Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,277
- 17,983
WADAU. Nimekuwamsikilizaji wa kipindi cha asubuhi cha Clouds FM cha Power Breakfast, ambachoni maarufu sana siku hizi, siku za karibuni GERALD HANDO kupitia segment yakeya Jicho la Ngombe amedhihirisha dhamira yake hasi kwa taifa letu, dhamirailiyojaa unafiki mkubwa.
HakikaGerald amejivika kuwa mtetezi wa maovu ya serikali, hususan bajeti hii ambayohata serikali yenyewe imekiri kuwa ni mbovu ikifanya mkakati wa kuiboresha.Ndugu zangu wenye nia thabiti ya kuleta mabadiliko katika mfumo mbovu wa serikalihii, nawaomba tuungane kwa nguvu zetu zote kukataa propaganda chafu za GeraldHando (siamini kama ni msimamo wa Clouds Fm kama ndivyo wawathibitishiewananchi).
Leo asubuhiamewakejeli wabunge wetu wote wanaoikosoa bajeti hii, akidai wanatafutaattention kwa wananchi, tena akienda mbali kwa kudai ni watovu wa nidhamu kwababa yao (Rais), tena hawafanyi kilichowapeleka bungeni. Hivi yeye ni nanimpaka atoe kashfa zote hizo? Au kwa kuwa amepewa jukwaa la kubwabwaja. Hakikanimemshusha thamani kwa hoja zake dhaifu!
Wadau,naandika kwa urefu nikiwa very disappointed na hawa wana habari uchwara (kamaGerald Hando) ambao wanaweka maslahi yao badala ya umma. Sielewi kwa mtazamo waGerald Hando wabunge kazi yako bungeni ni ipi kama sio kuihoji na kuibanaserikali, yawezekana hawafahamu hata majukumu ya mbunge (inataka elimu ilikujua hilo sijui kama anayo), anataka waende kusinzia kama baadhiwalivyochukuliwa na picha?.
Iwapoameamua kuwa msemaji wa serikali ya CCM, basi tujulishwe kwani hatuna tatizo naRadio Uhuru amabyo ni propaganda machine ya CCM, kila mtu anajua hilo na hatuna tatizao nalo, ilawapigania ukombozi wa kweli tutaendelea kuibana serikali, tukiwatumia wabungewetu kama Mnyika kueleza umma uozo wa serikali hii, asitukatishe tama kwanihatofanikiwa kamwe. Hongera Mnyika tuko nyuma yako katika hili.
Aluta Kontinua mpakaserikali itambue haki ya wananchi. Ole wao wanafiki siku zao zinahesabika
Hicho kipindi kilikufa baada ya "vichwa" wawili kutoka pale. Kipanya na hasa Fina Mango. Huyo Hando ndio aliwasaliti hao wawili hadi wakafukuzwa kazi. mwisho wa CCM ndio mwisho wa Radio hii