Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,018
- 1,508
Salaam!
Wakuu nipo nyumbani wilayani Pangani mkoani Tanga namalizia msiba wa kaka yangu wadamu aliefariki katika hospitali ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu ikishirikiana na hospitali ya TMJ ya Mikocheni zote za Dar es Salaam.
Tatizo hasa lilikuwa Tumbo kujaa maji, kushindwa kula,kutapika na kwikwi isiyokoma, na kwabahati sana licha ya kufanyiwa kila aina ya vipimo ugonjwa anaougua haukuweza kugundulika,katika kipindi cha takriban miezi minne alichougua alianza kwa kulazwa katika hospital ya taifa Muhimbili Kisha wakamuhamishia TMJ.
Ili afanyiwe vipimo ambavyo Muhimbili hawana pamoja na kutolewa maji tumboni ambayo hujaa tena, kulikuwa na utaratibu wa kumtoa maji tumboni, kila siku ya alhamisi alitolewa maji drip mbili au tatu, alionekana kama kupata nafuu na tukatolewa tukamuuguze nyumbani.
Lakini maendeleo yake yalikuwa ya kusuasua mara apate nafuu mara azidiwe na hali ilipokuwa mbaya zaidi tulimrejesha tena TMJ ambapo alilazwa tena kwa uchunguzi zaidi na kwa mara nyingine tena hawakuweza kugundua tatizo hivyo wakatuhamishia tena Muhimbili, ikumbukwe kipindi chote hicho tiba yakutolewa maji tumboni ilikuwa ikiendelea, baadae alishindwa kabisa kula na kunywa mpaka umauti ulipomkuta, Mungu amlaze mahala pema peponi kaka yangu.
Wakuu kitu kilichonisukuma leo hii kuwahabarisha nikwamba nimepokea taarifa nyingine rafiki yangu wa utotoni nae amefariki kwa tatizo sawa na Hilo la kaka yangu na mwendendo wa kuugua kwake unashabihiana kabisa, ingawaje sisi tunaishi Dar es Salaam yeye alikuwa anaishi Moshi. Wasiwasi wangu ni kwamba kama huu ugonjwa sio mpya basi hauna tiba.
Shukrani za dhati ziwafikie Madaktari na wauguzi wote wa Muhimbili na TMJ kwa ushirikiano na msaada waliotupa.