Uhuru Kenya ni Bilionea lkn bado anaiba tu, kwa nini?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,790
Huyu jamaa Raisi wa Kenya, amezaliwa kwenye Utajiri, amekulia kwenye Utajiri na wala hajui Umaskini ni nini, amekuwa Raisi wa Kenya lkn bado tu anawaibia masikini wa Kenya, kwa nini?

Uhuru Kenya alipaswa awe anatoa fedha kwa ajili ya charity sasa na siyo kuendelea kuibia Wakenya!
Wakenya kama mnajipenda, ondoeni huyu jamaa Ikulu, atawafilisi!

Uhuru kin in Sh5bn health scandal: Raila
 
Wewe unaelewa maana ya neno "kin" au ni uzushi na upotoshaji tu. Ina maana kila mtu kwenye ukoo wa rais Uhuru akihusika na wizi basi itakua ni rais ndiye ameiba? Mbona huko Bongo mwanaye rais Magufuli mlimsema sana kwenye mitandao kwamba kaiba mtihani ili akubaliwe kwenye chuo kikuu na rais hakuhusishwa binafsi. Japo mliipiga kimya juu kwa juu baadaye na hata kufuta jina la huyo mtoto kwenye mitandao.

Obama ndugu zake wanatajwa kwa mambo tofauti, wengine hata wakimponda na kuhusika na kampeni za Trump. Ukiwa rais haimaanishi kila mtu kwenye ukoo wako amekua rais pia. Wao ni watu wenye maisha yao binafsi na changamoto zao za kila siku na mishe zao.

Cha msingi ni rais asiwalinde hao wanaotajwa hata kama ndugu zake. Uchunguzi umeanza kufanywa, tunachoomba na kutegemea ni kwamba yeyote yule aliyehusika ataadhibiwa bila kujali ana undugu na rais wala nini, na akiwalinda basi ategemee tutampiga chini tu kwenye uchaguzi.
 
0991885955ebde54b712086bd5523c06.jpg
c02c74d6ba91f7e42bd0dd85bf146ade.jpg

[HASHTAG]#system[/HASHTAG] ya majambazi
 
Wizi upo kwenye damu yao na imekuwa tabia. Kuiba wanaona ni jambo la kawaida.
 
Back
Top Bottom