Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,832
Nchi ya Ujerumani ina idadi ya watu milioni 82 huku watu hao wakimiliki jumla ya baiskeli milioni 81. Ujerumani inayo jumla ya magari milioni 48. Mtoto akifika miaka 11 anatakiwa kujifunza na kukata leseni ya baiskeli ili kuweza kuendesha baiskeli kwenye barabara za umma. Barabara husika nyingi zimetengwa sehemu ya waendesha baiskeli.
Jumla kulikuwa na ajali 85,000 za baiskeli nchini Ujerumani huku 372 kati yao wakipoteza maisha Cologne na Berlin zikiongoza kwa ajali! Wajerumani wameamua kujenga barabara za mwendokasi za baiskeli. Ulaya matumizi ya baiskeli ni maarufu huku Amsterdam ukiwa machampioni. Matumizi ya baiskeli yanaimarisha afya na kutochafua mazingira.
Tanzania kwa mijini wengi wanaoendesha baiskeli ni wale wasioweza kumudu gharama za nauli na kwa baadhi ya mikoa iliyokuwa na utamaduni wa kutumia baiskeli, utamaduni huo unakufa taratibu baada ya kutamalaki kwa ujio wa boda!
Taarifa kwa msaada wa DW