Ugonjwa wa Ini

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Ini ni kiungo muhimu sana katika mwili wa binadamu. Ndicho kiungo kikubwa kilichopo ndani ya mwili. Ugonjwa wa cirrhosis ni ugonjwa wa 12 duniani kati ya magonjwa yanayosababisha vifo vitokanavyo na maradhi.

Cirrhosis husababishwa na unywaji pombe kupindukia, ugonjwa wa hepatitis B, C, na ugonjwa wa fatty liver disease. Kwa wagonjwa wengine chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijulikani. Kabla ya kuangalia ugonjwa wa cirhosis (tamka sirosis kwa kiswahili), kwanza tuangalie kazi ya ini kwenye mwili wa binadamu.

Ini linahusika na;
Kushughulikia chakula kilichosagwa kutoka kwenye utumbo mdogo (small intestine)
Hulinda mwili dhidhi ya magonjwa
Kutengeneza nyongo (bile)
Hudhibiti kiwango cha mafuta, sukari na chembechembe zijulikanazo kama amino acids kwenye damu
Huhifadhi vitamini, madini ya chuma na kemikali nyengine muhimu
Huvunjavunja chakula na kutengeneza energy inayohitajika mwilini
Ini hutengeneza chembechembe zinazozuia damu kuganda mwilini kama fibrinogen, prothrombin, factor V, VII, IX, X na X, protini C na S, antithrombin na nk.
Huharibu sumu na madawa ambayo yameingia mwilini.
Hutengeneza homoni aina ya angiotensinogen ambayo inahusika kupandisha presha ya damu mwilini wakati inapokutana na enzyme ya renin, enzyme hii ya renin hutolewa na figo wakati figo inapohisi presha imeshuka mwilini.
Husafisha damu kutokana na chembechembe mbaya na bakteria.
Hutengeneza enzyme na protini ambazo zinahitajika mwilini kwenye shughuli nyingi na hata kurekebisha tishu zilizoharibika.

Ugonjwa wa cirrhosis ni nini?
Cirrhosis ni matokeo ya ugonjwa sugu wa ini ambao hubadilisha tishu za kawaida za ini kwa njia ya fibrosis, scar tishu, matezi (regenerative nodules), kuziba damu kuingia kwenye ini na hivyo kufanya ini kushindwa kufanya kazi yake vizuri.

Visababishi vya ugonjwa huu
Cirhosis husababishwa na mjumuiko wa magonjwa mengi ambayo ni;

1. Ugonjwa wa ini unaosababishwa na unywaji wa pombe kupindukia kwa muda mrefu ( alcoholic liver disease) . Inakadiriwa asilimia 10 20 ya wanywaji pombe kupindukia kwa miaka 10 au zaidi ndio wanaopata ugonjwa huu. Yule anayekunywa pombe kwa muda mrefu huwa na asilimia kubwa ya kupata ugonjwa huu kutokana na kiwango cha pombe kuongezeka au kuwa kingi kwenye mwili wake. Pombe huharibu ini na kusababisha lishindwe kufanya kazi yake dhidhi ya mafuta, protini, na wanga (carbohydrates).
Na si lazima uwe mnywaji pombe ili upate ugonjwa huu.

Wanywaji pombe kupindukia pia wanaweza kupata tatizo la utapia mlo (malnutrition) kutokana na pombe kukosa virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini, kupungua kwa hamu ya kula, na kupungua kwa ufyonzwaji wa virutubisho vya chakula kwenye utumbo. Utapia mlo pia husababisha ugonjwa wa ini.

Unywaji wa pombe kupindukia huweza kusababisha ugonjwa aina ya alcoholic hepatitis ambao huambatana na homa, manjano kwenye mboni au ndani ya macho na kwenye ngozi, kuongeza ukubwa wa ini (hepatomegaly) na kudhoofika kwa mgonjwa

Dalili na viashiria vya ugonjwa wa cirrhosis

Wagonjwa wengi wa cirrhosis hawaonyeshi dalili zozote kwenye hatua za awali za ugonjwa huu. Dalili zinatokana na;

1. Kushindwa kufanya kazi kwa ini kadri ugonjwa unavyoongezeka
2. Kuharibika kwa umbile na ukubwa wa ini kutokana na kitu tunachoita kitaalamu kama scarring
Uchovu
Ulegevu
Kichefuchefu
Kupungua hamu ya kula hatimaye kupungua uzito
Kupungua hamu ya kufanya mapenzi

Hata hivyo, dalili na viashiria vingi vinaweza visitokee hadi mtu atakapopata madhara ya cirrhosis. Dalili na viashiria hivyo ambavyo hutokea baada ya madhara kutokea ni kama zifuatavyo;

