Ni pm kwa ushauri
Mkubwa naweza pata number yako ya simu na ww uko wapi maana mimi nataka kufuga kwa wingi1.Nguruwe anachukua miezi 6 mpaka 12 mpaka kufikia uzito wa kutosha (inategemeanan na malisho)
2.Inategemeana na nafasi yako, ukiwa upo pale full time, wapagazi watatu ni more than enough (kumbuka usipokuwapo watu wanakuwa na uzembe flan). mimi nnao sita chini ya usimamizi mkali.
3.inategemea uko wapi. huku kwetu hata kama haulimi gunia la pumba za mahindi ni Tsh 10,000/=! mashudu ya alizeti gunia ni 20,000/=!
4. Ekari moja wanakaa kwa amani yote. ni vizuri kuwa mbali na makazi ya watu.
5. inategemea uko wapi. kwangu mm nauwezo wa kuuza nguruwe 200 kwa mwezi bila shida. watoto inasumbua kidogo kwa sababu wananunua wafugaji, ukitaka kuwauza kwa urahisi wakuze mpaka miezi mitatu hv.
6. Minyoo na ukurutu. Kikubwa ni chanjo na usafi wa hali ya juu KILA SIKU (nguruwe ni msafi sana akitunzwa, wa kwangu nikimkuta sebuleni nacheka tu-ni WASAFI kama pet)
Nguruwe wanahitaji usimamizi wa karibu sana, uwajue kwa namba ili uweze kufuatilia maendeleo yao kila asubuhi. Ukiona mnyama mmoja amezubaa mwite doctor haraka sana. usiachie wasaidizi kila kitu, kuwa makini na kuhakikisha wanapata milo miwili ya kutosha bila kusahau vegs. nguruwe wanapenda maji-usiwanyime starehe ya kwa kuwabananisha hawatanenepa vya kutosha. Nguruwe ana uwezo wa kuzaa mara mbili kwa mwaka. Mimi sijasoma kilimo na mifugo, ni ubishi tu na kuthubutu vilivyoletwa na maisha magumu. MUHIMU UKUBALI KUKAA SHAMBA, JF UIPATE KWA TTCL NA SOLLAR!
Naomba number yako ya kwangu ni 0767164257
Naweza pata number yako na unafugia wapi ya kwangu ni 0767164257, kwani nataka kuaanza kufuga maeneo ya Tanga nina ekari kama 50 hiviKwa kuwa nna uzoefu wa kuendesha mradi wa nguruwe kwa mafanikio,watu wengi huulizia watoto wa nguruwe(piglets) kwa ajili ya kuanza mradi huo.Lakini hiyo sio namna nzuri kiuchumi.Namna sahihi kama unataka kifuga kibiashara ni kuanza na nguruwe wenye mimba!
SOMA HAPA UELEWE!Tutazungumzia chakula hapa kwa kuwa ndio gharama kubwa!
1.ukianza na piglet wa wiki 8,utamnunua kwa 60,000,
-week 4 za mwanzo atakula wastani wa 1kg/siku.Chukulia chakula 300/kg then jumla itakuwa =4x7x1x300=8,400
-kama utampandisha around week 28,week 20 atakula wastani wa 2kg/siku.jumla =20x7x2x300=84,000
-Atabeba mimba kwa siku 114.gharama ya chakula jumla=114x2x300=68,400
-atanyonyesha kwa week8.gharama ya chakula 8x7x6x300=100,800
Jumla kuu ya gharama ya piglet na chakula=261,600
Hii ni baada ya wiki 48(almost mwaka) ndio utaweza kuuza piglets wako wa mwanzo.akizaa 6 say na ukauza wote utapata 360,000
2.ukianza na nguruwe mwenye mimba ya wiki 8 uzao wa kwanza kwa 300,000
-utalea mimba kwa siku 58,gharama ya chakula=58x2x300=34,200
-gharama ya chakula wiki8 za kulea watoto=8x7x6x300=100,800
Jumla kuu ya gharama-435,00
Utaweza kuuza piglet wa kwanza ndani ya wiki 16(miezi4).
Kama umeelewa ndani ya wiki 40 tangu umenunua atakuwa amezaa mara 2 .gharama ya chakula itakuwa ni 304,200.Kama uzao wa kwanza majike uliwalea watakuwa tayari wamebeba mimba.
Gharama ya chakula kwenye mradi ndio kubwa,80%ya gharama zote.Ina maana ukitafuta namna ya kupunguza gharama ya chakula ndipo faida yako inaongezeka
Hakuna Nguruwe anaechinjwa.nguruwe anachukua miezi mingapi toka kuzaliwa mpaka kufaa kuliwa au kufaa kuchinjwa nyama ?
Hakuna Nguruwe anaechinjwa.
Wakitaka kuua wanapiga Nyundo kichwani. Anamwaga uharo biashara imekwisha.
Ndio ujue sasa .Kumbeee .... hata sisi hatujui lakini wewe wajua
Hongera sana mkuu, sasa hakikisha kuwa haufugi kama alivyokuwa akifuga mzee wako. Wewe fuga kisasa mpaka mzee wako ajisikie raha kukupeleka shule. Unaweza kufunga drinkers za kisasa ili kurahisisha ufugaji wako wa nguruwe na kuwafanya wawe na afya bora, tunapatikana Dar lakini kama upo mkoani tutakuagizia kwa gharama zetu. Piga simu namba: 0625504952..ufugaji wa nguruwe unalipa sana.
mimi nimeanza na watoto kumi mwaka huu,nimeiga huu ujasiriamali,mzee alikuwa anafuga tokea enzi ya ujana wake,katusomesha wote mpaka vyuo vikuu kwa huu ujasiriamali,asante sana mtoa uzi nazidi kujifunza mengi kwa huu uzi,ubarikiwe sana.
Karibu sana mkuu..okey..nipo mkoani k'njaro..ntakucheck..shukrani.!
Habari wapendwa
Samahan naomba kujua ufugaji wa nguruwe, malazi yao na matibabu yao.
Pia na ufugaji wa kuku wa kienyeji yaani jinsi ya kumnyang`anya vifaranga,na je nifanye hivo vikiwa vina umri gani?
Naitwa Moi Mwakye kutoka Mbeya.