Uhusiano wa mtoto kunyonya kidole na uwezo wake kiakili

Mwanzo wakunyonya kidole unanjia mbili, moja mtoto mdogo sana kuanzia siku moja huwa ni njaa na mbili Mtoto mkubwa kidogo kama miaka miwili yawezakuwa kuiga. Baadae inakuwa mazoea ya hiyo tabia. Ikishakuwa mazoea basi hunyonya hata akiwa kashiba au usingizini.


.....Mwanangu alikuwa hanyonyi kidole before daycare , baada ya kuanza nursery school tu,
hapo akiwa na 2 yrs. Akaanza kunyonya kidole, nikagundua kaiga kwa mtoto ambaye yupo pembeni mwa kiti chake.

Nikamwambia mwalimu awatenganishe wakae far apart from each other. Na nikawa mkali, kila anaponyonya kidole
I used to pinch him. Baada ya mwezi tu akaacha, na sasa yupo 3 yrs sijaona kamwe akinyonya kidole.
 
Wa kwangu alinyonya siku ya kwanza ya kuzaliwa coz maziwa yalikuwa hayatoki ,tena alikuwa akiingiza kidole gumba mpaka kinampalia but maziwa yalipoanza kutoka akaacha na kasahau now hata ukimpa hataki tena...ana week nne now..
 
Lol,mnanitisha mie mkubwa na kidole nanyonya nmejaribu kuacha nimeshindwa,samtimez n aibu laki najisahau nifanyaje ili niache?
 
mhh hiyo relation ya uwezo wa kiakili na kunyonya kidole inahitaji research ya ukweli nadhani. Mie nimenyonya kidole tangu nikiwa sijijui mpaka sekondari hivi na nikiwa niko makini sana hata leo kama sina kitu natafuna kucha. Mama alitumia mbinu zote akaamua aniache hivyo hivyo. Pia kuna mdogo wangu ana miaka tisa sasa bado ananyonya na mama hamsumbui kwa uzoefu wa mimi kuacha nikiwa mkubwa. Kiakili niko vizuri, primary mpaka o'level nilikuwa nakuwa mtu wa kwanza darasani. Huyo mdogo wangu pia wembe ni ule ule.
 
Lol,mnanitisha mie mkubwa na kidole nanyonya nmejaribu kuacha nimeshindwa,samtimez n aibu laki najisahau nifanyaje ili niache?

kichanje kwa wembe we c mkubwa! Na usipofanya hivyo hakuna njia nyingine ya kuacha! Me nliacha kwa njia hiyo nkiwa m2 mzima kabsa!
 
Ndugu zangu,
mara nyingi angalia stage ambayo mtoto anaanza kunyonya kidole.
mf mtoto anaanza kunyonya akiwa anamiezi mitatu, ni pale ambapo mama yake anaanza kwenda kazini/shughuli uwezo wa kunyonya mara kwa mara haupo.. Yapasa apate chakula kwa wakati bila kupoteza muda.
na yule wa miezi tisa the same kwani anakuwa anaingia ktk stage ya kula vyakula je anashiba?
uhusiano wa mtoto kiakili nimejifunza ni kuwa mtoto anahamishia concetration kwenye kidole hivyo uwezekano wa kuwa mzito ni mkubwa, si kweli kwamba hana akili.
Mimi agenda yangu mtoto ale ashibe mara zote akiwa 0-5. Mpe chakula/snacks/ asikae tumbo wazi.
Mtoto wangu wa kwanza kanyonya vidole ila ameacha, kweli mdomo unaharibika, mwingine ananyonya ulimi, na kadri anvyokuwa na njaa ndio frequency inazidi.

kazana ataacha.
 
Wala usiwe na wasiwasi kuhusu akili kucharge,..mtoto wangu wa kiume alikuwa ananyonya kidole mpaka darasa la kwanza (miaka 6) na akili zinachaj kweli,anakuwa wa kwanza tu darasani( la pili sasa) ..sema madhara yake anaweza akawa anaugua sana minyoo, afu kidole kinakonda kinyama, aliweza kuacha automatically lakin kwa kumkataza sana na ikiwemo mbakora!.....lakini kwa ushauri huyo mdogo mwache akifika kama umri wa miaka miwili mweke pilipili afu akinyonya mwambie chafu hiyo ataacha tu....




