Uhuni wa NEC - Nini Kifanyike Wanavyuo waweze kupiga kura October 25?

RockSpider

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
6,861
2,754
Nimepokea kwa masikitiko Makubwa kuwa tume imekataa Wanafunzi kupiga kura za Urais popote walipo ... Nini kifanyike ili waweze kupiga kura coming October 25?
 
Kwa nini Nec isiweke vituo kwa kila chuo ili wanafunzi wapige kura?
 
wanafunzi wa kitanzania ni wababaishaji na hawajijui hivyo wasilalamike maana kuna taratibu za kuhama kituo,sasa alaumiwe tume?
 
Haki ya kuchagua ama kuchaguliwa ipo kisheria ... Methodology haiwezi kuwa sababu za kunyima Mwanafunzi kuchagua eti kwa kuwa Uandikishaji Ulifanyika wakati Vyuo havijafungwa na Upigaji Kura Utafanyika wakati vyuo vimefungwa !! CCM wajinga sana ... wanafikiri kwa kufanya hivyo watapunguza ari ya mabadiliko nchini .... Wito wangu Wanafunzi wajipange wapatiwe Usafiri wa Kuwawezesha kufika maeneo yao ya kupiga kura ...
 
siwahurumiii kwa ujinga wao, siku hizi wana hata matawi ya ccm vyuoni acha wanyimwe haki yao ya msingi itawasaidia kuamsha fikra mbadala miongoni mwa wanachuo
 
Wanafunz wa vyuo vikuu hawatakua na uwezo wa kupiga kura kwakua wakat wa uandikishwaj vyuo vyote vilikua waz hivyo wanafunz wote walijiandikishia vyuoni mwao lakin wakat wa kupiga kura vyuo vyote vitakua vimefungwa na wanafunz wote wapo makwao na tume imesema kua mtu atapiga kura sehem aliyojiandikishia sasa hawa wanafunz watapigaje kura?

Na huu ni mchezo wa serekal wa kila wakat wa uchaguz kwakua wanajua wanachuo weng wapo upinzan kwaiyo wanafanya hivyo ili kupunguza nguvu za wapinzan.

Na tume yenyewe imeundwa na serekal iliyopo madarakan ndio maana madai yao hayashughulikiw kwa wakat sasa tutafanyaje ili waweze kupiga kura? Mchango wenu wadau ni wa maana sana
 
Hapo ni kubadili mfumo mzma wa serkali ndio solution kubwa kwa wanavyuo wa baadae.....lakini nimesikia kuna form za kujaza ili kusaidia wale waliopo mbali na sehemu walipo andksha.....mmmmh huuuu mfumo mi nkajua utakua mo advanced....
 
Hakuna hata mmoja atakayekosa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura! Kauli hiyo ya Tume iliwezesha watanzania wote popote walipo kujitokeza kwa wingi wakajiandikisha, the same applied kwa kanuni hiyo hiyo hakuna hata mmoja atakayeshindwa kupiga kura eti kwa sababu yeye ni mwanachuo! hilo siliamini na wala halitatokea Tanzania!
 
Kuna tetesi kuwa NACTE imevitaka vyuo vyote kifunga kwa ajili ya wanafunzi kwenda kupiga kura walipojiandikisha.
 
Nimepokea kwa masikitiko Makubwa kuwa tume imekataa Wanafunzi kupiga kura za Urais popote walipo ... Nini kifanyike ili waweze kupiga kura coming October 25?
Cha msingi viongozi wa UKAWA wajipange tu...
Either waongee na tume kuishauri tume iwaruhusu wanachuo wapigie kura za urais popote walipo. Tume ikikataa basi itafutwe orodha ya wanachuo waliojiandikisha, kisha uongozi wa ukawa uitishe harambee ya kuchangia Safari za wanachuo wote kwenda kupiga kura bila kujali itikadi ya vyama vyao kwa sababu kupiga kura ni haki ya kila mtanzania. Mwaka huu ni mpango wa Mungu kuikomboa Tanzania kutoka kwa mkoloni so huwezi zuia kiu ya mabadiliko waliyonayo wananchi. Naomba viongozi wa ukawa wafanyie kazi suala hili kwa nguvu zote.. tuko nyuma yenu viongozi wetu wapenda mabadiliko....
 
Haki ya kuchagua ama kuchaguliwa ipo kisheria ... Methodology haiwezi kuwa sababu za kunyima Mwanafunzi kuchagua eti kwa kuwa Uandikishaji Ulifanyika wakati Vyuo havijafungwa na Upigaji Kura Utafanyika wakati Kura zinapigwa !! CCM wajinga sana ... wanafikiri kwa kufanya hivyo watapunguza ari ya mabadiliko nchini .... Wito wangu Wanafunzi wajipange wapatiwe Usafiri wa Kuwawezesha kufika maeneo yao ya kupiga kura ...

Wapenda mabadiliko tujipange tuchangie usafiri kwa hawa vijana wakatekeleze hakin yao ya msingi. Mimi ninawafadhili wanafunzi wawili toka Arusha kwenda Mwanza. Je wewe?
 
Nimepokea kwa masikitiko Makubwa kuwa tume imekataa Wanafunzi kupiga kura za Urais popote walipo ... Nini kifanyike ili waweze kupiga kura coming October 25?

Jamani tufike mahali tutofautishe kazi za taasisi hizo. kazi ya NEC ni kuandikisha wapiga kura na kusimamia zoezi la kupiga kura mahali ambapo walijiandikisha. siyo kazi ya NEC kufungua au kufunga vyuo. wanafunzi walaamu vyuo kufungwa mpaka baada ya uchaguzi.
 
Tujipange wanamabadiliko ili hawa vijana wachuo wafike kwenye maeneo ya kupigia kura. Itakuwa jambo la maana.
 
Sheria ya uchaguzi Inakataa Wagombea ama vyama kusafirisha wapiga kura .... CCM wanajua wanachokifanya ... Muhimu hapa ni Wananchi tuamue kwa dhaati kuwasafirisha wanavyuo kwa fedha zetu wenyewe ...
Cha msingi viongozi wa UKAWA wajipange tu...
Either waongee na tume kuishauri tume iwaruhusu wanachuo wapigie kura za urais popote walipo. Tume ikikataa basi itafutwe orodha ya wanachuo waliojiandikisha, kisha uongozi wa ukawa uitishe harambee ya kuchangia Safari za wanachuo wote kwenda kupiga kura bila kujali itikadi ya vyama vyao kwa sababu kupiga kura ni haki ya kila mtanzania. Mwaka huu ni mpango wa Mungu kuikomboa Tanzania kutoka kwa mkoloni so huwezi zuia kiu ya mabadiliko waliyonayo wananchi. Naomba viongozi wa ukawa wafanyie kazi suala hili kwa nguvu zote.. tuko nyuma yenu viongozi wetu wapenda mabadiliko....
 
mi ntatoa accommodation kwa vijana watano wa kiume geto kwangu dar kiitonyama,,,,jumamosi mkesha kama alivyosepa putin wetu wa chadema pale azimio la kawe....
 
Back
Top Bottom