Ujirani mwema. . . ?Ama. . . .?

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,821
59,411
Hamna ubaya wowote mtu kuwa karibu na jiraniye maana ukaribu huo unaweza ukazaa urafiki sawa na undugu ukapata mtu wa kusaidiana nae.
Anyway kuna ambalo mie nimeshindwa kujua nia yake kwahiyo nataka kujua wanajamvi mnalionaje.

Kuna wanandoa wamehamia sehemu mpya hata mwezi haujaisha, wanapoishi ni ndani ya geti ambapo mwenye nyumba anaishi pamoja na mpangaji mwingine (mtu na mkewe, mtoto na dada wa kazi).

Hawa wapangaji wapya hawana dada wa kazi ila mke ni mjamwepesi kwahiyo kushirikiana muhimu. Sasa juzi jioni kaka alikua anamsaidia mkewe kuosha vyombo nje kwenye karo wakati ye anapika, mara yule mke wa jirani yao (mpangaji mwenza) akatoka nje na kumkuta yule kaka akiosha vyombo. Yule dada akamuuliza 'kheee unaosha vyombo'? Kaka akajibu 'ndio' tu alafu akaendelea. Dada akatoa offer. . .'acha nanii (dada wake wa kazi) atakusaidia'.

Sasa mhusika anajiuliza na kuuliza ni kwamba yule jirani aliona mumewe anaonewa kuosha vyombo akamuonea huruma ama? Au jirani anachokonoa tu ya watu akiwa hajui wanaishi vipi?Inahusu kutoa msaada kwa mume wa mtu bila kuombwa ikiwa mkewe yupo? Au ndio mafumbo ya "kwanini unaosha
vyombo na mwanamke unae?"

Mie nimeshindwa kujua kama ndo kujaliana kwa majirani au kuna jingine.
 
Hahha Lizzy, ningeshangaa sana kwanza kama mkaka alikubali!! Ninavyohisia haya ni makubaliano ya yeye na mkewe so akikubali kusaidiwa na msaidizi wa nyumba ya pili ni wazi makubaliano yake na mkewe hayakuwa ya ukweli bali either ya kinafiki au kushurtishwa.

Mke wa jirani naye mh! Haiba ya kike imemwishia akha!!
 
interesting
ndo maana ulikuwa missed here...lol

huyo dada alietoa offer ni mnafiki

alipaswa kumfuata mwanamke mwenzie na kutoa offer hiyo...

sio kumvaa tu 'mume wa mtu na kujifanya unashangaa anaosha vyombo
while unajua mkewe ni mjamzito'

visa hivyo...
 
The Boss hapo sasa, yaani unaanza tu vruuuum kwa mume wa jirani?? Mwe! Mbona shughuli?
Ni kweli usemayo mke wa jirani wa kuzoeana naye ni mke na si mume akha!!
 
Hahha Lizzy, ningeshangaa sana kwanza kama mkaka alikubali!! Ninavyohisia haya ni makubaliano ya yeye na mkewe so akikubali kusaidiwa na msaidizi wa nyumba ya pili ni wazi makubaliano yake na mkewe hayakuwa ya ukweli bali either ya kinafiki au kushurtishwa.

Mke wa jirani naye mh! Haiba ya kike imemwishia akha!!

Mamii mie nlikua nafikiria kama wewe ila nikawa naogopa labda sijafunzwa tabia nzuri ndo maana nikaona msaada wa style hiyo sio.

Kweli kazi ipo.
 
interesting
ndo maana ulikuwa missed here...lol

huyo dada alietoa offer ni mnafiki

alipaswa kumfuata mwanamke mwenzie na kutoa offer hiyo...

sio kumvaa tu 'mume wa mtu na kujifanya unashangaa anaosha vyombo
while unajua mkewe ni mjamzito'

visa hivyo...

Lolzzzz Boss. . . .

Ila kweli kumfata mwenzie na kumwambia "nimeona mzee anaosha vyombo, kama kazi zinakuzidia tupo wa kukusaidia mzee nae apumzike" ingekua more appropriate. Ni kama mwanaume mwenzio ajitolee kumsaidia mkeo kazi ya kukata majani na wewe upo bila kujua makubaliano yenu.
 
exactly...
 
Lazima atakuja kumsaidia mwanamke mwenzie na kazi zile za usiku.
 