Kuwa rangi ya manjano kwenye macho na ngozi kutokana na ukusanywaji wa bilirubin kwa wingi kwenye viungo hivi.
Kutapika
Homa
Kuharisha
Maumivu ya tumbo kutokana kuongezeka ukubwa wa ini au kutokana na vijiwe kwenye gall bladder (gallstones)
Kuwashwa mwili kutokana na bile salts iliyopo kwenye ngozi
Tumbo kuwa kubwa au kuvimbiwa kutokana na maji kujikusanya sehemu ya tumbo (ascites)
Kuongezeka uzito kwa sababu ya ukusanywaji wa maji mwilini
Kutoka damu kwenye fizi au pua, husababishwa na kutokuwepo na chembechembe zinazozuia damu kuganda
Kuvimba kwa miguu
Kupumua kwa shida
Kupungua nyama mwilini (Loss of muscle mass)
Kwa wanawake, kuwa na hedhi isiyokuwa ya kawaida kutokana kupungua kwa utolewaji wa homoni zinazosaidia wakati wa hedhi.

Damu kwenye matapishi au haja kubwa kutokana kuharibika mfumo wa kuzuia damu kuganda.
Spider angiomata Kutokea kwa mabaka yanayofanana na utandu wa buibui ambao katikati yake kuna rangi nyekundu. Hii inatokana na mishipa ya damu inayoonekana kwa sababu ya kuongezeka kiwango cha estradiol.

Kuongezeka mikunjo ya kwenye viganja vya mikono (palmar erythema) husababishwa na kupungua kwa homoni za mapenzi (sex hormone)
Kuongezeka kwa matiti kwa wanaume (gynecomastia) kutokana na kuzidi kwa kiwango cha homoni aina ya estradiol mwilini, hutokea kwa asilimia 66 ya wagonjwa wa cirrhosis.

Kupungua kwa korodani kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi vizuri kwa hypothalamus na pitituary gland. Hii husababisha uume kushindwa kusimama (kusimika), kushindwa kutia mimba mwanamke (infertility), na kupungua hamu ya kufanya mapenzi.

Mabadiliko ya kucha Kucha zinaweza kuwa na mistari (Muehrckes lines), au kuwa za rangi nyeupe pembezoni mwake na rangi nyekundu kwa mbele (terrys nails) au kujikunja kwa kucha pembeni (finger clubbing).

Bandama kuongezeka ukubwa (splenomegaly)
Kuongezeka unene na kufupika kwa ngozi ya viganja vya mikono na hivyo kusababisha vidole na viganja kuwa kwenye umbile la kujikunja (dupuytrens contracture)
Ini linaweza kuongezeka ukubwa, kupungua au kuwa la kawaida.
Kuonekana kwa mishipa ya damu sehemu ya tumbo (caput medusa)
Mgonjwa kuwa na harufu kali kama ya maiti kwenye pumzi kutokana na kuongezeka kwa dimethyl sulfide
Cruveilhier Bumgarten murmur Sauti fulani ambayo daktari anaweza kuisikia wakati akimpima mgonjwa kutumia stethoscope maeneo ya tumboni.

Mapigo ya moyo kwenda haraka mtu anapojaribu kusimama
Kusikia kiu sana
Mdomo kuwa mkavu au kukauka mate
Asterixis

AMEN..............!!
 
Ugonjwa wa ini
Ini ni kiungo muhimu sana katika mwili wa binadamu. Ndicho kiungo kikubwa kilichopo ndani ya mwili. Ugonjwa wa cirrhosis ni ugonjwa wa 12 duniani kati ya magonjwa yanayosababisha vifo vitokanavyo na maradhi.
Cirrhosis husababishwa na unywaji pombe kupindukia, ugonjwa wa hepatitis B, C, na ugonjwa wa fatty liver disease. Kwa wagonjwa wengine chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijulikani. Kabla ya kuangalia ugonjwa wa cirhosis (tamka sirosis kwa kiswahili), kwanza tuangalie kazi ya ini kwenye mwili wa binadamu.

