Uhuru wa kuabudu unahitajika kuwekewa mkazo, tupinge ubaguzi na udini

Waziri wa madini

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
379
465
Habari Wana JF Leo naandika huku machozi yananilengalenga.

Mimi ni mfanyakazi katika moja ya taasisi iliyo chini ya Serikali, kitu kilichonisukuma kuandika uzi huu ni kutaka kuamsha fikra za umoja na usawa katika imani zetu sehemu zetu za kazi kuna haja ya makusudi kuwepo usawa na hali ya kuvumiliana katika masuala ya kiimani ukizingatia Taifa letu ni moja na sisi ni wamoja na serikali haina dini Ila inaheshimu na kutambua dini zote.

Kuna matukio ambayo yamekuwa na muendelezo mbaya katika baadhi ya maofisi na mashirika mbalimbali binafsi ntajitolea mfano wangu.

Ikitokea nikawa nataka kufanya ibada kwa mujibu wa taratibu za dini yangu kwakuwa mimi ni muumini ninayefanya ibada mara tano kwa siku imekuwa changamoto kubwa kwanza naonekana kama mdini japo sijawahi kuhubiri kuhusu dini ,

Yani Ile kuhakikisha nafanya tu ibada hainipiti naonekana mdini na watu wanajadili, lakini hali tofauti kwa wenzangu wa Imani tofauti wao mtu akiwa mfanyaji ibada na mtu wa Imani thabiti anaoneka ni mtu sahihi na mchamungu hasa tena mtu mwema mwenye upendo, hautosikia mijadala kumuhusu wala kumuhoji.

Kuna siku tulikuwa tupo katika semina, basi kama ada ikabidi tufungue kwa maombi kiukweli nilishtushwa sana na matokeo yaliyotokea siku hyo.

Kwanza tulitakiwa tusimame,tufumbe macho na kufata kanuni na taratibu za kuitikia maombi ya dini nyingine hata kama taratibu zile na maombi yale yana ukakasi kwa upande wa Imani yangu, pili maombi ya upande mmoja tu yalitosha kufungua na kufunga Ile semina pasi na kuhusisha maombi au duah za imani nyingine hali ya kuwa inatambulika tupo katika mchanganyiko wa Imani.

Kuna mdada mmoja alikuwa ni bosi katika kitengo fulani ,watu walimuundia zengwe kwa kigezo cha udini kisa tu alikuwa yupo katika Imani tofauti na Imani ya mastafu wengi wa hapamean kulitengenezwa kama umoja Fulani wa kiibada sasa yeye pekee ndio alikuwa na Iman tofauti na wenzake wengi, waka waambia madereva waseme dada yule huwa anachagua madereva wa Imani yake tu pindi anapotaka kwenda safari,Basi dada wa watu akapigwa chini japo alikuwa mtendaji mzuri.

Lengo na kusudio la mada hii ni kwamba tuheshimu na kuthamini Imani za wenzetu Hakika ubaguzi ni dhambi mbaya Sana na yenye madhara makubwa .

Taifa letu limejengwa kwa misingi ya umoja ,upendo na kuvumiliana .

Tusiwekeze katika udini na ukabila haya Mambo yatatukwamisha katika kufikia mafanikio Kama Taifa.

Tusiweke chuki ya udini na ubaguzi au baadhi kujiona wao ndio wapo sahihi na wenzao wamepotea sababu niliwahi kumsikia mtu hapa kazini akisema yani nataman hata watu wa imani fulani wasiwepo hapa kazini sababu kila mtu wa Imani Ile ni mshirikina na anamajini. Haya Mambo yanaleta chuki na kuondosha upendo.

Kama ikiwa viongozi wetu wa dini ni wamoja wanakaa pamoja na kuwa wamoja na hata dini zetu zimetufunza umoja kwa nn tunabaguana sisi sote ni watoto wa mama mmoja WaArika na WaTanzania tupendane tuheshimiane ,tuilinde tunu yetu ya amani.
 
Achani upumbavu na utumwa wa kifikira dini zoote zimeletwa na watu weupe..dini ya kweli ni ile ya asili ya mababu zetu hizi nyingine zimekuja na maji(bahari)
 
Napenda sana kila mtu aabudu bila kumkwaza mwenzie!