Inaweza kuwa kwenye 'contexts' mbili:
1.Ni ile tu ya jirani kutaka kujionyesha kuwa na yeye yupo..i mean kuwachokonoa..but ili hii ipate mashiko ni lazima kujua kama mahusiano ya hawa majirani ndani ya huu mwezi mmoja yalikuwaje?..mabaya,ya kawaida au mazuri!
2.Just in a good faith..hii inaweza kuwa tu imebebwa na ile dhana ya 'mtibu kwanza mgonjwa PF3 baadaye'!..
However. all in all..mwezi mmoja ni muda kidogo kuja na 'a negative analysis'..binafsi ningelalia on a 'goodwill basis'
 
Huyo mwanaume ni mjinga tu alikosa kukaa kimya, ningekuwa mimi ningemwambia hivi; Mke wangu ni mshauri wangu, sio mfanyakazi, na ninge-endelea kumwambai mke wangu ni Almasi, kwa hio ni lazima ni mtake care na ni mtreat with love and respect ndo mana unaniona nakosha vyombo hapa.

Ningemalizia kwa kumyamazisha kabisa asinizoe tena, ningesema; Sikuja kwenu kuomba msada, na sina shida na msada wako....Na mara ya pili jifunze adabu, ukiona mtu na mke wake usiwaingilie katika maisha yao.
 
hivi ni kwamba hawa wanaume ha2takiwi kushirikiana nao kazi za nyumbani? huyo mwanamke angenikoma,kama ni makubaliano ye2 yeye kimemuhusu nn? kwann amsaidie? amekatika mikono au ndio hizo kazi za mwanamke? huyo mwanamke ana kiherehere.

Tuko ukurasa mmoja Da Mkubwa

By the way ninakutafuta kwa udi na uvumba, machozi yangu hayatokauka mpaka ni'kutane' nawe Da nyamayao.
bado nalia
 
Hahha Lizzy, ningeshangaa sana kwanza kama mkaka alikubali!! Ninavyohisia haya ni makubaliano ya yeye na mkewe so akikubali kusaidiwa na msaidizi wa nyumba ya pili ni wazi makubaliano yake na mkewe hayakuwa ya ukweli bali either ya kinafiki au kushurtishwa.

Mke wa jirani naye mh! Haiba ya kike imemwishia akha!!

Ila MwanajamiiOne ni watu wachache ambao huwa wanaenda kwenye extent ya kujiuliza hiyo (hapo kwa red). Wengi wetu tunakimbilia kumuona huyo mwanaume kama ni bhushoke bila kujua what's behind.

Tena uzoefu wangu unanionyesha kuna wanawake wa kutosha tu ambao wanapenda waume zao wawasaidie kazi kama hizo, lakini at the same time hawajisikii vizuri kuona kaka zao wanasaidia wake (wifi) zao. Straight away anakimbilia kusema 'kaka yangu ameishakuwa bhushoke'
 
my dearest MJ11....kosa ni langu jamani nilipitiwa kbsa kukueleza kwamba cku hizi c2mii tena ile no ya airtel, nina voda, nakutumia no tubonge mami 2jue mchakato.
 
hivi ni kwamba hawa wanaume ha2takiwi kushirikiana nao kazi za nyumbani? huyo mwanamke angenikoma,kama ni makubaliano ye2 yeye kimemuhusu nn? kwann amsaidie? amekatika mikono au ndio hizo kazi za mwanamke? huyo mwanamke ana kiherehere.

kweli kabisa ni vizuri kuwa mwangalifu ndoa huvunjwa na watu kama hawa wanao jidai wana huruma!
 
Alikua anatoa msaada tu najua kuna wanawake hawawezi kuona mwanaume akiwa jikoni au anafanya kazi za ndani, hua wanaamini hiyo ni kazi ya mwanamke
 
Mambo ya ndani ya nyumba ni mambo ya watu wawili. Mtu asiye ndani kuingilia mambo ya ndoa ya watu ili iweje? Kama mme anaona poa kuosha vyombo kuna tatizo gani?
 
Kwa sababu convention ya kutoka kwenye mila zetu kuingia huku tuliko bado ndo inaendelea kwa tanzania, bado kufanyika kwa kazi hizo by wanaume kunawapa shida watu wengine. Japo approach aliyotumia jirani siyo feasible ila kushangaa kwake si kosa. Binafsi nimelelewa kwenye mazingira ambayo si kitu cha ajabu mwanaume kuosha vyombo, mwenyewe huwa naosha na kupika sana2.
Na kama ni mimi huyo mwanaume siwezi kuruhusu vyombo nilivyotumia mimi na my wife akaoshe mwingine, yani no kwa kweli.
Kuna baadhi ya mambo ndani ya nyumba mke ndio kiongozi hivyo ni kweli huyo jirani angemuazima haus geli mkewe jamaa
 
Back
Top Bottom