Ufunguo wa furaha katika ndoa ni kumpenda mume kuliko watoto?

Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
May 23, 2010
1,471
722
"Ukimpenda mume ukamfanya afurahi basi mwisho wa siku familia yote itakuwa na furaha".Kasema bwana mmoja wakati alipoulizwa kwanini ndoa nyingi zinagubikwa na misukosuko!

"Mke anatakiwa kuweka "ndoa' iwe kipaumbele cha kwanza kuliko kila kitu na hata watoto".
Je inaleta maana?
 
To me it doesn't. . .
Wote (mume na ndoa yake pamoja na watoto) wanastahili kupewa kipaumbele. Au mtu aokoe ndoa huku akijidistance na watoto. . . sioni raha yake.
 
mume mke watoto wana make familia lazima wote mpendane
hayo mambo ya mke kuconcentrate na mume tu ni nidhamu ya woga lazima wote mpendane ili kuwa na familia bora na yenye furaha
 
Ni kizungumkuti. NI kweli wanaume wengi wanapenda kuwa second to none. Neno upendo ni gumu kulitafsiri. Mara nyingi utakuta kinachoongelewa ni attention. Sasa mama akiwa na watoto wadogo atakuwa ana pay more attention kwa watoto. Baba atakasirika na kuona mapenzi yamepungua. Ila inabidi watoto wakikua kidogo mama arekebishe hali kwani ni kweli inaweza kufanya ndoa ku shake.

Kwangu mimi watoto wakishafika miaka miwili naanza kuzidisha attention kwa baba yao. Kwa kifupi wanandoa wanahitaji faragha na si kuwa na watoto kila mahali, kwa mfano kuna wanaolala na watoto si kwa kuwa hakuna spare room; kwa kuwa mama hataki ku part na watoto wake.
 
only in africa,ambapo mume anafuliwa anapikiwa hadi anabrashiwa viatu!!!!!.....
sioni nyumba nzima ikiwa na furaha,ambapo mmoja ni kijakazi na mwingine ni mfalme.....!..huu ni unafiki!na ukiweka housegal akupunguzie kazi....mumeo anaishia kutembea naye...kisa 'ukaribu'...mnh......ukiweka unafiki pembeni ndoa nyingi za kiafrica hazina furaha(well,mwanamke hana furaha).....mara nyingi anastrugle kubalance mambo nyumbani yanayomtaka awe robot,na pia cloud ya mashaka/suspcion...alyways inahang ya infidelity ya mumewe......

am drunk...
 
To me it doesn't. . .
Wote (mume na ndoa yake pamoja na watoto) wanastahili kupewa kipaumbele. Au mtu aokoe ndoa huku akijidistance na watoto. . . sioni raha yake.

he! dogo ushaolewa tayari?
 
Huo ni mfumo dume na mapenzi ya hofu kwa wanawake na kukosa kujiamini.

Na wapo wanawake wa hivyo nimeshuhudia, una kuta anamtake care mume tu watoto hata hawakumbuki.

Unakuta chakula cha baba anapika peke yake special,
nguo za baba anazinyosha ana panga vizuri kabatini,watoto sasa nguo zinarundikwa kwenye boksi haijulikani chafu wala safi.

Matokeo mtoto akiwa mtu mzima na yeye anachukua time zake hana time na mama wala baba,mbaya sana.
 
Emilia sio tu chakula cha baba anapika mama, hata akipika dada baba atapikiwa wali nyama wakati watoto wanakula ugali maharage. Au unakuta asubuhi baba anapata chai nzito ya maziwa na mayai pembeni wakati watoto wanakula kiporo na chai ya rangi.

Na mie nimeshudia, sijui hawa wamama hua wanafikiria nini.
 
wewe mtoto noumer unamfundisha mama wa hiari?

Haya bwana, nimeamini elimu haina mwisho.

Jamani!!!
Haya basi siku nyingine ukiuliza swali ama ukitaka kitu hata kama najua kilipo ntashushhhhh tu.
 
Mnakosea sasa! Vitabu vya dini, samahani kwa nitakaemkwaza, vinasema 'mwanaume ampende mkewe' tena kwa 'akili'. Mwanamke anapaswa kutii tu yale yanayofaa kutii. Watoto wanapaswa kulindwa na kufundishwa na wazazi wote. Sasa wanawake siku hizi tunajipa jukumu la 'kupenda' tena hadi kutunza familia. Ndo maana vilio havituishi. Mi nimeamua nitulie tuliii nipendwe tu
NB: msiniwakie sana, nnakuwaga na moyo,lol
 
Emilia sio tu chakula cha baba anapika mama, hata akipika dada baba atapikiwa wali nyama wakati watoto wanakula ugali maharage. Au unakuta asubuhi baba anapata chai nzito ya maziwa na mayai pembeni wakati watoto wanakula kiporo na chai ya rangi.

Na mie nimeshudia, sijui hawa wamama hua wanafikiria nini.

Huu mbona ni upuuzi wa mwaka 47!
Kwanza mtu mzima haitaji kula kiviiile maana keshakua..anachohitaji ni ukarabati wa afya na kujiweka hai tu.
Watoto ndio wanahitaji kula zaidi tena vyakula kama maziwa, nyama etc.
Kumlea baba kama mtoto ni uzembe.
Halafu jamani, kwani upendo ni chakula?
 
Mnakosea sasa! Vitabu vya dini, samahani kwa nitakaemkwaza, vinasema 'mwanaume ampende mkewe' tena kwa 'akili'. Mwanamke anapaswa kutii tu yale yanayofaa kutii. Watoto wanapaswa kulindwa na kufundishwa na wazazi wote. Sasa wanawake siku hizi tunajipa jukumu la 'kupenda' tena hadi kutunza familia. Ndo maana vilio havituishi. Mi nimeamua nitulie tuliii nipendwe tu
NB: msiniwakie sana, nnakuwaga na moyo,lol

Hebu tupe hiyo formula yako ya kukaa tuliii upendwe.Inakuwaje mwenzetu?

Huu mbona ni upuuzi wa mwaka 47!
Kwanza mtu mzima haitaji kula kiviiile maana keshakua..anachohitaji ni ukarabati wa afya na kujiweka hai tu.
Watoto ndio wanahitaji kula zaidi tena vyakula kama maziwa, nyama etc.
Kumlea baba kama mtoto ni uzembe.
Halafu jamani, kwani upendo ni chakula?

Tausi sio kwamba upendo ni chakula hapana, ni kwamba baba anapata the best of everything.
Kwanzia muda wa mama mpaka mlo wake, watoto wanapata kwashakoo na kukosa ukaribu wa mama huko kwenye background.
 
Back
Top Bottom