mafutamingi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 2,772
- 2,171
John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA amekuwa akisisitiza umuhimu wa kukagua mfumo (software) ya kujumlisha kura (tallying). Rai ya Mnyika inatokana na hofu kwamba mfumo huo unaweza kuwa mkondo wa kuiba kura. Lakini NEC kupitia kwa Mwenyekiti wake amekaririwa akisema sheria hairuhusu ukaguzi wa mfumo huo kufanywa na vyma vya siasa. Ameendelea kusema kwamba vyama vya siasa vitaonyeshwa jinsi mfumo huo unavyofanya kazi lakini hawataruhusu ukaguzi wa aina yoyote kufanyika.
Mimi nadhani Jaji Lubuva angetumia busara kuondoa shaka ya aina yoyote kwamba wizi wa kura utafanyika kupitia mfumo huo. Ni kweli kwamba hakuna sheria inayotaka ukaguzi wa mfumo huo ufanywe na chama chochote cha siasa. Lakini kwa upande mwingine hakuna sheria yoyote inayokataza ukaguzi huo kufanywa. Jaji Lubuva atumiwe busara na aruhusu chama chochote kifanye ukaguzi. Kama ana hakika software hiyo iko intact, kwa nini awakatalie?