Ujambazi unaoibuka kwa kasi udhibitiwe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
Wiki hii yameripotiwa matukio kadhaa ya ujambazi ambapo watu wameuawa kwa nyakati tofauti na hivyo kuleta mtikisiko unaotishia amani ya nchi yetu. Kibaya zaidi, miongoni mwa matukio haya yanahusisha silaha nzito za kivita hali inayoogofya.

Lipo tukio la uvamizi wa vituo vya mafuta mjini Bukoba ambapo polisi walifanya kazi ya ziada kujibizana kwa risasi na majambazi na hatimaye watu watano waliuawa Januari 5, mwaka huu kitongoji cha Katoma, tarafa ya Kyamutwara. Watu hao hawakutambulika majina wala maeneo watokako.

Tukio lingine linahusisha majambazi wanne wenye silaha za kivita waliovamia uwanja wa ndege wa mgodi wa dhahabu wa Geita mkoani Mwanza wakiwa wameficha nyuso zao, aliishambulia ndege iliyobeba dhahabu kwa lengo la kupora madini hayo yaliyokuwa yakisafirishwa. Jambazi moja liliuawa kwa risasi.

Majambazi haya ambayo matatu yalipozidiwa yalitokomea msituni, inaelezwa yalikuwa na mabomu ya kutupa kwa mkono, bunduki aina ya SMG pamoja na bastola na yaliishambulia ndege hiyo yenye namba za usajili SH-TZX iliyokuwa ikipakia dhahabu kwenye gari maalum.

Jambazi aliyeuawa na ambaye anadaiwa kuwa kiongozi wa genge hilo alikuwa amevalia kininja na ushungi, miwani iliyokuwa mfukoni na anasadikiwa kuwa raia wa Burundi kutokana na nyaraka zilizokutwa mfukoni mwake na simu mbili. Tena alivalia suruali ya kijeshi.
Ujambazi mwingine umetokea huko Songea ambapo mtu mmoja aliuawa kwa risasi alipovamia kituo cha kusambazia umeme akiwa na

wenzake sita waliokimbia kwa lengo la kuiba mafuta katika kituo hicho cha Tanesco.
Matukio haya yaizindue serikali kwamba isijisahau kwani ingawa hali ya ujambazi nchini ilitulia kwa kitambo, vyombo vyetu vya usalama

visibweteke, viwe macho kwani wahalifu wana mbinu nyingi.
Lazima vijipange vema hasa maeneo ya mipakani ambapo ipo mianya mingi inayotumiwa na wahalifu kupenyeza na pia kuingiza silaha za kivita kama hizo zilizokamatwa katika tukio la mgodi wa Geita.

Tukiimarisha ukaguzi kwenye mipaka yetu kudhibiti wahamiaji haramu na ukaguzi makini kwenye viwanja vya ndege, vituo vyote vya mipakani kuhakikisha uhalali wa wanaoingia nchini, silaha haramu zinaweza kudhibitiwa kuingia nchini mwetu.
Lazima vyombo vya dola viwe makini kwani wapo pia watu wabaya wanaotumia vibaya sare za vyombo hivi kuvichafua pale zinaponaswa zikiwa zimevaliwa na wahalifu kama tukio la Geita.

Kazi hii isiachiwe askari wetu au wanajeshi wetu pekee bali hata ushiriki wa wananchi ni muhimu kwani wahalifu wengi hujichanganya na wananchi. Wananchi ni muhimu wakumbushwe mara kwa mara wajibu wao wa kutoa taarifa pale wanapomshuku mtu asiyeeleweka awe ni mgeni au mwenyeji.

Ndio kwanza mwaka mpya wa 2012 umeanza. Mwaka uliomalizika tuliumaliza salama. Matukio haya yawe changamoto kwa serikali yetu na vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuhakikisha majambazi katu hayatambi tena mwaka huu.
Jitihada kubwa zimeonekana mwaka uliomalizika na mwaka huu tunaamini vyombo vyetu vimejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa

majambazi yatakayothubutu, kabla ya kutekeleza uhalifu wao wanadhibitiwa.
Tunawapongeza polisi waliopambana katika matukio hayo na tunaamini kuwa kasi ya mapambano itaongezwa maradufu ili kuhakikisha

usalama wa raia, mali na amani ya nchi yetu kwa ujumla vinalindwa kwa gharama zote.
Kila mmoja wetu akitimiza wajibu wake, tunaamini mafanikio yatapatikana. Cha msingi na cha kuzingatia tuzingatie sheria, kanuni na wajibu katika kutekeleza yale tuliyojipangia kujiletea maendeleo na ulinzi wa nchi yetu.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

 
Kulikuwa na ile polisi jamii Mwema awali aliianzisha,,was good kupromote mahusiano ya polisi na wananchi na kuwawezesha kutoa taarifa voluntarily,lkn ukigeugeu wa hawa hawa polisi yanapokuja maswala mengine hasa siasa wanageuka ghafla na kukibeba chama tawala waziwazi na hivo kuamsha hasira za wananchi za miaka ileeeeeee ambapo mwananchi alikuwa akimwona polisi hamchukulii kama rafiki bali adui flani!! so safari bado ni ndefu!
 
na kama nikweli kwamba majambazi yanatoka nchi jirani basi inamaanisha mipaka yetu iko wazi na idara ya uhamiaji wamelala
 
Tunasingizia nchi jirani wakati mifumo yetu ya ulinzi ni mfu, BTW huyo jambazi anayehisiwa kuwa raia wa Burundi tayari amechukuliwa na ndugu zake wa maswa...........
 
Back
Top Bottom