Ini linahusika na;
• Kushughulikia chakula kilichosagwa kutoka kwenye utumbo mdogo (small intestine)
• Hulinda mwili dhidhi ya magonjwa
• Kutengeneza nyongo (bile)
• Hudhibiti kiwango cha mafuta, sukari na chembechembe zijulikanazo kama amino acids kwenye damu
• Huhifadhi vitamini, madini ya chuma na kemikali nyengine muhimu
• Huvunjavunja chakula na kutengeneza energy inayohitajika mwilini
• Ini hutengeneza chembechembe zinazozuia damu kuganda mwilini kama fibrinogen, prothrombin, factor V, VII, IX, X na X, protini C na S, antithrombin na nk.
• Huharibu sumu na madawa ambayo yameingia mwilini.
• Hutengeneza homoni aina ya angiotensinogen ambayo inahusika kupandisha presha ya damu mwilini wakati inapokutana na enzyme ya renin, enzyme hii ya renin hutolewa na figo wakati figo inapohisi presha imeshuka mwilini.
• Husafisha damu kutokana na chembechembe mbaya na bakteria.
• Hutengeneza enzyme na protini ambazo zinahitajika mwilini kwenye shughuli nyingi na hata kurekebisha tishu zilizoharibika.

Ugonjwa wa cirrhosis ni nini?
Cirrhosis ni matokeo ya ugonjwa sugu wa ini ambao hubadilisha tishu za kawaida za ini kwa njia ya fibrosis, scar tishu, matezi (regenerative nodules), kuziba damu kuingia kwenye ini na hivyo kufanya ini kushindwa kufanya kazi yake vizuri.

Visababishi vya ugonjwa huu
Cirhosis husababishwa na mjumuiko wa magonjwa mengi ambayo ni;

1. Ugonjwa wa ini unaosababishwa na unywaji wa pombe kupindukia kwa muda mrefu ( alcoholic liver disease) . Inakadiriwa asilimia 10 – 20 ya wanywaji pombe kupindukia kwa miaka 10 au zaidi ndio wanaopata ugonjwa huu. Yule anayekunywa pombe kwa muda mrefu huwa na asilimia kubwa ya kupata ugonjwa huu kutokana na kiwango cha pombe kuongezeka au kuwa kingi kwenye mwili wake. Pombe huharibu ini na kusababisha lishindwe kufanya kazi yake dhidhi ya mafuta, protini, na wanga (carbohydrates).
Na si lazima uwe mnywaji pombe ili upate ugonjwa huu.

Wanywaji pombe kupindukia pia wanaweza kupata tatizo la utapia mlo (malnutrition) kutokana na pombe kukosa virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini, kupungua kwa hamu ya kula, na kupungua kwa ufyonzwaji wa virutubisho vya chakula kwenye utumbo. Utapia mlo pia husababisha ugonjwa wa ini.

Unywaji wa pombe kupindukia huweza kusababisha ugonjwa aina ya alcoholic hepatitis ambao huambatana na homa, manjano kwenye mboni au ndani ya macho na kwenye ngozi, kuongeza ukubwa wa ini (hepatomegaly) na kudhoofika kwa mgonjwa

Dalili na viashiria vya ugonjwa wa cirrhosis

Wagonjwa wengi wa cirrhosis hawaonyeshi dalili zozote kwenye hatua za awali za ugonjwa huu. Dalili zinatokana na;

1. Kushindwa kufanya kazi kwa ini kadri ugonjwa unavyoongezeka
2. Kuharibika kwa umbile na ukubwa wa ini kutokana na kitu tunachoita kitaalamu kama scarring
• Uchovu
• Ulegevu
• Kichefuchefu
• Kupungua hamu ya kula hatimaye kupungua uzito
• Kupungua hamu ya kufanya mapenzi

Hata hivyo, dalili na viashiria vingi vinaweza visitokee hadi mtu atakapopata madhara ya cirrhosis. Dalili na viashiria hivyo ambavyo hutokea baada ya madhara kutokea ni kama zifuatavyo;