Mtu anayeabudu mambo yake mwenyewe mimi huwa nafurahi tu.

Tatizo linakuja pale anapotaka kunihusisha na mimi kwenye imani yake,

Tena kwa vitisho eti la sivyo Mungu atanichoma moto siku ya mwisho.

hapo ndipo dhana yote ya mungu huwa naitilia mashaka.
 
Achani upumbavu na utumwa wa kifikira dini zoote zimeletwa na watu weupe..dini ya kweli ni ile ya asili ya mababu zetu hizi nyingine zimekuja na maji(bahari)
Ushaanza ubaguzi na Wewe .Jambo baya nikulazimisha kila mtu aamini unachoaminj haifai acha Mara moja.Heshimu vumilia
 
Napenda sana kila mtu aabudu bila kumkwaza mwenzie!
Mtu anayeabudu mambo yake mwenyewe mimi huwa nafurahi tu.

Tatizo linakuja pale anapotaka kunihusisha na mimi kwenye imani yake,
Tena kwa vitisho eti la sivyo Mungu atanichoma moto siku ya mwisho.
hapo ndipo dhana yote ya mungu huwa naitilia mashaka.
Kama ni katika mafundisho yake na anahubiria watu wake it's ok au Kama anatumia busara na hekima kukushawishi ufate Iman yake pia sawa Ila kitu kibaya ni kudharau na kukejeli Imani nyingine hapo ndipo tubapofeli.
 
na kusudio la mada hii ni kwamba tuheshimu na kuthamini Imani za wenzetu Hakika ubaguzi ni dhambi mbaya Sana na yenye madhara makubwa .
Taifa letu limejengwa kwa misingi ya umoja ,upendo na kuvumiliana .
Tusiwekeze katika udini na ukabila haya Mambo yatatukwamisha katika kufikia mafanikio Kama Taifa
Very good conclusion, nadhani yatupasa kwenda mbali zaidi, sote tunapaswa kuitana Ndugu kama walivyoitana waasisi wa taifa letu, hivi sasa kuna watu wanajiita waheshimiwa, ukiwaangalia wametoka katika jamii tulizopo sisi, wanavuta hewa ileile na sisi, wanakula vyakula vilevile na sisi hata kunywa maji yaleyale na sisi, wanazikwa kwenye makaburi yaleyale na sisi, kipi kinawafanya wao kujiona ni bora zaidi?
 
Maneno makubwa Sana umeongea ndugu
 
Kama ni katika mafundisho yake na anahubiria watu wake it's ok au Kama anatumia busara na hekima kukushawishi ufate Iman yake pia sawa Ila kitu kibaya ni kudharau na kukejeli Imani nyingine hapo ndipo tubapofeli.
Hao walioleta hizo dini nao waliwabagua mababu zetu
 
Hao walioleta hizo dini nao waliwabagua mababu zetu
Hiko ni kitu ambacho huna ushahidi nacho mkuu,

Mimi nadhanj tujikite katika kukemea na kukomesha ubaguzi pasi na kuendeleza ubaguzi wa dini Kama hizi zakwetu zile zimeletwa kila mtu aamini anachoamini alimradi Imani yake haikiuki utu wa mtu mwingine na Sheria zanchi yetu.
 
Habari Wana JF Leo naandika huku machozi yananilengalenga.

Mimi ni mfanyakazi katika moja ya taasisi iliyo chini ya Serikali, kitu kilichonisukuma kuandika uzi huu ni kutaka kuamsha fikra za umoja na usawa katika imani zetu sehemu zetu za kazi kuna haja ya makusudi kuwepo usawa na hali ya kuvumiliana katika masuala ya kiimani ukizingatia Taifa letu ni moja na sisi ni wamoja na serikali haina dini Ila inaheshimu na kutambua dini zote.
Sio sawa kabisa.
Hizi kelel ziende mpaka kwa Zumaridi pia
 
Achani upumbavu na utumwa wa kifikira dini zoote zimeletwa na watu weupe..dini ya kweli ni ile ya asili ya mababu zetu hizi nyingine zimekuja na maji(bahari)
Hizo za asili zilishindwa vipi kutusaidia tusichukuliwe utumwani.

Kama zilishindwa kupambana na hizi za kuletewa uoni ya kwamba zilikuwa ni dhaifu.
 
Back
Top Bottom