Ni kweli usemacho lakini watoto wengine hawakanyiki mboko mtt hasikii pilipili yote analamba afu anakwambia mpake tena
 
Nina watoto 2 wakiume wamefuatana kuzaliwa.Mkubwa ana miaka 8 yupo darasa la 3 na alianza kunyonya kidole gumba tangu akiwa kichanga na bado anaendelea japo amepunguza kwa sasa.Darasani tangu alipokuwa chekechea hadi sasa anacheza na nafasi ya1-2.Kwa sasa ananyonya awapo usingizini. Mdogo ana umri wa miaka 3 ndo ameanza masomo ya awali.Akili yake ni kali sana na huyu ananyonya sana kidole kuliko ilivyokuwa kwa yule mkubwa. So uhusiano wa akili kuwa kidogo na kunyonya kidole kwa uzoefu wa wanangu hauna uhusiano wowote.Pia kuna suala la mtoto kutafuna kucha na uwezo mkubwa wa akili darasani na hili anaendelea nalo mtu hadi kufikia umri wa utu uzima. Utakuta mtu kucha zikikua badala ya kuzipunguza kwa wembe ama nail cutter yeye anakata kwa meno zinakuwa fupi wakati mwingine hadi damu inatoka na hili linaingia hadi kwenye tabia za kurithi yaani mzazi baadaye anakuja kuzaa watoto ambao nao wataendelea na tabia hiyo ya kutafuna kucha.Jambo moja nililoliona kwa watu hao ni kwamba darasani wengi ni moto wa kuotea mbali. Wataalamu watuelimishe kuhusu hilo.
 
haina tabu hiyo, kunyonya kidole ni kitu cha kawaida kabisa, wazungu mpaka wametengeza kidude chao kama kanyonyo flani hivi (jina lake limentoka kidogo) ambacho anapewa mtoto mnyonya kidole kuepuka hayo madhara madogo madogo ya kunyonya kidole asilia
 
Watoto ambao hua hawanyonyi vidole ni vilizii hakina kupumua ni analiaa tu lakini akiwa ananyonyaa hua wapolee kweli na wengi wakikua huachaa kunyonyaa
 
Sidhani kama kuna uhusiano,sababu mimi niko chuo sasa lakini nanyonya sana kidole hasa nikiwa namawazo na pia kucha nakula sana mpaka damu hunitoka lakini niko vizuri sana
 
Jamani hizo ni coincidence tu uwezo wa akili na kunyonya kidole Havina muingiliano. Hiyo ni dalili yakuwa huyo mtoto hashibi mnyonyesheni ashibe kabla hajakizoea kidole. Mama ale protein za kutosha maziwa yatoke mazito ashibe motto. Akitaka kunyonya kidole apewe nyonyo haraka NJAA imtoke. Kumuachisha mtoto kunyonya kidole zip simple approach na mtoto anaacha kupitia kwa daktari wa kinywa na meno sio medical dr wala hivyo mnavyowapaka watoto vidoleni.

We need scientific analysis not blah blah, let me do simple research then i'll come back with scientifically analysed thread, no reseach no right to comment
 
Kuhusu akili no way!!!! Sema anakuwa na mazingatio kidogo sana sababu hiko kidole kinatawala fikra sana!!!!!

Wangu kanyonya sana ila alipoanza michezo binafsi,magari,mpira na vinginevyo alipunguza sana he is two now anaongea sana na yuko poa sana kwenye ufahamu,memory,inquisitiveness ambazo ji dalili tosha kuwa sio mzigo!!!!!! So kila ukiwa naye ni maswali tu so muda wa kunyonya kidole umepungua sana isipokuwa akiwa analala tu!!!!!

Akiwa na fahamu zake msimuache iddle muda mrefu as anakuwa mpweke so anajifariji na kidole. Keep the baby occupied ataacha!!!!

Hata akiwa ananyonya kidole ukimpeleka kwenye interest zake utaona anasahau kabisa kunyonya kidole so kwa mimi naona akili ni suala la "genes" zaid kuliko learned traits!!!!!!!

Mtoto asilaumiwe kwa urithi alopata kwa wazazi please!!!!!
 
Mtoto wa dadangu anamiaka 6 na nusu yupo darasa la pili wakiume ana akili sana yani ni so bright na kachangamka sana, nae anatatizo la kunyonya kidole cha mkono wa kulia na kushika watu makwapa kwa kidole cha mkono wa kushoto na kunusa kidole alichoshika kwapa la mtu yani hadi anaboa tumetumia njia zote imeshindikana, ila akiwa shuleni,kanisani na sehemu yenye watu wengi anaogopa kunyonya.
hili tatizo la kushika watu makwapa ndo linakasirisha sana mwenye ushauri wowote wa kuitokomeza hii tabia?
 
Lol,mnanitisha mie mkubwa na kidole nanyonya nmejaribu kuacha nimeshindwa,samtimez n aibu laki najisahau nifanyaje ili niache?

Mmmmh yaani hata ukipewa milioni 500 uzihesabu na ukimaliza within 6hrs zinakuwa zako unaweza simamisha hili zoezi ili unyonye kidole????!!!!!!!!

Au umepewa writen interview ya kazi nzuri na.maswali yooote kwako maji unaweza acha andika/andika kwa uzembe sababu ya kidole?????!!!!!

Mind iddleness au relatively low concentration occupation ndio inakupa hiyo "loop" ya kunyonya kidole!!!!!!!
 
Back
Top Bottom