alikuwa na nani na kumjibu kuwa alikuwa na mjomba wake hatua ambayo alikana ndipo alipoanza kumshambulia kwa ngumi, mateke na mkanda na baadaye alichukua Praizi na kumng'oa jino kwa nguvu.

"Nilijitahidi sana kujieleza lakini ilishindikana alianza kunipiga kwa mateke na ngumi na alichukua Plaizi na kuniamuru nifungue mdomo na kuning’oa jino moja ambapo damu zilianza kuchuruzika na kuanguka chini"

Alisema licha ya kipigo hicho pia alichukua kitu chenye Icha kali na kumtoboa jicho moja ambalo hadi sasa hawezi kuona huku akimwambia maneno mazito na kumtishia kumuua.


Alisema hakujua jinsi alivyofikishwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni Daraja mbili na kutupwa getini kwani alishtukia akiwa hospitali.

‘’Nimetobolewa jicho na kung’olewa jino na Plaizi nina maumivi makali sana naiomba serikali ichukue hatua dhidi ya mume wangu kwani amenifanyia unyama wa hali ya juu sana’’alisema Jackline

Naye baba mzazi wa Jackline, Elimilis Mnkonyi alisema siku ya tukio wakiwa nyumbani majira ya saa saba usiku walipokea simu kutoka kwa mwanaume huyo akiwataka wakachukue mzoga wao hapo nje.

Alisema akiwa na mke wake, walienda hapo getini na kumkuta mtoto wao Jackline akiwa hajitambui na kuamua kumpeleka katika hospital ya Rufaa ya Mount Meru na baadaye alienda kutoa taarifa kituo cha polisi kupitia jalada namba ARS/RB/5416/2023.

"Baada ya kutoa taarifa polisi tulienda kumtafuta mtuhumiwa lakini ametoroka na polisi wanaendelea kumsaka"

Mkonyi mwenye watoto nane na wajukuuu 16, alifafanua kwamba mtoto wale alikuw aameolewa a mume wa ndoa lakini walitengana na kuamua kuishi na mwanaume huyo ambaye hata hivyo hakuwahi kujitambulisha kwake licha ya kusikia malalamiko ya ugomvi wa mara kwa mara.

Mkonyi alisema kuwa mtoto wake, Jackline aliwahi kumweleza mama yake kuwa mwanaume huyo amekuwa na tabia ya kumpiga mara kwa mara lakini yeye hajawahi kuelezwa kwani mtoto wa kike huongea zaidi na mama na hadi sasa hajulikani alipo mara baada ya kufanya tukio hilo la kinyama kwa jamii.

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Justin Msejo hakuweza kupatikana kwa simu yake ya kiganjani kuelezea tukio hilo kama mtuhumiwa ameshakamatwa au la kwani simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

UPDATES...
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Msejo amesema “Taarifa hizo zipo tunazifanyia kazi, tunaendelea kumtafuta mtuhumiwa kwa kushirikiana na Wananchi, tunaamini Mtuhumiwa anasoma mitandao na anaona kinachoendelea.”
 
Yaani misambwanda ilivyojaa mjini,kweli unapiga mwanamke kwa ajiri ya wivu!!dume la namna hii ni kichaa kabisa,piga mke kama anataka kudhulumu Mali Yako, nyumba, shamba, kampuni, lakini mke kaamua kutanua miguu apigwe pipe! mi nikasirike na kupiga,https://jamii.app/JFUserGuide no!

Mwache aende, oa mwingine
 
Pole yake Dada Jack line jamani.. Hichi kifume kijiandae kutumia debe kama choo muda mrefu, sasa hapo kakimbia akiamini hatopatikani... Kajipa hasara kibao ktk Maisha kwa maamuzi ya hovyo

1.kapoteza Amani ya maisha hapa duniani

2. Atapoteza hela kila anapohisi mtu ana jua.... Itabidi awanyamanzishe kwa tip

3. Laana litamfuata kila aendapo hatapata mke... Maana hata ajifanye mwema karma itafanya ajulikane ni mtu mbaya
3.huenda mtoto au watoto alizaa na bibi asiwaone Tena.. Au akiwa ona itakua kama wale wa lemutz😢😢
 
Chugga chugani bablah,😀😀 watu WA kaskazini miyeyusho sana,na manzi mzembe sana unasindwaje kupiga makelele usaidiwe,ila wanawake sometimes wanakuwaga mafala anaweza kuuliwa uku anajiona ili kumtunzia Siri njemba,mademu acheni huo usenge,unapigwa umetulia tu kama mpo kitandani kwenye sexy😀😀
 
Back
Top Bottom