Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Kama kuna neno linarudiwa rudiwa katika sakata linaloendelea sasa hivi ndani ya CDM ni kile kinachoitwa "uhafidhina" na wale wanaoita "Wahafidhina".
Sijui kama ndugu zetu wanaotumia neno hili wanalitumia wakijua maana yake hasa au wanalipa maana isiyokuwa yake hasa.
Uhafidhina kwani una matatizo gani gani? Na unalinganishwa na nini kwa upande mwingine maana katika siasa za kimataifa unapozungumzia "uhafidhina" unalinganisha na uliberali; je wale wanaopinga uhafidhina wao ni waliberali? Au wao ni watu huru (independents) au ni waliberali-mamboleo (neo-liberalists); au wao ni wataka mabadiliko (progressives)? Au wale wenye msimamo mkali (fundamentalists) ndio wanachukuliwa kama wahafidhina?