Ukarabati wa kituo cha polisi mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,961
2,138
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC).Thobias Andengenye akipanda mti wa ukumbusho wa uzinduzi wa kituo cha polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha baada ya kukarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967 na kugharimu kiasi cha shilingi milioni moja!
008.jpg

Kinachonisikitisha kuhusu tukio hili ni kuwa, hiki kituo kimekaa bila ukarabati kwa muda mrefu (miaka 45); na kumbe gharama ya ukarabati ni ndogo tu (Tshs 1,000,000 sawa na US $ 633) tu. Je ni kweli tunahitaji mpaka kampuni ya Vodacom ije kufanya ukarabati huu wa gharama kidogo namna hii? Ajabu katika tukio hili la matumizi ya US $ 633 tunamhusisha Kamanda wa mkoa, lakini inapofika wananchi wamepatwa na maafa makubwa (zaidi ya US $ 633); kamanda wa mkoa hawezi kuonekana. Ni ushauri wa bure tu, taasisi za serikali ziyaelekeze mashirika makubwa kama Vodacom, Barrick etc kwenye miradi mikubwa au kusaidia yanapotokea majanga makubwa!!!
 
Tatizo mkuu kwa serikali ukute BoQ za ukarabati huo zilikuwa mamilioni ya shilingi. Cha ajabu hela aliyotumia kwenda kufungua kituo hicho ni zaidi ya fedha ya ukarabati huo! Hiyo ndo ya baba mwana X!
 
Back
Top Bottom