Uhaba wa sarafu vituo vya mwendokasi utaftiwe ufumbuzi

Ozone_

Member
Dec 30, 2023
88
107
Heri ya mwaka mpya watumiaji wote wa jf .
Katika siku za hivi karibuni baada ya kutangazwa kuongezeka kwa nauli za usafiri wa umma (hususani daladala) nimejikuta nikiwa mdau wa usafiri huu maarufu wa mwendokasi katika safari zangu za hapa mjini.

Sijajua ni ugeni wangu au ni nini maana nina mda mrefu sijautumia ila karibia kila siku nikiwa katika ukataji wa tiketi nakutana na kauli za wahudumu "chenji hamna" hapo sasa ni hiari yako uanze kutafta hiyo chenji, au usubiri abilia mwingine mwenye sarafu au mwisho ukiwa na haraka hiyo chenji yako uiache.

Hali hii nimeishuhudia hasa katika vituo vya kuanzia ubungo maji hadi magomeni. Ila sijawahi kumbana na hali hii kule kariakoo.

Ninachowaza je hawa wahudumu hujikusanyia kiasi gani kutokana na hela zinazobaki maana wasafiri ni wengi. Je waendeshaji wa mradi huu hii changamoto wameichujulia vipi?

Conclusively, naona ni bora kurejeshwa kwa matumizi ya kadi ili kuepusha kero ndogo ndogo na kupotezeana muda.

Naomba kuwasilisha.
#NI MTAZAMO TU!!!
 
Back
Top Bottom