FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,792
- 5,375
salaam,
ni kweli kuwa kigoma imekuwa nyuma muda mrefu sana toka taifa limepata uhuru. Mkoa mzima wa kigoma umekuwa hauna miundombinu ya uhakika tofauti na reli aliyojenga mjerumani. Mkoa umekuwa ukipokea wakimbizi kwa muda mrefu sana. Maji yamekuwa ni shida, barabara na umeme. Biashara haijachangamka sana licha ya kuwa na bandari. Hata hivyo haina maana kuwa tumekaa kimya bila kufanya lolote
ni kweli kuwa kigoma tupo nyuma sana. Lakini ikumbukwe kuwa hatujawahi kuomba chakula toka nchi ipate uhuru yaani kigoma haijawahi kuwa na njaa. Tunajilisha wenyewe na kuuza ziada nchi jirani.
- hivi sasa kuna miradi mikubwa miwili ya barabara (mwandiga - manyovu inayounganisha mji wa kigoma na mji wa bujumbura na kisha uvira (drc) na ile ya kigoma - kidahwe kama sehemu ya barabara ya kigoma - tabora. Miradi hii itaunganisha kigoma na nchi za kongo na burundi na hivyo kukuza biashara.
- eneo lote la kigoma ujiji pamoja na sehemu za kigoma vijijini hivi sasa ni special economic zone. Mwezi wa saba tra wametoa leseni maalumu ambapo sasa kigoma itakuwa ni destination port na hivyo kuongeza biashara na kutengeneza ajira.
- bandari ndogo ya kagunga inajengwa na soko ili kuongeza biashara katika mpaka wa kagunga na burundi.
- miradi ya maji mingi sasa imeanza kutekekelezwa katika maeneo ya vijijini. Eu water facility iligharamia mradi wa maji katika vijiji 5 na hivi sasa worldbank imetoa kazi inayofanywa na kampuni ya redeco gmbh ya ujerumani kwa miradi ya vijiji 10 katika wilaya ya kigoma. Nordic fund inagharamia mradi wa maji wa manispaa ya kigoma.
- mcc inajenga mrado wa umeme malagarasi ambao utakamilika mwaka 2012 na kuweza kumaliza tatizo la umeme katika mji wa kigoma na mji wa kasulu.
- tumejenga shule kata zote. Baadhi ya vijiji kama kalinzi, nyarubanda, mukigo, matizo vina shule mbili za sekondari.
Kwa vyovyote vile maendeleo ya kigoma ambayo imekuwa marginalized kwa miaka mingi (kumbukeni kigoma ilikuwa ni chanzo cha manamba) hayawezi kutokea kwa kulipuka tu. Inahitajika kazi kubwa sana na ya ziada. Tunajitahidi.
Ndio maana mkoa wa kigoma haujawahi kuipa ccm zaidi ya 60% katika kura za wabunge. Mwaka 2005 national avarage ilikuwa 69% na kwa kigoma ccm walipata 58% (10% below national avarage). Huu ni ujumbe tosha kuwa watu wa kigoma tumechoshwa na kuwa marginalized.
Tunajiamini kuwa tutavuka viunzi hivi. Tunajiamiin kuwa tutaweza kushindana ndani ya tanzania. Kwa kuwa tumeweza kujilisha miaka yote hii, tutaweza kushinda changamoto za maendeleo.
welldone bwana zitto tunataka kuona kigoma inabadilika ,kigoma iwe kigoma yenyewe kuna ziwa kule ambalo na lenyewe ni kitega uchumi kizuri tu raia wasikumbuke habari za manamba tena iwe historia ,raia waamini wale viongozi waliowapa kura zao hawakukosea
tumechoka kila siku kulia ooh nchi ooh kigoma ooh too much