Uhuru wa dhamiri ni zawadi iliyo njema tuliyopewa na baba mbinguni, tuutetee kwa nguvu zote

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,693
UHURU WA DHAMIRI

Ni zawadi iliyo njema tuliyopewa na BABA WA MBINGUNI.

Jambo hili wengi wanaweza kutolitilia maanani hasa nchi baadhi za Afrika, Mashariki ya Kati na Asia, maana nchi hizo zinapitia mgandamizo wa uhuru wa dhamiri kiasi kwamba wakazi wake wanaishi kwa hofu.

Hofu inaondoa kujiamini na inaleta utumwa, maana mtumwa ndio ana hofu kwa bwana wake. Watoto wengi wamepoteza kujiamini kwasababu ya malezi ya utisho; upendo huleta afya. Aliye lelewa kwa hofu na aliye lelewa kwa upendo wako tofauti kabisa.

Mahali penye utisho sana wa sheria ya kulazimishwa kwa adhabu, watu hawana amani, maana shinikizo ukimbiza amani na kuzalisha hofu.

"Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.[1 Yohana 4:18]."

Mungu hatumii nguvu kushikiza watu wamtii au kumpenda, bali anataka tumpende kwa hiyari, katupa freedom of choice. Na nchi zote zenye freedom of choice zina maendeleo kuliko nchi za kidikteta. Nchi yeyote yenye kutumia nguvu kushinikiza mambo yake, ata kama imepiga hatua ya kimaendeleo, basi itegemee mapinduzi au maandamano au anguko kabisa.

Gadafi aliwapa kila kitu Walibya, lakini akasahau kuwapa uhuru, walimpindua. Chinai imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo lakini haina maendeleo ya uhuru wa dhamiri, tunashuhudia sasa Wachina wa HongKong wakigomea serikali ya China Bara kwa maandamano makubwa yenye uharibifu, maana serikali ya China Bara inataka kuwaondolea uhuru wao wa mda mrefu walioupata kwa Waingereza. Hawahitaji kabisa kutawaliwa na sheria za China Bara bali za Muingereza. Ukionja uhuru, ni ngumu kurudi katika utumwa.

Unaweza kuona kwanini USA ina maendeleo sana? Wana siri gani ya urembo, mbona kama ni waovu vile kuliko sisi? Wengi tunajilinganisha na wa Marekani kwa habari ya uovu na kuwaona wao ni waovu kuliko sisi. Huenda, lakini inawezekana sisi ndio waovu sana kuliko wao. Bora kufanya dhambi kwa uhuru kuliko kufanya dhambi kwa kujificha, maana unajinyima lakini motoni utaenda.

Ndio maana Mungu anahitaji tuwe wakweli na wa wazi. Kujaa katika nyumba za ibada si kipimo cha utakatifu, wenzetu hawajai katika nyumba za ibada ila ndio wanatoa misaada tele kwa wahitaji, sisi tumejaa uchoyo, uchungu, na masengenyo.

Uhuru wa kisiasa

Uhuru wa kiuchumi/Soko huria

Uhuru wa Kidini

Hivyo vitu vitatu hapo juu, dio msingi wa maendeleo ya kitaifa. Ulaya walipitia mgandamizo wa uhuru wa kisiasa sababu ya wafalme, walipitia mgandamizo wa uhuru wa kiuchumi kwasababu familia za kifalme na maofisa ndio walitawala biashara na mali, walipitia mgandamizo wa uhuru wa kidini kwasababu Papa wa Rumi alipewa fursa ya kutawala Ukristo wote Ulaya.

Wote waliotofautiana na wakuu hao waliuawa au kuteswa ama kufungwa na wengine kupotezwa na mali zao kutaifishwa. Damu yao haikumwagika bure. Lakini watu [vizazi vyao] walichoka mateso ya kunyimwa uhuru wa dini, siasa na uchumi, walipindua wafalme, waliua maofisa waliojipa ukuu wa uchumi, zaidi ya yote walikataa UPAPA na hatimaye walimpindua mnamo mwaka 1798, na kumnyang'anya kabisa mji wa Roma mnamo mwaka 1780.

