Ukaguzi wa vyeti vya taaluma ya udereva

Ntinje

Senior Member
Feb 2, 2019
118
100
Habari wadau!

Katika mitandao ya kijamii kuna clip inamuonesha Kamanda wa usalama barabarani akiongelea juu ya ukaguzi wa vyeti vya taaluma ya udereva. Nasisitiza hapa amesema MADEREVA WOTE WA MAGARI. Narudia " MADEREVA WOTE WA MAGARI WATEMBEE NA NAKALA ". Hatua kama hiyo italeta taafurani nyingine katika nchi hii.

Swali:
Huyu aliyeko barabarani anaendesha gari, nani alimpatia hiyo leseni ya udereva? Je aliipata pasipo kuonesha cheti cha mafunzo? Basi hapo ndipo tunajifunza kuwa " kila katika kani ya kutenda kuna kani mkabala inayolingana nayo" maana yake huyu mtu hawezi kuwajibika peke yake lazima na mamlaka iliyotoa leseni iwajibike.

Hoja fikirishi:
Wapo watu mbalimbali ambao hawajapita shule lakini bado ni wazuri katika fani hiyo kuzidi hata wale waliopita katika mafunzo huko darasani. Watu wa mfano kama huo, wizara ya elimu ilifika mahala ikawatambua watu wajuzi ambao hawajapita katika mifumo isiyo rasmi. (Binafsi nawapenda sana, they are more practical). Hivyo, basi endapo mnaona inafaa basi mrasimishe uhalali wao.

Ushauri wa ziada:
1. Kutizama mifumo yetu wapi tulikosea na tuanze kurekebisha siyo hizo hatua ambazo tunataka kuzichukua. Ukitizama kwa sasa "rate" za ajali zimepungua na bado hata zile zilizopo source yake kubwa si uzembe wa madereva bali ni sababu nyingi kadha wa kadha zikiwemo ubovu wa barabara. Ebu niombe tuwaache wananchi wafanye kazi zao.

2. Pia nishauri sana wale waliopewa dhamana ya kuongoza watu (except P, VP, PM) tunao wajibu mkubwa sana wa kutafakari ni namna gani tuna wasaidia hawa viongozi wetu wakubwa (P, VP and PM) na siyo kuleta mambo yatakayowagombanisha na raia.

Asante.

Mungu ibariki JMT
 
Kwanza kabla sijachangia nikushauri uwe unaandika sentesi kwa vituo na paragraph.

Back to the topic.

Ukaguzi uliotangazwa ni wa kawaida na unahusisha madereva wa magari makubwa ya abiria na unafanyika mara kwa mara na hata ukienda ku renew leseni class C lazima uende na cheti.

So ni kawaida na usiogope.
 
Back
Top Bottom