Uhusiano wa upungufu wa damu na lishe kwa wanawake

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
13,834
20,247
Je, kuna mahusiano au uhusiano wowote kati ya tatizo la upungufu wa damu kwa wanawake walio kwenye umri wa kuzaa (miaka 15 mpaka 49), kwa wanawake wajawazito, tatizo la vifo vitokanavyo na uzazi, na tatizo la upungufu wa damu kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5?

Ni nadra sana kuona wataalamu wa afya wakigusia uhusiano huu, lakini kupitia makala hii tutaanza kupata uelewa kama uhusiano huu upo au haupo?

Takwimu za Serikali zinaonyesha kuwa vifo vya wanawake wakati wa kujifungua vinaongezeka nchini kutoka 453 kati ya 100,000 mwaka 2010 hadi vifo 543 kati ya 100,000 mwaka 2015. Malengo yetu kama nchi ni kufikia chini ya vifo 292 kati ya wanawake 100,000 wanaojifungua mwaka 2021, na hatimaye kufikia chini ya vifo 70 kati ya wanawake 100,000 wanaojifungua ifikapo mwaka 2030.

Inasemekana kuwa idadi hii ya vifo inaendana sanjari na tatizo la upungufu wa damu kwa wanawake na katika hili takwimu za “Tanzania Demographics Health Survey” TDHS 2015 zinaonyesha kuna uhusiano wa karibu sana kati ya tatizo la upungufu wa damu kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa miaka 15 hadi 49, kwa wanawake wajawazito. Kitakwimu, asilimia 44.8 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa wana upungufu wa damu huku asilimia 57.1 ya wajawazito wana upungufu wa damu.

Hapa ndipo inapokuja hatari ya vifo vya uzazi na watoto kuzaliwa na tatizo la upungufu wa damu. Takwimu za “Tanzania National Nutrition Survey” TNNS 2018, mikoa inayoongoza kwa tatizo la upungufu wa damu kwa wanawake walio kwenye umri wa kuzaa nchini kwa Kundi hili ni:

Shinyanga asilimia 59.4, Mwanza asilimia 55.4, Kigoma asilimia 54.2, Simiyu asilimia 53.7 na Dar es Salaam yenye asilimia 53.1

Takwimu za “Tanzania National Nutrition Survey” TNNS 2018 zinatuonyesha pia mikoa inayoongoza kwa tatizo la upungufu wa damu kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5: Shinyanga asilimia 70.9, Geita asilimia 68.1,Kigoma asilimia 67.2,Morogoro asilimia 65.7 na Mwanza asilimia 62.6.

Hii inatuonyesha nini? Mwanamke aliye kwenye umri wa kuzaa anapokuwa na tatizo la upungufu wa damu anakuwa hatarini zaidi ama kupoteza maisha yeye na anapojifungua, au kujifungua mtoto mwenye upungufu wa damu, mwenye kilo ndogo sana au njiti na changamoto nyingine mbalimbali. Naamini hadi sasa tupo pamoja katika kuelewa kwamba upo uhusiano wa karibu kati ya tatizo la upungufu wa damu kwa wanawake walio kwenye umri wa kuzaa na kwa wajawazito. Pia vifo kwa uzazi, upungufu wa damu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Lakini je, ni kwa nini wanawake wanapata tatizo hili?

Kwa ufupi, tatizo la upungufu wa damu kwa mwanamke linaanza anapoanza kupata hedhi anakuwa na hatari kubwa zaidi ya kupata utapiamlo wa upungufu wa damu kutokana na upungufu wa madini joto “iron” mwilini. Hii husababishwa na damu nyingi ambayo hupotea kipindi yupo katika hedhi. Vile vile, mwanamke akiwa mjamzito mwili wake huhitaji damu nyingi zaidi. Lishe duni huchangia hali kwa kiasi kikubwa. Ili kuongeza damu mwilini na kuhakisha hupati tatizo la utapiamlo wa upungufu wa damu ni lazima ule vyakula venye madini joto “iron” nyingi kama: maharage,dengu, njegere,choroko, korosho, viazi vya kuokwa/chomwa,

mboga za majani kama spinach na mchicha, vyakula vilivyowekewa virutubisho “Whoe-Grain”, Samaki aina ya prawns, maini ya ng’ombe, mbegu za maboga na broccolli.
 
Tatizo hili la upungufu wa damu kwa wanawake linatibika na mwanamke kupona kabisa?

Kama ni ndio, kwa njia zipi au utaratibu upi?
 
Na pia Kuna huusiano wowote au athari zozote kwa mwanamke mwenye tatizo hili na ufanyaji wa tendo la ndoa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom