Ukatili wa Kijinsia kwa watoto Kanisani: Tupinge kuita watoto wachawi mbele ya kanisa na kuwarekodi kwente tv na redio

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,957
22,156
Tukielekea kuadhimisha wiki ya ukatili wa kijjnsia kuna mambo yanaendelea baadhi ha makanisa ya manabii mitume na makuhani hayanipendezi.

Kuna mambo ukienda makanisani kwa watajwa hapo juu naumia sana.

Wanaita watoto wadogo kabisa wanawambia wewe uko kikundi cha wachawi. Kwa uwoga wanajibu ndio. Wanaulizwa umeingizwa na nani? Unasikia bibi mzaa mama ama babu mzaa bibi.

Jamani mjue shetani nae ni mwongo na mdanganyifu. Tusikubali kudhalilisha hawa watoto makanisani.

Waziri husika tunaomba mwonye haya mambo madhara yake ni makubwa.

Hawa watoto wanasoma wanahitaji kuwa na familia zao. Imagine mtu anawaona kwenge tv unahisi shuleni si wanawaita wachawi hao?

Mtoto unamtesa kisaikolojia haijalishi mlimpanga ajibu hivyo.

Kingine unasimamisha mtoto unamwambia wewe unahusika na wachawi anajibu hapana. Unalazimisha hutaki nikusaidie anakujibu unisaidie nini? Kama ni redio wakisikia haya majibu wanapozi kabisa na tv unakuta sauti haitoki why?

Kama mnahisi mtoto huyu anahusika na uchawi, mtume mtumishi amchukue na wazazi wake mpelekeni mahema ya maombi haina ulazima kuwaonesha watoto wadogo wakikiri wao ni wachawi.

Tuache kudhalilisha watoto makanisani.
 
Wachawi hamtaki Siri zenu ziwekwe wazi...

Tumewastukia...

Sikuhizi tunawajua Siri zenu...
 
Wachawi hamtaki Siri zenu ziwekwe wazi...

Tumewastukia...

Sikuhizi tunawajua Siri zenu...
Hapana Donatila. Ukristo hauko kumdhalilisha mtu.

Soma biblia vizuri, manabii walitumwa kwenda kumuonya mtu dhambi zake kibinafsi na hawakutangaza hadharani...rejea:

Isaya kumuonya Hezekia, Elia kumkemea Ahabu.

Mungu hushughulika na mtu. Mungu huwa hamdhslilishi mtu vinginevyo wanawake michepuko dhambi zao Mungu angezifunua kwa waume zao.

Kinachofanyika makanisani ni biashara ya maombi.

Manabii fake wamefarakanisha ndoa na ndugu kwa kuwaita wachawi. Katika hili biblia inasema HERI WAPATANISHI.

Lakini sasa mitume wenu fake wanafarakanisha.

Sikiliza...Mungu anamhitaji hata mchawi aokoke.

Ninasisitiza makanisa fake yaache kudhalilisha watu

Niitieni

Dkt. Gwajima D

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom