Patriote
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 1,718
- 1,047
Suala la ugawaji wa vitalu vya uwindaji wa kitalii limekuwa likiisumbua serikali kwa miaka mingi sana na kufanya viongozi wetu mara kadhaa kutoana povu pale suala hili linapojadiliwa. Sio kwamba ugawaji wa vitalu kwa wawekezaji unatumia technolojia ya hali ya juu sana, la hasha, ukiingia kwenye undani wa suala hili utagundua kuwa kinachowafanya viongozi wetu kutoana povu ni kutaka wao/familia zao/jamaa zao wapate mgao wa vitalu hivi. Hili hasa ndilo tatizo la msingi ktk suala zima la ugawaji wa Vitalu. Ipo orodha ndefu ya vigogo, ndugu, jamaa na marafiki wa vigogo wa nchi hii waliomilikishwa maeneo ya mahoteli na au vitalu vya uwindaji wa kitalii ktk hifadhi zetu.
Kichefuchefu kilichopo katika upendeleo huu ni kwamba vigogo/ndugu/jamaa hao wanapopewa hayo maeneo kwa upendeleo wengi wao wanakuwa hawafwati sheria zilizopo kwa vile wanajua kuna anayewalinda na kuwakingia kifua, watu hawa hawana uwezo wa fedha wala utaalam, uzoefu, wala nyenzo za kufanya shughuli za utalii hivyo huishia kuuza/kukodisha maeneo hayo kwa wawekezaji wa kigeni kinyume na sheria/utaratibu. Hili ndilo hasa chimbuko lingine la ugomvi kati ya wawekezaji wa kigeni na serikali.
Serikali inatumia mgongo wa kujifanya inataka wazawa wamilikishwe Vitalu vya uwindaji wa kitalii kumbe kimsingi inalenga kuwanyang'anya wawekezaji wa kigeni waliokuwa wanamiliki maeneo hayo toka awali ili kuwapa "wazawa" ambao kimsingi ni vigogo wenyewe/watoto wao/ndugu, jamaa na marafiki zao tena wasio na sifa za kuendesha biashara hiyo. Hali hii inapelekea Serikali kupoteza mapato mengi sana. Kama kweli Serikali inapenda wazawa wamiliki rasilimali zao, Mbona Reginald Mengi hakupewa Kilimanjaro Hotel instead akapewa Muarabu wa Suti???Kama serikali inapenda wazawa, kwa nini wachimba madini wadogowadogo wanatimuliwa maeneo ya migodini???
Ugomvi huu sasa umevuka mipaka na kuingia kwenye anga za kimataifa ambapo Shirikisho la Kimataifa la Wawindaji ('Safari Club International-SCI) limeamua kuanika hadharani mvutano uliopo kati ya serikali na baadhi ya kampuni za uwindaji za kigeni huku likionya watalii wanaoingia nchini.Shirikisho hilo la Convention' ambalo huandaa maonyesho ya kimataifa ya kampuni za uwindaji kila mwaka, kupitia jarida lake la 'Hunting Report' toleo la Oktoba na Novemba mwaka huu, linaeleza kuwa kutokana na kuwepo mgogoro wa ugawaji vitalu nchini hivi sasa mazingira ya uwindaji sio mazuri. Tamko hilo au tahadhari hii inaweza ikapelekea kupungua kwa pato la Taifa linalotokana na Uwindaji wa kitalii.
HITIMISHO: Ndugu zangu suala la ugawaji vitalu na maeneo ya ujenzi wa mahoteli ndani ya hifadhi zetu kwa ujumla wake limegubikwa na utata unaosababishwa na ufisadi, uchu/ulafi wa viongozi wetu pamoja na upendeleo kwa ndugu, jamaa na marafiki zao. Ndugu zangu tusidanganywe kuwa Serikali inapenda sana wananchi wake na ndio maana imeamua kutoa vitalu hivyo wa wazawa, wazawa wanaoongelewa hapa kwa asilimia kubwa ni walewale wanaotuibia rasilimali zetu. Je katika hali hiii nini kifanyike?? Mana PCCB ndo hivyo kazi yake kubwa ni kusafisha na kutetea ufisadi!!!!???
Nashauri ili serikali ipate pato la kutosha na iondokane na lawama zisizokuwa na msingi, vitalu vigawiwe kwa mnada wa wazi kuliko huu utaratibu wa kugawa vitalu kwa kwa kujifungia na kwa kujuana. kwa kufanya hivi lawama, kujuana na ufisadi vitakuwa havina nafasi.