• Kuwa rangi ya manjano kwenye macho na ngozi kutokana na ukusanywaji wa bilirubin kwa wingi kwenye viungo hivi.
• Kutapika
• Homa
• Kuharisha
• Maumivu ya tumbo kutokana kuongezeka ukubwa wa ini au kutokana na vijiwe kwenye gall bladder (gallstones)
• Kuwashwa mwili kutokana na bile salts iliyopo kwenye ngozi
• Tumbo kuwa kubwa au kuvimbiwa kutokana na maji kujikusanya sehemu ya tumbo (ascites)
• Kuongezeka uzito kwa sababu ya ukusanywaji wa maji mwilini
• Kutoka damu kwenye fizi au pua, husababishwa na kutokuwepo na chembechembe zinazozuia damu kuganda
• Kuvimba kwa miguu
• Kupumua kwa shida
• Kupungua nyama mwilini (Loss of muscle mass)
• Kwa wanawake, kuwa na hedhi isiyokuwa ya kawaida kutokana kupungua kwa utolewaji wa homoni zinazosaidia wakati wa hedhi.
• Damu kwenye matapishi au haja kubwa kutokana kuharibika mfumo wa kuzuia damu kuganda.
• Spider angiomata – Kutokea kwa mabaka yanayofanana na utandu wa buibui ambao katikati yake kuna rangi nyekundu. Hii inatokana na mishipa ya damu inayoonekana kwa sababu ya kuongezeka kiwango cha estradiol.
• Kuongezeka mikunjo ya kwenye viganja vya mikono (palmar erythema) husababishwa na kupungua kwa homoni za mapenzi (sex hormone)
• Kuongezeka kwa matiti kwa wanaume (gynecomastia) kutokana na kuzidi kwa kiwango cha homoni aina ya estradiol mwilini, hutokea kwa asilimia 66 ya wagonjwa wa cirrhosis.
• Kupungua kwa korodani kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi vizuri kwa hypothalamus na pitituary gland. Hii husababisha uume kushindwa kusimama (kusimika), kushindwa kutia mimba mwanamke (infertility), na kupungua hamu ya kufanya mapenzi.
• Mabadiliko ya kucha – Kucha zinaweza kuwa na mistari (Muehrcke’s lines), au kuwa za rangi nyeupe pembezoni mwake na rangi nyekundu kwa mbele (terry’s nails) au kujikunja kwa kucha pembeni (finger clubbing).
• Bandama kuongezeka ukubwa (splenomegaly)
• Kuongezeka unene na kufupika kwa ngozi ya viganja vya mikono na hivyo kusababisha vidole na viganja kuwa kwenye umbile la kujikunja (dupuytren’s contracture)
• Ini linaweza kuongezeka ukubwa, kupungua au kuwa la kawaida.
• Kuonekana kwa mishipa ya damu sehemu ya tumbo (caput medusa)
• Mgonjwa kuwa na harufu kali kama ya maiti kwenye pumzi kutokana na kuongezeka kwa dimethyl sulfide
• Cruveilhier Bumgarten murmur – Sauti fulani ambayo daktari anaweza kuisikia wakati akimpima mgonjwa kutumia stethoscope maeneo ya tumboni.
• Mapigo ya moyo kwenda haraka mtu anapojaribu kusimama
• Kusikia kiu sana
• Mdomo kuwa mkavu au kukauka mate
• Asterixis

AMEN..............!!
Mkuu Asante kwa darasa murua, je! Ugonjwa wa ini unatibika?
 
Mungu ndo kanileta kwenye hii page nina tatizo moja ambalo nimejaribu kuwaeleza madaktari na hakuna aliewahi kunielewa , nikila kdg nahisi kuvimbiwa, harufu mdomon kama panya alie oza, miguu kuvimba bila sababu au nikikaa sana , acidi nyingi mwilini maana nasikia mwilini kama kuna vitu vinaniunguza, viungo vinawaka moto , mwili unawasha mno hasa kwenye baridi afu nasikia vitu vichungu mdomoni ambavyo nikivitapika huwa napata nafuu kubwa mno ni kama tindikali flani ila nikitapika nakaa baafa ya wikimbili vinaanza tena nikitapika napata nafuu nateseka mnooooo sasa nimesoma hapa nikaoma ni bile saltiliyo kwenye ngozi.

Du sijui nifanyeje naombeni ushauri nimekata tamaa ya maisha nahuea nataman nife kwa mateso nayopata. Msaada tafadhari
 
Mungu ndo kanileta kwenye hii page nina tatizo moja ambalo nimejaribu kuwaeleza madaktari na hakuna aliewahi kunielewa , nikila kdg nahisi kuvimbiwa, harufu mdomon kama panya alie oza, miguu kuvimba bila sababu au nikikaa sana , acidi nyingi mwilini maana nasikia mwilini kama kuna vitu vinaniunguza, viungo vinawaka moto , mwili unawasha mno hasa kwenye baridi afu nasikia vitu vichungu mdomoni ambavyo nikivitapika huwa napata nafuu kubwa mno ni kama tindikali flani ila nikitapika nakaa baafa ya wikimbili vinaanza tena nikitapika napata nafuu nateseka mnooooo sasa nimesoma hapa nikaoma ni bile saltiliyo kwenye ngozi. Du sijui nifanyeje naombeni ushauri nimekata tamaa ya maisha nahuea nataman nife kwa mateso nayopata. Msaada tafadhari


Nenda hospital au muone Daktari, jaribu kwenda kwa madaktari tofauti tofauti,maana hata Dk.wametofautiana utaalam na uzoefu..
 
Back
Top Bottom