Ndipo Ulaya ikawa HURU, hawakutaka tena kurudia kuwa chini ya madhabahu ya Roma na Ufalme. Leo wanaishi kwa demokrasia, ingawa kuna fununu za waovu fulani ambao wanataka kurudisha utawala wa zamani, yaani utawala wa madhabahu na ufalme, hilo tutaliona wakati mwingine.

Kitu ambacho kilichanganya dunia ya wapinga uhuru wa dhamiri zama hizo ni ukuaji wa taifa la Marekani bila kuwa na mfalme wala PAPA. kwao kilikuwa ni kitu kisichowezekana kabisa, wafalme wa Ulaya na Papa walisikika wakitoa laana na kutangaza anguko la Marekani kwa mfumo wake huo wa utawala katika uhuru. Na mambo yaliyo washangaza ni kama ifuatavyo:-

Yafuatayo ni maneno ya kikatiba ambayo ndio sababu ya taifa la Marekani kuitwa taifa la uzuri katika unabii wa Biblia.

 Liberty and Justice for all. Uhuru na haki kwa wote

 Congress shall not make no Law respecting the establishment of religion, or prohibiting the free exercise thereof. Bunge halitatunga sheria yeyote ikipendelea uanzishwaji wa dini au kuzuia uhuru wa kuwepo kwake.

 But no religion test shall ever be required as qualification to any office or public trust under the united state. Hakuna daima kigezo cha kidini kitakacho hitajika kuwa sifa ya kushika ofisi yoyote ya utumishi wa umma chini ya serikali ya Marekani.

 We hold these truths to be self-evident, that all men are created equal that they are endowed by the creator with certain in alienable rights, that among this are life, liberty, and the persuit of happiness. Tunashika kweli hizi ziwe mashahidi binafsi, kwamba watu wote wameumbwa kwa usawa, kwamba walipewa na muumba wao haki maalumu za kudumu, kwamba kati ya hizi ni maisha, uhuru, na kutafuta furaha.

TAMKO LA LAANA KWA KATIBA YA MAREKANI.

Papa Pius 1X, katika waraka wake wa mwaka 1864 anadai serikali haina mamlaka ya kuwapa watu wake uhuru wa kuchagua dini yeyote wanayoiona ni ya kweli. Ni kanisa pekee ndilo lina haki ya kiserikali kutangaza kuwa dini ya Kikatholiki ndio dini ya kiserikali, kwa kuwaweka/kuwakatilia mbali kando wengine wote. Na walaaniwe wale wote wanaotangaza uhuru wa dhamira na wa kuabudu kwa kudai kuwa kanisa halina mamlaka ya kutumia nguvu. The syllabus of Pope Pius IX, December 1864

BIBLIA INASEMA HIVI

"Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?[1 Wakorintho 10:29]."

Katiba ya Marekani inafuata Biblia, anguko lao litakuja pale tu watakapo iasi katiba yao hiyo. Ni katibu nzuri sana yalikulijenga taifa, mataifa mengi duniani yamejaa udini, udikteta, ukabila, hofu na ukavu ndio matokeo yake.

Wewe kiongozi wa dini ama wewe mwanasiasa, msijenge chuki na watu wanao wakosoa, ama msijenge uchungu na wale mnaopishana nao kimtazamo. Maana kuna viongozi wa dini wanatawala waumini, hawataki waumini wawe uhuru ili wasije wakagundua hila zao, vivyo hivyo kwa wanasiasa.

Ukiona hivyo kwamba mnatishwa kuhoji dini zenu au lolote lile, hilo ni jibu kuwa kuna ukengeufu, pia ni pando la machafuko kwa baadae. Maana mtu wa kweli haaogopi kuhojiwa wala kuwafunga mdomo wanaomkosoa, hana la kuogopa maana anatenda haki; mwovu ndio anapenda kufanya mambo yake gizani. Yesu anasema:-

"Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.[Yohana 3:21]."

TETEA UHURU WA DHAMIRI.
 
Back
Top Bottom